Tuesday, June 3, 2014

Kariakoo Market Corporation na Habari Mazao Founders

 Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo  Bwana Florens Seiya akisaini Mkataba baina ya Shirika la Masoko ya Kariakoo na Habari Mazao Founders.Mkataba huu wa ushirikano utawezesha sasa KMC kufanya kazi kwa pamoja na Habari Mazao katika kuhakikisha kuwa bei halisi za mazao zinapatikana kwenye Mtandao wa Shirika muda wote na pia Wadau wengine watazipata taarifa hizi kwa njia ya simu zao za mkononi (SMS Solution). Zoezi hili la utiaji saini ulifanyika jana katika Ofisi ya Meneja Mkuu.
 Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo akiupitia Mkataba kwa  mara ya  mwisho  kabla hajausaini jana Ofisini kwake; na aliyeshikilia mikataba ni Mratibu wa Masoko Project kutoka 2SEEDS Network Bi.Monique Galvao ambaye aliiwakilisha Taasisi hiyo.
 Bi.Monique Galvao muwakilishi wa 2SEEDS Network aliyesimama akitoa maelezo ya msingi kuhusiana na Mkataba wa ushirikiano kati ya KMC na Habari Mazao kwa jinsi gani utakavyokuwa na tija kwa Shirika la Masoko ya Kariakoo.Habari Mazao Founders inawaunganisha vijana hawa Christian Mlayi mwenye T-Shirt ya bluu,Kaboda Suguedo mwenye miwani na Bariki mwenye shati nyeusi.
Mjumbe wa Bodi ya Shirika la Masoko ya Kariakoo Bi. Esther Chogero akitia sahihi yake katika Mkataba wa ushirikiano baina Shirika la Masoko ya Kariakoo na Habari Mazao Founders; kwa ajili ya kufanya kazi pamoja katika Mradi wa ukusanyaji na utoaji taarifa za bei  kutoka Soko kuu la Kariakoo kwa njia ya SMS na Website.Hafla hii ya kutiliana saini ilifanyika jana katika Ofisi ya Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko.