Monday, June 30, 2014

Pata taarifa mbalimbali za kimaendeleo kutoka Shirika la Masoko ya Kariakoo Jijini Dar Es Salaam

 Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo Bwana Florens Seiya akipeana mkono na Bwana Beenedict Tesha Mkurugenzi wa Jamaa Technology ambaye ni Service Provider.Hapo walikuwa wakibadilishana mkataba wa utoaji  huduma yaani Service Level Agreement (SLA) baada ya kusaini.Hafla hii ilifanyika Jumanne iliyopita katika Ofisi za Shirika la Masoko ya Kariakoo Jijini Dar Es Salaam.Aliyesimama kati yao ni Bi.Anna Rocha Mkurugenzi wa 2SEEDS Network hapa nchini Tanzania.
 Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo Bwana Florens Seiya akizungumza na Waandishi wa habari Ofisini kwake mara baada ya uzinduzi wa tovuti ya Shirika la Masoko ya Kariakoo ambayo kwa sasa kwa kupitia tovuti hiyo watu mbalimbali wataweza kuona taarifa mbalimbali za bei za mazao yauzwayo katika Soko Kuu la Kariakoo kila siku na wakati wowote.
 Katika picha hapo juu ni Mkuu wa Kitengo cha Tehama(ICT) katika  Shirika la Masoko ya Kariakoo Bwana Anderson Shaka akiwa anatoa maelekezo mafupi ya namna gani ya kutumia Simu za mkononi ili kupata bei za mazao mbalimbali yanayouzwa katika Soko Kuu la Kariakoo.lakini pia bei hizo kwa baadhi ya mazao makuu ya chakula bei zake zipo katika Website ya Shirika hili.Waandishi wa habari kutoka katika Vyombo mbalimbali vya habari walihudhuria uzinduzi huo Jumanne wiki iliyopita.
 Mkurungenzi wa 2SEEDS Network Tanzania Bi.Anna Rocha akitoa maelezo ya namna gani Mtandao wao unavyofanya kazi hapa nchini tangu mwaka 2011.Pamoja na mambo mengine pia lakini pia 2SEEDS Network ni Washirika wakubwa na Shirika la Masoko ya Kariakoo katika kuwatafutia  masoko ya bidhaa/ mazao ya Wakulima kutoka vijijini hasa katika Wilaya ya Korogwe ambako wanawawezesha Wakulima katika kuibua miradi ya uzalishaji mali na kuwaasimamia kwa karibu ili kufikia malengo ya kimaendeleo na maisha bora.

Bwana Christian Mlayi ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Habari Mazao Founders akiwa Ofisini kwa Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo akizungumza na Waandishi wa habari Jumanne iliypita mara baada ya uzinduzi wa Mtandao wa kutoa taarifa za bei za mazao kutoka Soko Kuu la kariakoo. Habari Mazao founders wameshirka wa mradi wa Masoko kwa kutengeneza Mfumo ambata ambao hufanya kazi sambamba na Mfumo mkuu wa bei wa Shirika la Masoko(KMC Database Management System).

Monday, June 23, 2014

Shirika la Masoko ya Kariakoo pamoja na Washirika wake 2Seeds Network na Habari Mazao


Kariakoo Market Corporation (KMC) na Washirika wake 2Seeds Network na Habari Mazao
kwa pamoja watafanya uzinduzi wa Tovuti,Blog na Huduma ya SMS.
Huduma ya SMS (SMS SOLUTION) inatarajiwa kutumiwa katika kutoa taarifa za bei za mazao mbalimbali ambayo huletwa katika Soko Kuu la Kariakoo lililopo Jijini Dar Es Salaam. Vyombo kadhaa vya Habari vimealikwa katika Uzinduzi huo kesho tarehe 24/6/2014 kuanzia saa 4.00  hadi 4.30 asubuhi.
Hafla hiyo itafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Shirika la Masoko ya Kariakoo uliopo katika Jengo Kuu la Soko ghorofa ya Kwanza.

Wednesday, June 18, 2014

Safari ya Wajumbe wa 2SEEDS Network kutoka DSM wakiwa kijijini Tabora

 Familia ya Wanatabora imependezaa saaana! Katika kijiji hiki kuna mradi wa kutengeneza crips za viazi na mihogo.2SEEDS Network husimamia kwa karibu sana maendeleo yake.
Hapa ni kijijini tabora (ndogo) moja ya vijiji vilivyopo wilayani Korogwe;hapa katika picha kutoka kulia ni Bwana Anderson Shaka Mkuu wa Kitengo cha ICT katika Shirika la Masoko ya Kariakoo,Christian Mlay kutoka Habari Mazao Founders,Munguatosha Mfanyabiashara toka Soko Kuu la Kariakoo  na Henry Rwejuna Mtakwimu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo.Wapo na wenyeji wao dada Haliyahewa.

