Monday, April 27, 2015

2SEEDS Network walipotemebelea Soko Kuu la Kariakoo

Katika picha hapo juu ni Mtumishi wa Shirika la Masoko ya Kariakoo Bi.Romana Lukanga akiwa ameambatana na Vijana wanaofanya kazi kwa kujitolea  (Volunteers) katika Shirika lisiliokuwa la kiserikali la 2SEEDS Network lenye makao yake makuu nchini Marekani,vijana hao wakiwa katika eneo la Shimoni Kariakoo. Ziara hii hii waliifanya mwishoni mwa wiki iliyopita.


 Bi.Lukanga Romana akitoa maelekezo kwa vijana wa 2SEEDS Network namna anavyofanya kazi yake yakuingiza taarifa za bei za mazao mbalimbali ambayo yanauzwa sokoni Kariakoo.Vijana hao wa 2SEEDS Network wengi wao huishi katika vijiji mbalimbali ambavyo vipo katika Wilaya ya Korogwe vijijini wakiwasaidia wananchi mbalimbali katika kuibua miradi na kuiendesha ili kuboresha  maisha yao.

Katika picha hapo juu ni Bi.Romana Lukanga akiwaonyesha vijana wa 2SEEDS Network jinsi anavyoitumia simu ya mkononi (Smartphone) kuingiza taarifa ya bei za mazao.