Tuesday, April 1, 2014

Kutoka Kariakoo Soko Kuu leo

 Soko Kuu la Kariakoo lililopo Jijini Dar Es Salaam ni kubwa siyo  tuu Tanzania hapa; bali katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati.Hii hapa katika picha ni sehemu tuu ya Soko hili ambayo imejengwa katika mfumo wa Handaki  kuingia kwenda katika sehemu ya Soko la Jumla maarufu kama Shimoni.Magari ya mizigo huingia Shimoni kwa kupitia njia hii kwenda kushusha bidhaa ma mbalimbali kavile Matunda,Viazi,Ndizi na nyinginezo nyingi.
Usalama wako wewe na mali zako Mteja au Mfanyabiashara uwapo  Soko kuu la Kariakoo lililopo Jijini Dar Es Salaam siyo wa kutafuta! Ulinzi ulioimara na madhubuti kabisa upo. Kama uonavyo mwenyewe katika picha hapo juu ni moja ya Maafisa waandamizi wa Usalama wa Shirika la Masoko Kariakoo akiwa na Radio Call yake mezani ambayo hutumika katika harakati za kuhakikisha usalama upo sokoni.Bwana Beatus Moringe ni mtu mwenye uzoefu wa muda mrefu katika masuala ya usalama.

USAFI NI SEHEMU YA MAISHA YETU SOKO KUU LA KARIAKOO

Shirika la Masoko ya Kariakoo (SMK), huzingatia sana suala zima la Usafi katika maeneo yake kila siku. Katika picha hapo juu ni Gari mojawapo kati ya mengi likiwa eneo la Shimoni likiwa linapakia takataka; hufanya kazi ya kuondoa takataka zinazozalishwa Katika Soko Kuu la Kariakoo kutokana na uingizwaji wa bidhaa mbalimbali toka mikoani.Magari haya hufanya kazi Usiku na Mchana ili kuhakikisha eneo la Soko  Kuu la Kariakoo linakuwa safi muda wote.
Katika picha hapo juu ni Bwana Seifu Abdalah ambaye  ni Mtumishi wa Shirika la Masoko kutoka katika Idara ya Usafi,alikutwa eneo la Shimoni akikagua mifereji ya Majitaka inayopita eneo hilo ili kuhakikisha Mfumo mzima wa maji taka upo sawa sawa.Kutokana na umuhimu wa Mfumo huu wa majitaka katika miundombinu ya Soko hili ukaguzi kama  huu hufanyika kila siku na mara kwa mara.