Thursday, May 8, 2014

Bodi ya Ushauri ya Shirika la Masoko ya Kariakoo ilikutana leo asubuhi

 Mweneyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Shirika la Masoko ya Kariakoo Bwana Wilson Kabwe ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Jiji la Dar Es Salaam akifungua Kikao cha dharula cha Bodi hiyo leo mapema asubuhi. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Shirika la Masoko;kikao hicho kililenga kujadili agenda moja tuu muhim ambayo ni Mstakabali wa Shirika la Masoko ya Kariakoo baada ya bomoabomoa iliyofanywa katika maeneo ya Viwanja vya Shirika hilo mwezi mmoja uliopita.
 Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko Bwana Florens Seiya ambaye ni Katibu wa  Bodi hiyo alipokuwa akitoa taarifa ya Shirika kuhusiana  na bomoabomoa  na athari ambazo zimelikumba Shirika pamoja wafanyabiashara ambao walikumbwa kwayo. Pamoja na hasara kadhaa wa kadhaa katika taarifa yake aliyoiwasilisha kwa Bodi hiyo na hatua kadhaa  ambazo Uongozi wa Shirika la Masoko ulizichukua hadi sasa.
 Mwenyekiti wa Bodi Bwana Wilson Kabwe mwenye kitabu chenye rangi nyekundu  katikati akiwa katika kutembelea maeneo ya viwanja vya Shirika mapema leo asubuhi kwani mara baada ya kufungua kikao hicho cha Bodi aliamuru  Wajumbe wa Bodi kwenda site ili kujionea hali halisi na ramani inayoonesha mipaka ya viwanja vya Shirika la Masoko;ili kuwapa picha halisi Wajumbe wakati wa kuchangia mawazo yao.Aliyeshika bahasha ni Meneja Mkuu wa Shirika.
 Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko Bwana Florens Seiya akitoa maelezo kuhusu ramani na mipaka ya viwanja vya Soko Kuu la Kariakoo kwa Wajumbe wa Bodi mapema leo asubuhi.Shirika la Masoko ya Kariakoo lilianzishwa kwa Sheria Namba 36 ya  Bunge ya Mwaka 1974 hivyo lina Haki zote za kuendesha shughuli zake katika viwanja bila kuingiliwa na Taasisi nyingine kama yalivyo Mashirika mengine ya Umma hapa nchini.
 Eneo hili ambalo Wajumbe wamesimama na kupewa maelezo ni barabara ya Pemba ambapo  pembeni yake kuna kisima cha maji ambacho kinamilikiwa na Shirika,ambacho mwezi mmoja uliopita kilkuwa kimevunjwa pampu yake na wakati wa bomoabomoa iliyoendeshwa na Manispaa ya Ilala na katika siku chache baadaye Wahandisi wa Shirika walikifanyia ukarabati.
 Mwenyekiti wa Bodi Bwana Wilson Kabwe akiwa ameongozana na Wajumbe wa Bodi hakuishia tuu maeneo ya nje; bali aliingia hadi maeneo ya Shimoni kujionea hali halisi ya Wafanyabiashara wanavyopata shida kwa msongamano mkubwa ambao umesababishwa na kitendo cha kubomolewa eneo la Soko la Wazi na kuwafanya wafanyabiashara hao kukimbilia wote Shimoni. Hapa akielekea eneo la Gate la kuingilia Shimoni maarufu kama Gate (5).
Hapa ziara  ilikuwa inaendelea kuelekea Shimoni kwenye Soko la Jumula,kutoka  kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Usalama wa Shirika Bwana Jossam Mzava, Bibi Ester Chogero Katibu wa TUICO katika Shirika la Masoko,Mwenyekiti wa Bodi Bwana Wilson Kabwe,Bwana Mwakabinga Meneja Utumishi kutoka Jiji,Meneja Mkuu wa Shirika Bwana Florens Seiya na Bibi Dk.H.Kawawa ambaye ni Bibi Afya wa Jiji la Dar Es Salaam pamoja na wajumbe wengine.