Monday, June 8, 2015

MKUTANO MKUU WA 2SEEDS Network KOROGWE

 Katika picha ni  sehemu tuu ya Wanamtandao wa 2SEEDS Network ambao walihudhuria mkutano huo maalum ambao hufanyika kila mwaka kwa ajili ya kutathimini maendeleo ya miradi mbalimbali ya uzalishaji mali ikiwamo ya kilimo na ufugaji. 2SEEDS Network ni Shirika lisilokuwa la Kiserikali ambalo makao yake makuu yapo katika Jiji la Washington  nchini Marekani,shirika hili limekuwa likifanya juhudi za kuboresha maisha ya wakulima wadogowadogo kwa kuwasaidia kuibua miradi tofautitofauti kulingana na mazingira wanayoishi na kuisimamia kwa karibu sana kwa kushirikiana na Wanavijiji huku wakiwasaidia kupata elimu ya Ujasiriamali.

 Sehemu ya Wajumbe ambao ni Wanamiradi husika wakiwa wamekaa ndani ya Ukumbi wa kanisa la Anglican uliopo nje kidogo  ya mji wa Korogwe,huku wakiendelea kufuatilia mambo yaliyokuwa yamejiri katika mkutano huo mwishoni mwa wiki iliyopita
 Wanamtandao wakifanya mjadala kuhusu miradi wanayoiendesha katika vijiji tofauti wakati wa mkutano wa mwaka ulipofanyika siku ya Jumamosi ya tarehe 6/6/2015 wilayani Korogwe.
Mkurugenzi Mkuu wa 2SEEDS Network hapa nchini Tanzania kama anavyoonekana katika picha hapo juu Bi.Ana  Le Rocha akifafanua jambo wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka. Mkutano huo ulifanyika wilayani Korogwe mkoani Tanga mwishoni mwa wiki iliyopita. Mkutano ulikuwa unafanya tathimini juu ya miradi mbalimbali ambayo inaendelea katika maeneo mbalimbali katika vijiji vilivyomo ndani ya wilaya ya Korogwe Vijijini.