Friday, October 25, 2013

BEI YA VITUNGUU YASHUKA SOKONI KARIAKOO, KUTOKA Sh 150,000/= HADI Sh. 70,000/= KWA GUNIA

Pichani ni magunia ya vitunguu yaliyopo katika soko Kuu la Kariakoo Jijini Dar es Salaam, vitunguu sokoni Kariakoo vimeshuka bei hadi kufikia bei kati yaSh. 800/= na 1,000/= kwa kilo, ambapo gunia la vitunguu kwa sasa linauzwa Sh. 70,000/=  kutoka Sh. 150,000/=

Mtakwimu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo Ndugu Henry Rwejuna akiwa na Mratibu wa Mradi wa Masoko Monique Galvao wakiendelea na shughuli zao katika moja ya maeneo ya kuuzia vitunguu Sokoni Kariakoo Jijini Dar es Salaam mapema leo asubuhi.


Pichani hapo juu ni mfanyabiashara wa Soko Kuu la Kariakoo ambae jina lake ni Jackson Atanas Kibwe akipanga vitunguu katika meza yake ya biashara Sokoni Kariakoo. Jackson ambae ni mfanyabiashara maarufu sokoni hapa anapatikana kwa mawasiliano yafuatayo; 0712 834355

Shaban Muhud Saro (kulia) akiwa na watumishi wa Shirika la Masoko ya Kariakoo mapema leo asubuhi, ambapo Mtakwimu wa KMC alipofika mezani kwake. Shaban Muhud Saro ambaye pia ni mfanyabiashara wa vitunguu Sokoni Kariakoo amelipongeza Shirika la Masoko ya Kariakoo kwa kuanzisha mtandao wake ambao utasaidia kutoa taarifa mbalimbali zinazopatikana sokoni Kariakoo. Lakini pia Shaban Muhud Saro ametoa mawasiliano yake kwa yeyote atakaye hitaji huduma yake anapatikana kwa simu 0655 358343 au 0688 943368

Karibuni ujipatie vitunguu Sokoni Kariakoo