Sunday, June 28, 2015

Soko Kuu Kariakoo Na Wakulima Vijijini

 Soko Kuu la Kariakoo haliishii tuu kupokea mazao yanayofika Sokoni badala yake sasa limekuwa likifanya ziara maalumu kuwatembelea wakulima walioko vijijini hasa katika Wilaya ya Korogwe kwa kuanzia, huku wakishirikiana na 2SEEDS Network shirika lisilokuwa la Kiserikali kutoka nchini Marekani kwa pamoja taasisi hizi mbili zimekuwa zikiwasaidia wakulima katika kuibua na kuendesha miradi mbalimbali ya kiuzalishaji mali, pia Soko  la Kariakoo likiwapa msaada zaidi kwakuwapa kipaumbele katika kupata soko la mazao wanayozalisha. Katika picha hapo juu ni moja ya mashamba ya wakulima hao walioko Korogwe Vijijini.

 Katika picha hapo juu ni Wanamtandao wa 2SEEDS Network wakiwa shambani wakiangalia maandalizi ya shamba yakiendelea. Mratibu wa mradi huo Bwana Cameron mwenye begi mgongoni alifika kijijini Bungu

Katika picha hapo juu ni shamba la mboga aina ya kabichi, shamba hili lipo katika kijiji cha Lutindi juu milimani kabisa Korogwe Vijijini. Mazao haya kwa kiasi kikubwa husafirishwa kuja  kuuzwa katika Soko kuu la Kariakoo Jijini Dar Es Salaam. Kwa ushirikiano wa 2SEEDS Network wakulima hawa wamekuwa wakizalisha kwa bidii mazao mbalimbali kama vile pilipili hoho,karoti,vitunguu maji, conflowers,bitroots n.k

Thursday, June 18, 2015

Mkutano Mkuu wa 2SEEDS Network 2015

 Hapa katika picha Wanamtandao wametawanyika katika vikundi mbalimbali wakijifunza mambo na hatua mbalimbali ambazo miradi imefikia kwa lengo la kubadilishana mawazo, kwa kuzingatia kuwa Mkutano mkuu kama huu ambao huwakutanisha Wanamtandao hawa hufanyika mara moja tuu katika mwaka.
 Wanamtandao wakiwa wamekusanyika katika Mradi wa Masoko (Masoko Project) wakiwa na shauku yakujua jinsi ambavyo shughuli ya ukusanyaji taarifa za bei na kuhifadhiwa katika mfumo wa Kompyuta wa Masoko yaani KMC Database System na baadaye kutumwa kwa wakulima na walaji wa bidhaa.
 Katika picha hapo juu ni Wajumbe  wa mkutano wakutoka katika miradi mbalimbali wakiwa wanamsikiliza Afisabiashara kutoka Shirika la Masoko Kariakoo Bwana Vedastus Valentine akiwaelezea jambo kuhusu mradi wa Masoko ambao kazi yake kubwa ni kujenga Mfumo wa kuhifadhia na kutoa taarifa za bei kwa Wakulima na walaji wa bidhaa mbalimbali za mazao ambazo huuzwa katika Soko Kuu la Kariakoo.
Katika picha hapo juu ni Viongozi (Project Cordinators) wazawa  wa miradi yote nane inayoendelea kwa ushirikiano na Shirika la 2SEEDS Network lenye makao yake makuu  katika Jiji la Washington nchini Marekani. Katika miradi hiyo nane saba ipo katika vijiji vya Bombomajimoto,Kijungumoto,Magoma,Tabora,Kwakiliga,Magoma kwata ,Lutindi hii saba ipo Wilayani Korogwe na Mradi mmoja wa Masoko huu upo katika Soko Kuu la Kariakoo Jijini Dar Es Salaam.

Tuesday, June 16, 2015

Miradi ya Wanamtandao wa 2SEEDS Network

 Katika picha hapo juu ni Wanamtandao wa 2SEEDS Network,akina mama hawa wamekuwa wakijituma kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha wanafikia malengo yao ya Kikundi. Wanamtandao hawa wapo katika Kijiji cha Tabora nje kidogo ya Wilaya ya Korogwe.Wanamtandao wanajishughulisha na utengenezaji wa Crips za viazi,karanga zenye mchanganyiko na mayai na wanakausha mboga za majani kwa kutumia mashine za bei nafuu, amabayo kila mwanamtandao katika kikundi anamiliki.
Mradi katika picha hapo juu unavyojaribu kuelezea malengo ya miradi yote ni kuwabadilisha maisha yao Wanamtandao.
Kijungumoto mradi pekee miongoni mwa miradi nane, wenye kutoa asali na nta na umekuwa wenye mafanikio makubwa sasa tangu umeanzishwa na tayari Wanamtandao wameanza kufaidi matunda yake.

