Thursday, January 15, 2015

Nanasi ni Matunda bora kwa afya

Soko Kuu  la Kariakoo lililopo Jijini Dar Es Salaam hupokea kila aina ya mazao. Katika picha hapo juu ni mananasi amabayo tayari yamefikishwa katika soko hili maarufu hapa Jijini Dar es Salaam. Mananasi haya huuzwa kwa bei ya jumula na rejareja sokoni hapo.

Nyanya zapanda bei sokoni

Mvua nyingi zinazoendelea katika mikoa maarufu ya uzalishaji nyanya imesababisha bei ya nyanya kupanda bei katika Soko Kuu la Kariakoo kwa  nyanya grade ya kwanza.
Nyanya nyingi huingizwa katika Soko Kuu la Kariakoo kutoka mikoa ya Iringa,Njombe,Mbeya,Morogoro na Arusha.