Monday, June 16, 2014

Madiwani kutoka Halmashauriya Manispaa ya ILALA walipotembelea Soko Kuu la Kariakoo Alhamisi wiki iliyopita

 Katika picha hapo juu ni Bwana Edson Fungo ambaye aliongoza Ujumbe wa Madiwani kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kufika katika Ofisi za Shirika la Masoko ya Kariakoo Alhamisi wiki iliyopita. Ujumbe huo ulifika kukagua maumbo ambayo yatatumika na Wafanyabiashara wa eneo la Soko la Wazi
Meneja Mkuu wa Shirika Bwana Florens Seiya mwenye kitabu mkononi na Bwana Edson Fungo wakielekea eneo la Soko la Wazi katika viwanja vya Shirika la Masoko ya Kariakoo.
 Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo  aliyeshika kitabu mkononi akiwaeelezea jambo Waheshimiwa Madiwani katika eneo la Soko la Wazi katika viwanja  vya Shirika la Masoko ya Kariakoo.
 Hapa kwa makini kabisaa Madiwani wakimsikiliza Meneja Mkuu wa Shirika Bwana Florens Seiya ambaye amenyoosha mkono.Hapa alikuwa akitoa ufafanuzi kuhusu uzito unaoruhusiwa kuwa juu ya eneo hilo  linalotenganisha jengo kuu la Soko na Soko Dogo, ambalo linakusudiwa kutumika kwa Wafanyabiashara kufanya biashara zao kama ilivyokuwa mwanzo.
 Hapa ziara ya kutembelea viwanja vya Shirika ilikuwa ikiendelea sehemu hii hapa ni upande wa ambako liko lango kuu la kutokea eneo la Shimoni.Meneja Mkuu wa Shirika Bwana Florens Seiya na Bwana Edson Fungo Mkuu wa msafara wa Madiwani wakiwa wametangulia mbele.
 Hapa ni Meneja Mkuu wa Shirika Bwana Florens Seiya amabye ameshika kitabu akifafanua jambo kwa  Waheshimiwa Madiwani wa kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala walipotembelea Soko Kuu la Kariakoo na kufanya kikao cha kujadili namna ya kuwarejesha  Wafanyabiashara waliokuwa wakifanya shughuli zao katika eneo la Soko la Wazi; sambamba na kikao hicho walikagua maumbo ambayo yatatumika katika viwanja hivyo vya Shirika kupangia bidhaa mbalimbali.
 Katika picha hapo juu Wajumbe wa mkutano wakirejea katika Ukumbi wa mikutano wa Shirika la Masoko baada ya kutembelea maeneo ya viwanja vya Shirika na kupata maelezo jinsi Wafanyabiashara watakavyopangwa ili kurejea kufanya biashara katika eneo la Soko la Wazi.Waliotangulia mbele kutoka kulia ni Bwana Edson Fungo ambye aliongoza Ujumbe wa Madiwani toka Manispaa ya Ilala katika ziara; anayefuata ni Meneja Mkuu wa Shirika Bwana Florens Seiya na mwenye shati la draft ni Afisa usalama wa Shirika Bwana Moringe
Hii ni sehemu tuu ya Wajumbe wa Kikao maalum cha Madiwani na  kutoka manispaa ya Ilala  na Uongozi wa Shirika la Masoko ya Kariakoo wakiwa katika majumuisho mara baada ya kutembelea maeneo ya viwanja vya Shirika.