Friday, February 21, 2014

Habari za leo kutoka Shirika la Masoko ya Kariakoo Jijini Dar Es Salaam-Tanzania


 Katika picha hapo juu ni Wajumbe wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Shirika la Masoko Kariakoo ambacho kimefanyika leo Ijumaa tarehe 21/2/2014 katika ukumbi wa mikutano wa shirika hilo.
 Wajumbe wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi  wakimsikiliza Meneja Mkuu wa shirika la Masoko ya Kariakoo yeye kama Mwenyekiti wa kikao hicho alipokuwa akiongoza leo Ijumaa tarehe 21/2/2014.
 Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya kariakoo Bwana Florence  Seiya akifafanua jambo wakati wa kikao cha baraza la Wafanyakazi katika shirika la Masoko Kariakoo-(SMK); kwa kawaida kikao hiki huhudhuriwa pia na Mjumbe mmoja wa TUICO kutoka  Ofisi kuu ya TUICO mkoa.
 Katika picha hapo juu  ambaye amesimama na kunyosha mkono ni Katibu Mkuu wa TUICO kutoka mkoa wa Ilala DSM akiwaaga wajumbe wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi; mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho.
Katika hapo juu ni Katibu wa TUICO toka mkoani Ndugu Willy Kibona  katikati;akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa TUICO katika Shirika la Masoko ya Kariakoo, Bibi Ester Chogero Katibu na Bwana Ncheye Kulwa ambaye ni Mjumbe wa TUICO katika Shirika
Mzee Rashid Nguyu (Mfanyakazi wa Shirika)akiwa katika kikao cha baraza la wafanyakazi  akiwa amepozii akifuatilia  maelezo ya Meneja Mkuu  pichani hayupo, pembeni yake katika kiti ni kabrasha lake alilokuwa amepewa siku (3) kabla ya kikao hicho.