Monday, May 26, 2014

Soko Kuu la Kariakoo na umri wake wa miaka 40

 Soko Kuu la Kariakoo ambalo linasimamiwa na Shirika la Masoko ya Kariakoo (SMK) tangu mwaka 1974; kwa mujibu wa Sheria Na.36 ya Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.Shirika hili itakapofika tarehe 8/12/1914 litakuwa linatimiza miaka 40 tangu Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius K.Nyerere alipofungua rasmi shughuli za uendeshaji wa Shirika hili hapo tarehe 8/12/1974.
Kila mahali huwa na taratibu zake za kiutendaji katika kusimamia watu,katika picha hapo juu utaona baadhi ya askari wa Shirika wakiwa katika ukaguzi wa mpangilio wa bidhaa ambazo wafanyabiashara hupanga katika maeneo yao tofauti na taratibu za Shirika.Wafanyabiashara hawa wakati mwingine baadhi yao huvuka alama za mistari ambayo imechora kuwaonesha mipaka ya  sehemu zao; hivyo hulazimika maaskari hawa kufanya operesheni ya kukagua maeneo mbalimbali ili kuwarekebisha wale wanaokuwa wamekiuka utaratibu huo wa upangaji bidhaa zao.

Kutoka Sokoni Kariakoo leo!

 Karoti na Pilipili Hoho pamoja na mboga  mbalimbali  za majani hupatikana katika Soko kuu la Kariakoo kwa wingi sana kila siku. Lakini bidha hizi zote zipo katika viwango vya hali ya juu katika ubora kwa mlaji kwa kuzingatia mazingira bora ya Soko la Kariakoo llilopo hapa Jijini Dar es Salaam-Tanzania.
Nyanya kutoka Iringa zinaingia katika Soko Kuu la Kariakoo kila siku katika majira haya. Nyanya hizi kutoka mkoani Iringa huanza msimu wa mwezi Mei na kuendelea; zina ubora wa kipekeee sana katika matumizi.Sasa usikose kujipatia bidhaa hii bora fika Kariakoo Sokoni eneo la Shimoni ambapo utaweza kupata kwa bei ya jumula na rejareja kwa kadiri ya mahitaji yako iwe ya familia au biashara. Karibu sanaaaa!