Sunday, March 30, 2014

Mfahamu Mfanyabiashara Mkongwe Sokoni Kariakoo

Mfanya biahara mkongwe katika Soko Kuu la Kariakoo akiwa katika duka lake la bidhaa mbalimbali.Mzee Suleiman Mwaipungu anaelezea kuwa amekuwepo katika mitaa ya Kariakoo akifanya biashara ya vyakula  hata kabla ya Soko kuu la Kariakoo halijajengwa

Huyu ni Mfanyabishara maarufu na wa siku nyingi sana katika Soko Kuu la Kariakoo lililopo Jijini Dar Es Salaam. Mzee Suleiman Mwaipungu amekuwepo katika Soko hili tangu mwaka 1974 lilipoanzishwa.Fika katika Soko dogo umuunge mkono katika biashara zake kwa kununua nafaka kama vile mtama,njegere,choroko,Mchele,Karanga na nyinginezo;pia anauza mifuko kama inavyoonekana katika picha hapo juu.

Friday, March 28, 2014

2SEEDS Network katika Ziara yao Kariakoo

 Katika picha hapo juu ni miongoni mwa Watumishi wa mtandao wa 2SEEDS waliotembelea mapema leo Sokoni Kariakoo.Hapa walikuwa wakipata chakula cha mchana pamoja na mwenyeji wao Bwana Vedastus Valentine ambaye ni Mtumishi wa Shirika la Masoko ya Kariakoo katika Idara ya Biashara.Idadi kubwa ya Watumishi wa 2SEEDS Network huishi Wilayani Korogwe wakifanya shughuli mbalimbali za kiuzalishaji wakishirikiana na Wakulima wadogowadogo kwa lengo la kukuza vipato vya Wakulima hao.
Katika picha  hizo hapo juu ni miongoni mwa Watumishi wa kutoka katika Asasi isiyokuwa ya Kiserikali ijulikanayo kwa jina la 2SEEDS Network yenye Makao Makuu yake nchini Marekani. Leo walikuwa wametembelea Sokoni Kariakoo na kuona maenedeleo ya Mradi ambao wanaufanya kwa ushirikiano na Shirika la Masoko ya Kariakoo.Lakini pia walipata nafasi yakuongea na baadhi ya Wafanya biashara hapo Sokoni.

Thursday, March 27, 2014

Matunda ya kila aina yanapatikana Kariakoo Sokoni.

 Maembe hayo katika picha hapo juu yapo tayari kwa kuuzwa kwa wateja wa jumla na rejareja pia!
Bei yake ni kati ya TSh.500 hadi 700
Katika picha hapo juu ni mifuko ambayo ina matunda aina ya Apples yakiwa yameshushwa toka katika gari mojawapo leo mapema alfajiri. Matunda haya kwa sasa yanatoka katika Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga. Asilimia kubwa ya matunda yanayotoka Lushoto huuzwa katika Soko Kuu la Kariakoo lililopo Jijini Dar Es Salaam.

Wednesday, March 26, 2014

Kariakoo Leo!

 Katika picha hapo juu ni moja ya Magari ya mizigo ambayo huleta  mazao mabalimbali katika Soko la Kariakoo. Hapo lipo ndani katika Soko la Jumla Shimoni, lilikutwa leo alfajiri likishusha Matunda aina ya Apples  toka Lushoto Tanga.
Matikiti haya yanauzwa kwa bei ya Jumula na rejareja Soko kuu la Kariakoo Jijini Dar Es Salaam.Kwa mahitaji  ya matunda kila aina fika Kariakoo Shimoni

Tuesday, March 25, 2014

Hizi ni Green beans ni aina mojawapo mboga nzuri ambazo zinauzwa hapa katika Soko Kuu la Kariakoo Jijini Dar Es Salaam.Huzalishwa katika mikoa ya Arusha na Tanga. Bei yake ni Tsh.3000/= kwa Kilo moja.

Mboga za Majani zinapatikana Sokoni Kariakoo pia!



 Leo ni mbogamboga tuu! ndugu Mteja mboga hizi zinatokea katika mikoa ya Tanga sehemu za Lushoto,Korogwe na kule mkoani Arusha.
Hapo juu katika picha ni mchanganyiko wa mbogamboga  kama vile Zukin hizo zenye muonekano kama matango,Cotmill,Retus na nyinginezo.Hizi zinapatikana Kariakoo sokoni katika eneo la soko wazi.

Thursday, March 20, 2014

Habari toka ndani ya Kariakoo Market Corporation leo

 Katika picha hapo juu ni Wanafunzi wanaosoma kozi ya Uhasibu katika chuo cha 
The Kilimanjaro Institute of Business & Technology  kilichopo Jijini DSM. Wanafunzi hawa wapo katika mafunzo kwa vitendo (PT) katika Shirika la Masoko ya Kariakoo.Hapa wanaelekezwa jambo na Mtumishi mmojawapo wa Shirika mwenye Tsheti nyeupe MrsMwinga. Wanafunzi kutoka kulia ni  Pendo Francis,Libelius Vedastus,Elisamehe Temu na Lipina David.
 Mwanafunzi huyu Elisamehe Temu akiwa anaendelea na shughuli zake mapema leo asubuhi katika Ofisi za Shirika la Masoko ya Kariakoo;hapa alikutwa akifanya moja ya kazi ambayo alipangiwa na msimamizi wake.

Tuesday, March 18, 2014

TANGAZA BIASHARA YAKO KWA BEI NAFUU

Sasa unaweza kutangaza biashara yako katika mtandao wa Shirika la Masoko Kariakoo (www.kariakooblog.blogspot.com) kwa bei nafuu sanaaa kama inavyoonekana pichani hapo juu. Sehemu zote zinazowakilishwa na herufi zinauzwa. Tangazo lako litalipiwa kwa mwezi. Biashara yako itaonekana Dunia nzima!

NB: bei ya matangazo inaweza kubadilika.

Thursday, March 6, 2014

SASD TRADING COMPANY: WAUZAJI WA BIDHAA ZA PLASTIC SOKO KUU KARIAKOO

Pichani hapo juu ni Suleiman Ahmed Dudu akiwa katika ofisi yake iliyopo katika soko Kuu la Kariakoo Jijini Dar es Salaam. Suleiman ni Mkurugenzi wa SASD TRADING COMPANY .Baadhi ya bidhaa zinazo patikana hapa ni P.P rollers & L.D rollers, P.P packet & L.D packet, Printed plastic bag, Food colour & Flavouring Essence.  



Suleiman Ahmed Dudu akiwa kazini kwake


Managing Director Suleiman Ahmed Dudu unaweza kumpata kwa mawasiliano yafuatayo   

0715 303536 au 0784 303536

MATUNDA

Pichani hapo juu ni matunda aina ya maembe yakiwa mezani katika sokoni Kariakoo eneo maarufu kama soko la wazi. Pata maembe safi kutoka kariakoo.