Saturday, October 5, 2013

ULINZI KATIKA SOKO LA KARIAKOO WAIMARIKA



Shirika la Masoko ya Kariakoo limeimarisha ulinzi katika eneo zima la Soko ili kuhakikisha Soko linakuwa katika hali ya usalama wa uhakika wakati wote, Hii ni kutokana na watu wengi wa kutoka maeneo mbalimbali kufika katika Soko hili kuweza kujipatia huduma. Katika ulinzi huo umehusisha askari wa Shirika la Masoko ya Kariakoo pia askari wa Jeshi la Polisi ambao hawako katika sare rasmi hayo yalisemwa na Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo Bw. Florens M. Seiya wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari walipomtembelea Ofisini kwake mapema wiki hii.