Thursday, October 10, 2013

YALIYOJILI LEO SOKONI KARIAKOO!!

Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo, Ndugu Florens M. Seiya, akiongoza mkutano wa  Menejiment ya Shirika la Masoko ya Kariakoo leo,ikiwa ni moja ya  mikutano ya asubuhi ya kawaida ambayo hufanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Shirika. Mikutano ya namna hii hufanyika mara mbili katika wiki  ikiwa na lengo la kujadili na kutathimini utendaji kazi.


katika picha hapo juu ni Meneja wa fedha Mrs.Marieta Masaua akiwasilisha taarifa ya mapato ya Shirika,kushoto kwake ni Afisa Biashara Muandamizi wa Shirika la Masoko ya Kariakoo Bi.Daynes Sooi


Bwana Marco Mganga , Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi akifuatilia kwa makini maelezo ya Meneja wa fedha mapema leo asubuhi katika mkutano ambao ulifanyika katika ukumbi wa mikutano.

Menejimenti ya Shirika la Masoko ya Kariakoo ikiwa katika mkutano wake wa kawaida leo asubuhi! Mkutano ulifanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Shirika la Masoko.



Bi.Kamugisha  Mkuu wa kitengo cha Usafi katika Shirika la Masoko ya Kariakoo akifuatilia jambo katika  mkutano wa asubuhi mapema leo asubuhi.

Bi.Primitiva Kamugisha Mkuu wa Kitengo cha Usafi katika Shirika la Masoko ya Kariakoo akiwa katika mkutano wa kawaida wa Menenjimenti wa asubuhi , kulia kwake  ni Bi. Gloria Kalabamu  Mkuu wa Kitengo cha sheria Shirika la Masoko.

NJOO KARIAKOO UJIPATIE SAMAKI WABICHI.


 Pichani ni mfanya biashara maarufu wa samaki anayejulikana kwa jina la Bw Ramadhani Mlekwa anayefanya shughuli zake katika Soko kuu la Kariaoo. samaki wanaoonekana pichani ni aina ya "King fish"


 Mteja akihakiki uzito wa samaki aliyemnunua  kwa kupima katika mizani.Samaki hawa wanapatikana Sokoni kariakoo.


Baadhi ya wateja waliofika leo  kununua samaki ndani ya Soko Kuu la Kariakoo kama inavyoonekana
pichani.Sokoni Kariakoo kila bidhaa hupatikana  kuanzia  Nafaka,Matunda,Viungo,Mbogamboga,Samaki na nyama


 Wafanya biashara wa Shirika la Masoko ya Kariakoo wakiuza bidhaa zao kama inavyoonekana pichani, katika soko la wazi. katika vipimo vya lita nne maarufu kama sado.Nyanya zinauzwa kati ya Sh.2000/= hadi Shilingi 3000/=kwa bei ya leo kwa sado



Biashara ya nyanya, karoti,hoho na nyinginezo mbalimbali hufanyika katika  Soko kuu la  Kariakoo kwa bei za rejareja na jumla. Katika hapo juu ni moja ya wafanya biashara mashuhuri sana hapa Sokoni akiwa katika meza yake! Karibuni wote mjipatie bidhaa safi na bora!!









Mawasiliano katika biashara ni mhimu! mama ambaye jina lake halikupatikana mapema akipanga bidhaa zake katika meza ya biashara huku akiwasiliana  na wateja wake kama anavyooneakana katika picha.


Kitengo cha Usalama katika Shirika la Masoko ya Kariakoo



Katika picha hapo juu ni  mtuhumiwa wa wizi wa simu akiwaamekula pingu baada kutiwa mbaroni kwa tuhuma ya kuhusika katika wizi wa simu.Hapo anasubiri kuhojiwa na Afisa muandamizi wa Usalama
.

Katika picha hapo juu ni  mtuhumiwa wa wizi wa simu akiwa chini ya ulinzi mkali wa askari wa usalama wa Shirika la Masoko ya Kariakoo. (Jina lake limehifadhiwa)