Monday, December 30, 2013

MAANDALIZI YA SIKU KUU YA MWAKA MPYA 2014


Pichani hapo juu ni baadhi ya wafanyabiashara wa soko la wazi la Kariakoo, wakiwa na wateja wao mapema leo asubuhi. Soko la wazi Kariakoo unaweza kupata mahitaji yako mbalimbali kama inavyoonekana pichani hapo juu.


Jipatie nyanya kwa Shilingi 5,000=/ tu sokoni Kariakoo Jijini Dar es salaam Tanzania, bidhaa hizi zinatoka sehemu mbalimbali nchini Tanzania kama vile Morogoro, Mwanza, Iringa, Tanga na maeneo mengine nchini.

Nyanya zikiwa kwenye sado ya lita4 zikiuzwa kwa shilingi 5,000
Viazi vinauzwa kwa shilingi 7,000=/ tu!



Thursday, December 26, 2013

WATU WAFURIKA SOKONI KARIAKOO KUFUATA BIDHAA

Magari yakiwa yameegeshwa katika eneo la soko Kuu la Kariakoo Jijini Dar es Salaam. 


 Pichani hapo juu ni baadhi ya wateja waliofika sokoni Kariakoo Jijini Dar es Salaam wakipata huduma kutoka kwa wafanyabiashara wa sokoni hapa, mahala hapa palikuwa panauzwa nguo kwa bei ya chini sana.

Maegesho ya magari katika eneo la soko Kuu la Kariakoo likiwa limefurika magari ya watu mbalimbali waliokuja Kariakoo kujipatia huduma kama inavyoonekana pichani hapo juu.

Sunday, December 22, 2013

BIDHAA SAFI NA BORA ZINAPATIKANA SOKONI KARIAKOO JIJINI DAR ES SALAAM

Wafanyabiashara wa Soko la Wazi Sokoni Kariakoo, wakiwa na wateja wao mapema leo asubuhi katka soko Kuu la Kariakoo Jijini Dar es Salaam.

Katika msimu huu wa siku kuu karibuni sokoni Kariakoo wateja wetu wote ili muweze kujipatia bidhaa bora sokoni Kariakoo Jijini Dar es Salaam.

BIASHARA KATIKA MSIMU WA SIKU KUU ZA NOEL NA MWAKA MPYA.


Mfanyabiashara wa sokoni Kariakoo Jijini Dar es Salaam akiandaa miti maalumu kwa ajili ya siku kuu ya Christ Mass.


Badhi ya bidhaa za Msimu wa Siku Kuu, kama zinavyoonekana pichani hapo juu katika Soko la Kariakoo Jijini Dar es Salaam- Tanzania.
  

Friday, December 6, 2013

BORESHA BUSTANI YAKO SASA KWA KUTUMIA ZANA BORA ZA KILIMO!

Torori
Pichani hapo juu ni torori maalum kwa shughuli za mikono, kama vile kuhamisha mizigo midogo midogo kutoka sehem moja kwenda sehemu nyingine, kubebea mchanga, samadi kwa ajili ya bustani. unaweza kupata vifaa hivi Sokoni Kariakoo Jijini Dar es Salaam kwa bei kati ya
Shilingi 50,000 hadi Shilingi 48,000/= kwa torori za rangi ya kijani.
Shilingi 650000 hadi Shilingi 60000/= kwa torori za rangi nyeusi kama zinavyoonekana hapo juu pichani.


Mipira ya Maji

Katika hatua za kuboresha bustani ama shamba kwa kilimo cha umwagiliaji, basi unaweza kutumia mipira bora na imara kama hii hapa pichani;hapa utapata mipira ya nchi 1 kwa shilingi 75,000/= kwa urefu wa mita 50.
 nusu nchi (1/2) kwa shilingi 50,000 kwa urefu wa mita 50.  Vyote hivyo vinapatikana dukani kwa Emma Macherehani waliopo Sokoni Kariakoo Jijini Dar es Salaam.

Emma Macherehani unaweza kuwapata kwa mawasiliano yafuatayo.
+255 755363157
+255 717 830 813
Email: emmanuelikaonya@yahoo.com

WAFANYA BIASHARA KUONDOA BIDHAA ZAO KATIKA ENEO LA BARABARA SOKONI KARIAKOO

Askari wa Shirika la Masoko ya Kariakoo, wakiwapa maelekezo ya kuondoa bidhaa zao walizopanga barabarani katika eneo la Shirika la Masoko mapema leo asubuhi.  

Tuesday, December 3, 2013

HOHO, KAROTI SAFI ZINAPATIKANA SOKONI KARIAKOO

Tuesday, November 26, 2013

GUEST HOUSE FOR SALE 350 MILLION ONLY!!!!

