Thursday, May 29, 2014

Kuna nini Kariakoo Sokoni asubuhiiiii?

 Maembeee! karibu upate maembe ya kila aina yanayozalishwa hapahapa nchini kutoka mikoa ya Tanga,Moro na kwingineko! Karibu sanaa! Matunda ya kila aina huuzwa eneo la Shimoni ndani ya Soko Kuu!
Mratibu wa Masoko Project Bi.Monique Galvao wa 2SEEDS Network na Mrs.Romana Lukanga wakiwa katika pozi  la pamoja mara baada ya maelekezo mafupi namna ya kutumia Smartphone wakati wa kutuma bei za mazao kwenye Mfumo wa taarifa wa Shirika la Masoko(KMC Database System) katika ofisi za Shirika la Masoko.

Kariakoo Market Corporation na 2Seeds Network

Katika picha hapo juu ni Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kariakoo wakiwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa 2SEEDS Network hapa nchini Tanzania Bi.Anna mwenye miwani kulia alipowatembelea wafanyabiashara hapo katika eneo la Soko la jumla  maarufu kwa jina la  Shimoni.Mfanyabiashara aliyesimama karibu naye ni Bwana Munguatosha Mtui yeye ni Mfanyabiashara maarufu wa Karoti na Pilipili hoho.
Katika Picha hapo juu ni Wajumbe wa Menejimenti ya Shirika la Masoko wakiongozwa na Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko Bwana Frolens Seiya wa pili kutoka kushoto na wa kwanza kushoto ni Bwana James Meeks ambaye ni Mwenyekiti wa 2Seeds Network toka nchini Marekani. Hapa ni mara baada ya mkutano uliokuwa ukifanya tathimini ya maendeleo ya Mradi wa Masoko;katika mkutano huo Viongozi Wakuu wa  2SEEDS Network walihudhuria kutoka Marekani.Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Shirika la Masoko.
Mkuu wa Kitengo cha ICT katika Shirika la Masoko ya Kariakoo Bwana Anderson Shaka akiandikisha jina katika kitabu cha Wageni katika Ofisi za Makao  Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). Bwana Anderson Shaka aliambatana na Mratibu wa Masoko Project  Bi.Monique Galvao pichani hayupo; walifika katika Ofisi hiyo kurejesha Fomu ya maombi  ya kununua namba maalum (SHORT CODE) kwa ajili ya Shirika la Masoko ya Kariakoo itakayotumika kwa ajili ya kutoa Taarifa za bei halisi za mazao ambayo huuzwa katika Soko Kuu la Kariakoo.

Mtumishi wa TCRA Bwana Lumumba akiwa anachukua  taarifa mhimu kutoka katika Fomu ya maombi iliyowasilishwa kwa ajili hatua za awali za usajili ili kununua ShortCode kwa ajili ya matumizi ya Shirika la Masoko ya Kariakoo.Aliyesimama ni Bwana Anderson Shaka Mkuu wa Kitengo cha ICT kutoka Shirika la Masoko ya Kariakoo Jijini Dar Es Salaamu,ambaye aliambatana na Bi.Monique Galvao Mratibu wa Masoko Project kutoka 2SEEDS Network.

Mkuu wa Kitengo cha ICT katika Shirika la Masoko ya Kariakoo Bwana Anderson Shaka akifafanua jambo kwa moja  ya Viongozi  wakuu  aliyevaa T-Sheti nyeusi wa Shirika lisilokuwa la Kiserikali liitwalo SEEDS Network lenye makao yake makuu nchini Marekani. Viongozi hawa walifika katika Soko Kuu la Kariakoo kukagua maendeleo ya mradi ambao unatekelezwa kwa ushirikiano baina ya Shirika la Masoko ya Kariakoo (SMK) na 2SEEDS Network,wenye lengo lakuwawezesha Wakulima na Wafanyabiashara wa mazao mbalimbali kupata bei halisi za mazao kutoka Soko Kuu la Kariakoo  kwa njia ya Mtandao kupitia Simu zao mkononi.