Thursday, April 10, 2014

Matumaini mapya kwa Wafanyabiashara Sokoni Kariakoo!

 Katika picha hapo juu ni jopo la Wakaguzi wa ndani wa Shirika la Masoko ya Kariakoo wakiangalia ubora wa maumbo amabayo yaliletwa katika Ofisi za Shirika  jana.Maumbo hayo yakiisha kuthibitishwa yataanza kutumika katika eneo la Soko la Wazi lililopo kati ya Jengo Kuu la Soko na Soko Dogo ambapo Wafanyabiashara  watayatumia kupanga bidhaa zao mablimbali humo na kuwauzia wateja.Wakaguzi hao wakiongozwa na Mkuu wao Bwana Paul Kiwera aliyevaa kitambulisho kutoka kulia, Bwana Ncheya Kulwa na Bwana Longino .A.k.a Mkulu wa Bangoye!
Katika picha hapo juu ni "Sampo"(sample) ya maumbo ambayo yanatarajiwa kutumiwa na Wafanyabiashara ambao mapema wiki  iliyopita walibomolewa meza zao katika eneo la Soko la  Wazi la Kariakoo.Eneo hilo ni sehemu ya Kiwanja cha Soko Kuu la Kariakoo. Wafanyabiashara hao watakuwa wanatumia maumbo hayo kupanga bidhaa zao mabalimbali wanazoziuza sokoni hapo.

Ziara ya Meneja Mkuu wa Shirika pamoja na Timu yake ya Menejimenti ya Shirika.

 Meneja Mkuu akipata maelezo kutoka kwa Muhandisi wa Shirika Bwana Flavian Mlellwa wakati wa ziara ya kuzungukia maeneo ya Soko kuu la Kariakoo mapema leo asubuhi.Meneja Mkuu Bwana Florens Seiya aliambatana na Wakuu wa Idara na Vitengo ambao wote kwa pamoja huunda Menejimenti ya Shirika. Kutoka Kushoto aliyeshika Radio Call ni Mkuu wa Kitengo cha Usalama Bwana Mzava,anayefuata ndiye Meneja Mkuu,anayetoa maelezo ni Mkuu wa Kitengo cha Matunzo(Muhandisi),na wengine ni Meneja wa Fedha Mrs. Marieta Masauwa na Bi.Dainess Sooi anayekaimu nafasi Meneja Mipango na Biashara .
 Mfanyabiashara wa Mbogamboga katika eneo la Soko dogo akiongea na Meneja Mkuu wa Shirika kama alivyokutwa na leo asubuhi katika eneo lake la biashara.
 Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko Bwana pamoja Menejimenti yake wakiwa wanapokea maelezo kutoka Mfanyabiashara akielezea jinsi ambavyo huwa wanapanga bidhaa zao katika eneo hilo. Hapo katika eneo la Soko dogo.
 katika picha hapo juu ni Kisima cha Maji ambacho kinamilikiwa na SMK kipo katika eneo la Soko Dogo. Wiki iliyopita kilikuwa kimeharibiwa kwa kuvunjwa Pampu yake wakati wa bomoabomoa.Ndugu msomaji kama unavyoona katika picha kisima hicho kimefanyiwa ukarabati na Kitengo cha Uhandisi cha Shirika la Masoko na hatimaye kuanza kutoa huduma ya maji tena.

 Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko aliyetangulia mbele akiwa anarejea Ofisini kwake leo asubuhi mara baada ya kuzungukia maeneo mbalimbali ya Soko Kuu la huku akiwa ameambatana na Menejimenti yake.
Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo  Bwana Florens Seiya akifanya majumuisho ya ziara alioifanya ya kuangalia na kuzungumza na baadhi ya Wafanyabiashara ambao hufanya biashara zao katika maeneo kadhaa ambayo yalikumbwa na bomoabomoa ya Manispaa wiki iliyopita. Majumuisho hayo aliyafanyia Ofisini kwake leo asubuhi baada ya ziara aliyokuwa ameambatana na Wajumbe wa Menejimenti ya Shirika.

Habari katika Picha toka Shirika la Masoko ya Kariakoo

Hii ni sehemu ya Wajumbe waliohudhuria Mkutano wa dharula ulioitishwa na Chama cha Wafanyakazi TUICO ili kupeana taarifa za mstakabali wa yaliyotokea na hatua zilizochukuliwa na Uongozi wa Shirika la Masoko ya Kariakoo.Pia katika mkutano huo Uongozi wa TUICO uliwakumbusha Watumishi wa Shirika kuwa na mshikamano wa pamoja ili kuona kuwa Shirika likzidi kupiga hatua kimaendeleo.
 Kutoka kulia ni Katibu wa TUICO katika Shirika la Masoko ya Kariakoo Bibi Ester Chogero,Bwana Joseph Mweyo Mwenyekiti wa TUICO ,na Bwana Ibrahimu Masha amabaye ni Mjumbe wa TUICO Taifa kutoka Shirika la Masoko ya Kariakoo. Wote kwa pamoja wakiendesha Mkutano a Wafanayakazi jana mchana. Mkutano huo ulilenga kujadili Agenda kuu mbili tuu ikiwamo Mwenendo mzima wa Watumishi wa Shirika pamoja na Kuwajulisha Wafanyakazi kuhusu zoezi la bomoabomoa amabalo ililikumba  Shirika wiki iliyopita.
 Aliyesimama ni Katibu Mkuu wa TUICO  Bibi Ester Chogero akisoma waraka maalum sana amabao ulihusishwa na  moja ya agenda muhim zilizojadiliwa katika Mkutano huo wa dharula ulioitishwa na Uongozi huo wa TUICO.
 Viongozi wa TUICO tawi la Masoko ya Kariakoo wakishauriana jambo na Wajumbe wa Menejimenti ya Shirika la Masoko ya Kariakoo. Hii ilikuwa ni jana Jumatano ilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Shirika hilo.
Wafanyakazi wa Shirika la Masoko ya Kariakoo wakitoka nje baada ya mkutano wa Dharula ulioitishwa na Chama cha Wafanyakazi TUICO Tawi la Masoko.Mkutano huu ulifanyika jana Jumatano tarehe 9/4/2014 mchana.