Saturday, September 6, 2014

Hafla ya kukabidhi vyeti kwa Wafanyakazi bora

 Katika picha hapo juu ni Meneja Utumishi na Uendeshaji katika Shirika la Masoko ya Kariakoo Bwana Godwin Mrosso anayepiga makofi mara baada ya kumkabidhi cheti maalum cha ufanyakazi bora Bibi Romana Lukanga  aliyeshika cheti,na aliyesimama katikati ni Bwana Joseph Mweyo ambaye ni Mwenyekiti wa TUICO katika Shirika la Masoko; na ambaye ameshika bahasha kulia kabisa ni Bibi Ester Chogero yeye ni Katibu wa TUICO hapa katika Shirika la Masoko.Meneja Utumishi alimuwakilisha Meneja Mkuu wa Shirika Bwana Florens Seiya ambaye alikuwa na shughuli zingine za kiofisi.Hafla hiyo ilifanyika jana mchana katika Ukumbi wa mikutano wa Shirika.
 Katika picha hapo juu ni Bibi Primitiva  Kamugisha  Kaimu Meneja wa Idara ya Usafi akipokea cheti cha Ufanyakazi bora kwa niaba ya Mtumishi wa Idara yake ambaye hakuwepo katika hafla hiyo hapo jana.
 Aliyesimama ni Bibi Romana Lukanga akitoa shukrani kwa Uongozi wa Shirika  kwa niaba ya Wafanayakazi bora waliotunukiwa vyeti,pamoja na shukrani lakini pia aliwasisitiza wafanyakazi wenzake waliopata vyeti hivyo kuwa wasibweteke nakuona kuwa wameshashinda bali inawapasa kuongeza bidii katika utendaji wao wa kazi ili wazidi kuwa mfano mara kwa mara katika Shirika.
 Katika picha hapo juu aliyesimama ni Meneja wa fedha katika Shirika la Masoko Mrs.Marieta Massaua akitoa  pongezi kwa Watumishi wa Shirika walioshinda na kuwa Wafanyakazi bora katika Shirika.Hafla hiyo iliyofanyika jana mchana katika Ukumbi wa Mikutano wa Shirika.
Bwana Ibrahim Masha akiwa amesimama kutoa nasaha kwa Watumishi wa Shirika waliohudhuria hafla ya kukabidhi vyeti kwa Wafanyakazi bora wa Shirika kwa mwaka 2012/2013.Hafla hiyo ilifanyika jana mchana katika Ukumbi wa Mikutano wa Shirika. Bwana Ibrahim Masha yeye ni Mjumbe wa halmashauri ya TUICO ngazi ya Taifa.