Monday, June 15, 2015

Mradi wa Vitunguu saum- Bombo Majimoto Korogwe

Picha ya hapo juu inaonyesha mojawapo ya Nyumba za mazao(Green House) ambazo ndani yake kama unavyoweza kuona mna matuta kadhaa ya vitunguu saum.Mradi huu umeonekana kuwa wenye kuleta mafanikio makubwa kwa wanakikundi cha Bombomajimoto,ambapo mbali ya shamba hili la pamoja tayari kila mwanakikundi ameanzisha shamba lake binafsi ili aweze kustawisha zao hili la vitunguu saum.

 Katika picha hapo juu ni sehemu tuu ya  matuta katika shamba la  vitunguu saum vinavyoendelea kustawishwa na wanakikundi hiki cha Bombomajimoto huko Korogwe Vijijini chini ya uangalizi wa Shirika la 2Seeds Network.

 Katika picha hapo juu ni kabati ambalo linatumiwa na Wanakikundi  cha BomboMajimoto kutunzia vifaa mbalimbali yakiwemo madawa maalum kwa ajili ya kutunza mazao katika mashamba yao.
 Hapo juu ni picha ya pamoja ya Wanakikundi wa Bombo Majimoto na wageni waliowatembelea kuona maendeleo ya mradi wa vitunguu saum unaoendeshwa kwa njia ya kilimo cha kawaida na kwakutumia mfumo wa nyumba za mazao(Green house). Kutoka kushoto ni Bwana Anderson Shaka Mtaalamu wa Mawasiliano kwa njia ya Kompyuta  kutoka Shirika la Masoko Kariakoo, wapili ni Mama Tatu Mwanakikundi, Bwana Vedastus Valentine Afisa Biashara kutoka Shirika la Masoko Kariakoo, Bwana Shebe mwanakikundi  ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kikundi na aliyekaa ni Bwana Hamdani naye ni Mwanakikundi.
Afisa biashara wa Shirika la Masoko Kariakoo aliyesimama katikati Bwana Vedastus Valentine akiwapa ushauri Wanamtandao wa 2Seeds Network wa kikundi cha Bombo Majimoto Korogwe Vijijini wakati alipowatembelea ili kujionea maendeleo ya mradi huo wa vitunguu saum.wengine waliosimama aliyevaa kofia ni Bwana Shebe ambaye ni mwenyekiti wa Kikundi cha mradi huo na mwingine ni Bwana Hamdani.

Wednesday, June 10, 2015

Wanamtandao

Katika picha hapo juu ni ya Wanamtandao amabao wameunganishwa na Shirika la 2SEEDS Network ambao wamo katika vikundi tofautitofauti kutoka katika miradi mbalimbali ipatayo nane na ambayo imesambaa katika vijiji mbalimbali vilivyomo katika wilaya ya Korogwe Vijijini. Vijiji hivyo ni hivi vifuatavyo Kwakiliga,Tabora,Magoma, Magoma Kwata, Bombo Majimoto,Kijungumoto,Lutindi na Bungu.

Katika vijiji hivyo kuna miradi mbalimbali ya uzalishaji mali kama vile ufugaji nyuki,kuku na mbuzi na kilimo cha mazao mbalimbali.

Tutakuwa tunawaletea taarifa za mradi mmojammoja kila siku hadi mwisho.

Wanamtandao wa 2SEEDS Network - Korogwe Vijijini

 Katika picha hapo juu ni sehemu ya bwawa la samaki, na banda la kuku ambalo limejengwa ndani ya eneo la bwawa kama linavyoonekana hapo katika picha. Miradi hii miwili inategemeana kiutunzaji kwani mbolea inayotokana na kuku katika banda hudondokea ndani ya bwawa la samaki na kuwa chakula cha samaki. Miradi hii ipo katika kijiji cha Magoma Kwata wilayani Korogwe vijijini,lakini pia miradi hii iliyobuniwa na Wanamtandao wa 2Seeds Network ipo chini ya uangalizi wanamtandao wa Shule ya Msingi Kwata.

 Katika picha hapo juu ni banda la kuku likwa na kuku ndani yake na tayari mradi huu umeanza kuzalisha mayai,mojawapo ya miradi iliyopo katika Kijiji cha Magoma Kwata unaosimamiwa na baadhi ya Wanafunzi wa Shule hiyo ya Kwata ambao wameunganishwa katika Mtandao wa 2SEEDS Network.

 Katika picha hapo juu ni mradi wa Vitunguu saumu ambao naoupo katika kijiji cha Magoma Kwata,wanamtandao waliopo katika kikundi hiki hutumia drip irrigation method katika kumwagilia mimea ya vitunguu katika matuta yake kama inavyoonekana mipira hiyo midogomidogo imetandazwa kwa kufuata mistari ya mimea.

 Katika picha hapo juu aliyesimama wapili kutoka kulia ni Bwana Vedastus Valentine ambaye ni Afisa Biashara kutoka Shirika la Masoko Kariakoo akiwa anamsikiliza mwanakikundi anaejulikana kwa jina Babu Francis  Mwamkai aliyeshika miwani mkononi mwake akitoa maelezo jinsi wanavyojitahidi kuenedesha miradi yao kwa umakini ili waweze kufikia malengo yakufikia maisha bora.