NYUMBA MPYA YA KULALA WAGENI YENYE VYUMBA (9), ILIYOKAMILIKA KWA KILA KITU ILIYOPO ENEO LA MPUYANI-KISARAWE INATAZAMANA NA KIWANDA KIPYA CHA SARUJI INAUZWA KWA SHILINGI ZA KITANZANIA MILIONI 350 /=

MAWASILIANO  PIGA NAMBA HII:  +255 (0) 784 824 013

"A NEWLY CONSTRUCTED GUEST HOUSE OF NINE BED ROOMS LOCATED HIGH OPPOSITE THE NEW CEMENT FACTORY AT MPUYANI-KISARAWE IS AVAILABLE FOR SALE AT 35O MILLION TSH. THE GUEST HOUSE IS FULLY FURNISHED."

CONTACT PHONE +255 (0) 784 824 013


Tuesday, November 19, 2013

Mashine za TRA zaleta kizazaa mitaa ya Kariakoo!

Kizazaa cha Mashine za TRA kimepelekea Maduka mengi pamoja na Ofisi kadhaa zinazoendesha shughuli zake za biashara  katika mitaa ya hapa Kariakoo kufungwa kabisa na kutofanya shughuli zake za kila siku za uzalishaji mali kwa takribani siku mbili sasa tangu jana!

Kariakoo kama inavyofahamika kuwa ni sehemu yenye pilikapilika nyingi za biashara katika Jiji la Dar Es Salaam; lakini hali haikuwa hivo jana Jumatatu na hata leo hii!

Kama hiyo haitoshi hata msongamano wa magari umepungua sanaaa kwani shughuli nyingi zimesimama!

Baadhi ya Wafanyabiashara walionekana wakiwa wamekaa nje ya maduka yao na wengine kupitapita tuu katika mitaa mbalimbali!

Lakini pia hali hii imeleta usumbufu  kwa Wafanyabiashara wa kutoka nchi jirani za Congo DRC,Zambia,Malawi,Uganda,Rwanda,Burundi,Kenya na hata Visiwa vya Commoro ambao wamekuja  Jijini DSM kwa ajili ya kununua bidhaa mbalimbali ili kupeleka kwao wamekwama! kwakuwa maduka mengi yamefungwa! Huenda hali hii inaweza kuwaharibia bajeti zao!

Monday, November 11, 2013

BIDHAA BORA ZINAPATIKANA SOKONI KARIAKOO


Pichani hapo juu ni dagaa kutoka Kigoma wanapatikana sokoni Kariakoo kwa bei nafuu, fika Kariakoo uweze kujipatia dagaa wahi!!!!



 Soko la wazi Kariakoo, wafanyabiashara wa soko la wazi wakiandaa bidhaa zao mapema leo asubuhi. Hapa unaweza kupata nyanya, kabichi, viazi na vingine vingi; kwa matumizi ya familia yako,Mghahawani au Mama Lishe.


 Vitunguu swaumu, vitunguu maji tangawizi vyote vinapatikana sokoni; karibuni wote mjipatie bidhaa bora kwa afya boraaaaa!!!

 Pili pili safi kwa bei poa kabisa,kila aina ya pilipiliiiii!!! "Money for value" bwana! Mpendwa Mteja usiogope kufika Kariakoo sokoni kwa mahitaji yako ya kila siku!


Friday, November 8, 2013

SAMAKI WABICHI WANAPATIKAN SOKONI KARIAKOO

 Pichani hapo juu ni samaki aina ya "Redsnaper" hawa ni miongoni mwa samaki adimu sana, samaki hawa sasa wanapatikana Soko Kuu la Kariakoo Jijini Dar es Salaam -Tanzania. Samaki hawa ambao mara nyingi huliwa katika mahoteli makubwa nchini sasa wanauzwa sokoni  Kariakoo, jipatie samaki hawa ujenge afya kwa Sh. 12000/= tu pesa ya Kitanzania.


Wafanyabiashara wa samaki katika soko Kuu la Kariakoo wakiwa wamekaa katika eneo lao la kazi kama wanvyoonekana picha.

 JIPATIE NDIZI SAFI SOKONI KARIAKOO.


 Wachuuzi wa mizigo katika soko Kuu la Kariakoo (Shimoni) wakishusha ndizi katika moja ya magari kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini Tanzania. 

 Kwa ndizi safi na bora kwa afya yako, karibu Sokoni Kariakoo Jijini Dar es Salaam.

Wednesday, November 6, 2013

EMMA MACHEREHANI: Wauzaji wa Cherehani Sokoni Kariakoo

 Pichani hapo juu ni duk la Emma Macherehani lililopo ndani ya soko Kuu la Kariakoo, hawa ni wauzaji wa kubwa wa Cherehani aina zote kama vile Buterfly, Zou 43, Usha, Juki, mashine za Sweta Overlock size zote. Mashine za ngozi, Mikasi ya umeme na kawaida, Mashine za kudalizi kama Taking, Aksa,nyuzi aina zote pamoja na spea mbalimbali za cherehani.

 Hii ni sehemu ambayo mteja anaingia na kuchagua cherehani anayoitaka mwenyewe, kama zinavyoonekana pichani hapo juu, zipo aina nyingi za cherehani kwa bei za kuridhisha kabisa. Karibuni wote Kariakoo sokoni katika duka linaloitwa Emma Macherehani mjipatie cherehani bora na imara.

