Tuesday, May 27, 2014

Sample za Maumbo yatakayotumika katika Soko la Wazi

 Katika picha ni "sample" ya maumbo ambayo yanatarajiwa kutumika Sokoni Kariakoo katika Soko la Wazi ambapo kwa sasa hapajaanza kutumiwa na Wafanyabiashara tangu Manispaa ya Ilala walipovamia na kubomoabomoa meza zilizokuwa zinatumiwa na Wafanyabiashara hao mapema mwanzoni mwa mwezi wa Aprili 2014.Waliosimama na kuziangalia ni Afisa Biashara  Bwana Vedastus Valentine mwenye shati la bluu na Mhandisi wa Shirika Bwana Flavian Mlelwa.
Wafanyabiashara watakuwa wanapanga bidhaa zao humu katika Maumbo haya na kuwauzia Wateja, Maumbo haya yanakusudiwa kuanza kutumika katika eneo la Soko la Wazi katika Viwanja vya Shirika la Masoko ya Kariakoo katika siku chache zijazo mara baada ya taratibu zote kukamilika.

Karibuni Kariakoo Soko Kuu-Jijini Dar-Es Salaam

 katika picha hapo juu ni Katibu Muhtasi  katika Ofisi ya Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo Mrs.Grace Kahatano,kama alivyokutwa Ofisini kwake akiendelea na shughuli zake.
 Shirika la Masoko la Kariakoo lina Idara nyingi mabalimbali, katika Picha hapo juu ni Afisa Biashara Bwana Vedastus Valentine aliyekaa na Mtakwimu wa Shirika la Masoko Bwana Henry  Rwejuna wakiwa ofisini wakijadiliana jambo; wote hawa kwa pamoja wapo katika Idara ya Biashara.
Soko Kuu Kariakoo siyo tuu huuza vyakula pekee bali  ndani ya Soko hili kuna maduka mengi sana yanayouza Pembejeo za Kilimo zikiwemo mbolea,madawa ya kuulia wadudu pamoja na mitambo/machine mbalimbali zinazotumika kufanya kazi za Kilimo.katika picha hapo juu muuzaji mojawapo akiwa anaunganisha aina mojawapo ya kupulizia dawa shambani ili aweze kuifanyia majaribio kabla yakumuuzia Mteja wake. Kumbe Kariakoo ni Soko muhimu sanaa kwa kila mmojawetu ikiwa wewe ni Mlaji au Mzalishaji. Karibu sanaa Kariakoo Soko Kuu upate mahitaji yako.