Katika picha hapo juu ni Mradi wa mbuzi wa maziwa ambao pia upo katika Kijiji hichohicho cha Magoma Kwata, tayari mradi huu umeanza kutoa matunda kwakutoa maziwa. maziwa hayo yanatumiwa na wanafunzi katika kuboresha afya zao,lakini kwa mujibu wa maelezo ya babu Francis Mwamkai wanao mpango wa kuongeza idadi ya mbuzi hao katika kuhakikisha kuwa mradi huo unawaletea tija zaidi.

Monday, June 8, 2015

MKUTANO MKUU WA 2SEEDS Network KOROGWE

 Katika picha ni  sehemu tuu ya Wanamtandao wa 2SEEDS Network ambao walihudhuria mkutano huo maalum ambao hufanyika kila mwaka kwa ajili ya kutathimini maendeleo ya miradi mbalimbali ya uzalishaji mali ikiwamo ya kilimo na ufugaji. 2SEEDS Network ni Shirika lisilokuwa la Kiserikali ambalo makao yake makuu yapo katika Jiji la Washington  nchini Marekani,shirika hili limekuwa likifanya juhudi za kuboresha maisha ya wakulima wadogowadogo kwa kuwasaidia kuibua miradi tofautitofauti kulingana na mazingira wanayoishi na kuisimamia kwa karibu sana kwa kushirikiana na Wanavijiji huku wakiwasaidia kupata elimu ya Ujasiriamali.

 Sehemu ya Wajumbe ambao ni Wanamiradi husika wakiwa wamekaa ndani ya Ukumbi wa kanisa la Anglican uliopo nje kidogo  ya mji wa Korogwe,huku wakiendelea kufuatilia mambo yaliyokuwa yamejiri katika mkutano huo mwishoni mwa wiki iliyopita
 Wanamtandao wakifanya mjadala kuhusu miradi wanayoiendesha katika vijiji tofauti wakati wa mkutano wa mwaka ulipofanyika siku ya Jumamosi ya tarehe 6/6/2015 wilayani Korogwe.
Mkurugenzi Mkuu wa 2SEEDS Network hapa nchini Tanzania kama anavyoonekana katika picha hapo juu Bi.Ana  Le Rocha akifafanua jambo wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka. Mkutano huo ulifanyika wilayani Korogwe mkoani Tanga mwishoni mwa wiki iliyopita. Mkutano ulikuwa unafanya tathimini juu ya miradi mbalimbali ambayo inaendelea katika maeneo mbalimbali katika vijiji vilivyomo ndani ya wilaya ya Korogwe Vijijini.

Wednesday, June 3, 2015

Watumishi wa Shirika la Masoko Kariakoo

 Katika picha hapo juu ni Bwana James Kanyilili akiwa ofisini kwake mapema leo asubuhi. Bwana Kanyilili ni mtumishi wa Shirika hili la Masoko katika Idara ya Fedha

Katika picha hapo juu ni Bwana Jacob Nombo,naye pia akiwa mezani anaendelea na shughuli zake za kila siku,naye ni mtumishi katika Idara ya Fedha.

KIKAO CHA BODI YA USHAURI

 Kikao cha Bodi ya Ushauri kilichofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita. Kikao hicho kilikuwa na kazi ya kujadili na kuipitisha Bajeti ya Shirika kwa mwaka wa fedha 2015/2016. Katika picha hapo juu kutoka kulia ni Bi.Sarah Yohana Kaimu Mwenyekiti wa Bodi akiongoza kikao hicho, wa pili  ni Katibu wa Bodi ambaye pia ni Meneja Mkuu wa Shirika Bwana Florens F.Seiya na anayefuata ni Meneja Utumishi wa Shirika Bwana Godwin Mrosso.

Katika picha hapo juu ni Bi.Sarah Yohana Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Shirika la Masoko Kariakoo,akifunga kikao cha Bodi hiyo mara baada ya kujadili na kuipitisha bajeti ya Shirika  kwa mwaka wa fedha wa 2015/2016 mwishoni mwa wiki iliyopita. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Shirika la Masoko Kariakoo.

Monday, June 1, 2015

SOKO LA WAZI LAREJEA KARIAKOO

 Katika picha hapo juu mapaa madogomadogo yanayoonekana ni mapaa ya meza mpya ambazo zimetengezwa katika ubora zaidi kwa ajili ya kupanga bidhaa katika eneo hilo la Soko la Wazi ambalo lilivunjwa. Eneo hilo lipo katika kiwanja cha Shirika la Masoko kati ya Jengo Kuu la Soko na Soko dogo

Wafanyabiashara wakiwa katika maeneo yao yakufanyia biashara mapema leo asubuhii.