Pichani hapo juu ni Clara Kaaya ambaye ni Mkurugenzi  wa Emma Macherehani sokoni Kariakoo Jijini Dar es Salaam- Tanzania akiwa ofisini kwake mapema leo asubuhi.



Cherehani ya kisasa ya kushonea nguo, cherehani hii inatumia umeme, jipatie cherehani hii dukani kwa Emma Macherehani;wapo ghorofa ya kwanza ndani ya soko kuu Kariakoo Jijini DSM


 Pichani ni (Overlock machine) hii ni cherehani ya kudalizi, bei yake ni nafuu sana, jipatie kwa Tsh 1,500,000=/ ni mashine imara na  inayoweza kurahisisha shughuli zako za kudalizi nguo mbalimbali na kwa ufanisi zaidi.








 Hii ni mashine ya kuprinti tisheti, ni mashine inayotumia memory card au USB Cable, kwa wale wenye shughuli za kuprint basi mshine hii inawafaa sana. Karibuni Emma Macherehani.waliopo Kariakoo hapa Jijini DSM

Huu ni uzi kwa ajili ya kushonea nguo za aina mbalimbali, pia uzi huu unapatikana kwa Emma Macherehani sokoni Kariakoo

Pichani hapo juu ni Mota za cherehani na spea mbalimbali, pia zinapatikana sokoni Kariakoo jijini Dar es Salaam-Tanzania
Emma Macherehani unaweza kuwapata kwa mawasiliano yafuatayo.
+255 755363157
+255 717 830 813
Email: emmanuelikaonya@yahoo.com

Monday, November 4, 2013

PATA NYANYA, VITUNGUU PILIPIPLI, HOHO NA VINGINE VINGI SOKONI KARIAKOO KWA BEI POA


Wafanyabiashara wa eneo la wazi katika Soko Kuu la Kariakoo wakiendelea kufungua biashara zao mapema leo asubuhi. katika eneo hili unaweza kujipatia nyanya, vitunguu, pilipili, karoti, hoho, bamia kwa bei ya kawida na vitu vingine vingi kama inavyoonekana pichani



Mzani kwa ajili ya kupimia bidhaa ukiwa mezani tayari kwa kazi, ambapo baadhi ya bidhaa hupimwa kwa kilo.

Karoti safi na bora zinapatikana sokoni kariakoo, karibuni wote!!


Vitunguu kutoka Morogoro vinapatikana sokoni Kariakoo Jijini Dar es Salaam-Tanzania


Pichani ni mfanya biashara maarufu wa vitunguu katika eneo la Kariakoo Shimoni, akiwa katiaka meza yake ya biashara kama picha invyoonesha hapo juu.


KING FISH: SAMAKI MTAM KUTOKA BAHARI YA HINDI


Tanzania tumejaliwa maliasili nyingi kuanzia nchi kavu hadi majini. Pichani hapo juu ni samaki aina ya King Fish ambaye amevuliwa katika Bahari ya Hindi Jijini Dar es Salaam, akiwa mezani sokoni Kariakoo tayari kwa kuuzwa.

Vipande vya Samaki kingfish vikiwa mezani kwa ajili ya kuuzwa, karibuni wote mjipatie samaki.


Geti kuu la kuingilia  Kariakoo Shimoni, ambapo magari kutoka sehemu mbalimbali nchini hupita katika mlango huu ili kuweza kupakua mzigo. Soko la kariakoo lililojengwa miaka ya 1970.

Friday, November 1, 2013

MATUKIO KATIKA PICHA LEO SOKONI KARIAKOO

VITAMBULISHO VYA WAFANYABIASHARA


 Afisa biashara wa Shirika la Masoko Kariakoo Bi.Mwinga Luhoyo (kushoto) akihakiki kitambulisho cha mfanya biashara Bw. Amiri  wa Soko Kuu la Kariakoo eneo la Shimoni.


 Maafisa biashara wa Soko Kuu la Kariakoo Bi.Mwinga (kushoto) akiwa na Zefania Maiko (kulia)  wakipitia kwa makini faili la usajiri a wafanyabiasha wa sokoni Kariakoo Jijini Dar es Salaam mapema leo asubuhi.


ZEFANIA MBISE:Mfanyabiashara  Mashuhuri wa mayai.



 Mfanya biashara ambaye amekuwa akifanya biashara zake kati ya Dar es Salaam na Arusha Bwana Zefania pichani hapo juu akiwa eneo la Soko Kuu la Kariakoo ambaye shughuli yake ni kuleta mayai ya kuku wa kienyeji kutoka Mkoani Arusha nakuwauzia wateja wake wa Jijini Dar es Salaam.

 Ili kutambua yai zima na bovu, yale yanayonekana kuwa na rangi nyekundu kwa ndani ndio mazima tofauti na hiyo rangi sio zima.