Tuesday, June 17, 2014

Mkutano wa Mwaka wa 2SEEDS Network uliofanyika Korogwe Mkoani Tanga

 Katika picha hapo juu  ya kwanza juu  kushoto ni picha ya pamoja ya Wajumbe  wa Masoko Project kutoka Shirka la Masoko ya Kariakoo Jijini Dsm wajumbe hao kutoka kushoto ni Henry Rweijuna,Sophy,Anderson ShakaChristian Mlay,Monique na Munguatosha;picha ya pili juu ni Bwana Anderson Shaka akigawa kadi zenye namba kwa ajili ya kufanyia mazoezi ya kuuliza bei kwa njia ya SMS,picha ya chini kushoto ni Wajumbe wa Mkutano wakiwa katika chumba cha mkutano na picha ya chini kulia ni Mjumbe kutoka Masoko Project Bwana Christian Mlayi akitoa maelezo ya namna ya kutuma SMS ili kuuliza bei za mazao kutoka katika Soko Kuu la Kariakoo.
Katika picha hapo juu ni hekaheka za safari ya Wajumbe wa Masoko Project kutoka Dar Es Salaam. Hapa walikuwa wakisafiri kuelekea kijiji cha Tabora kilichopo nje kidogo ya mji wa Korogwe takribani KM 8 hivi;wakitumia usafiri wa bajaji hapo walikuwa wamenasa kwenye matope hivyo ikawalazimu kutelemka nakuanza kusukuma bajaji.
katika msafara huo alikuwepo Sophy,Munguatosha,Christian Mlay,Monique Galvalo,Henry Rweujuna,Anderson Shaka na madereva wa bajaji.
Vijiji vyenye miradi ya 2SEEDS Network Tabora,Kwakiliga,Kijungumoto,Bombomajimoto,Lutindi,Magoma vyote vipo katika Wilaya ya Korogwe.

Monday, June 16, 2014

Madiwani kutoka Halmashauriya Manispaa ya ILALA walipotembelea Soko Kuu la Kariakoo Alhamisi wiki iliyopita

 Katika picha hapo juu ni Bwana Edson Fungo ambaye aliongoza Ujumbe wa Madiwani kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kufika katika Ofisi za Shirika la Masoko ya Kariakoo Alhamisi wiki iliyopita. Ujumbe huo ulifika kukagua maumbo ambayo yatatumika na Wafanyabiashara wa eneo la Soko la Wazi
Meneja Mkuu wa Shirika Bwana Florens Seiya mwenye kitabu mkononi na Bwana Edson Fungo wakielekea eneo la Soko la Wazi katika viwanja vya Shirika la Masoko ya Kariakoo.
 Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo  aliyeshika kitabu mkononi akiwaeelezea jambo Waheshimiwa Madiwani katika eneo la Soko la Wazi katika viwanja  vya Shirika la Masoko ya Kariakoo.
 Hapa kwa makini kabisaa Madiwani wakimsikiliza Meneja Mkuu wa Shirika Bwana Florens Seiya ambaye amenyoosha mkono.Hapa alikuwa akitoa ufafanuzi kuhusu uzito unaoruhusiwa kuwa juu ya eneo hilo  linalotenganisha jengo kuu la Soko na Soko Dogo, ambalo linakusudiwa kutumika kwa Wafanyabiashara kufanya biashara zao kama ilivyokuwa mwanzo.
 Hapa ziara ya kutembelea viwanja vya Shirika ilikuwa ikiendelea sehemu hii hapa ni upande wa ambako liko lango kuu la kutokea eneo la Shimoni.Meneja Mkuu wa Shirika Bwana Florens Seiya na Bwana Edson Fungo Mkuu wa msafara wa Madiwani wakiwa wametangulia mbele.
 Hapa ni Meneja Mkuu wa Shirika Bwana Florens Seiya amabye ameshika kitabu akifafanua jambo kwa  Waheshimiwa Madiwani wa kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala walipotembelea Soko Kuu la Kariakoo na kufanya kikao cha kujadili namna ya kuwarejesha  Wafanyabiashara waliokuwa wakifanya shughuli zao katika eneo la Soko la Wazi; sambamba na kikao hicho walikagua maumbo ambayo yatatumika katika viwanja hivyo vya Shirika kupangia bidhaa mbalimbali.
 Katika picha hapo juu Wajumbe wa mkutano wakirejea katika Ukumbi wa mikutano wa Shirika la Masoko baada ya kutembelea maeneo ya viwanja vya Shirika na kupata maelezo jinsi Wafanyabiashara watakavyopangwa ili kurejea kufanya biashara katika eneo la Soko la Wazi.Waliotangulia mbele kutoka kulia ni Bwana Edson Fungo ambye aliongoza Ujumbe wa Madiwani toka Manispaa ya Ilala katika ziara; anayefuata ni Meneja Mkuu wa Shirika Bwana Florens Seiya na mwenye shati la draft ni Afisa usalama wa Shirika Bwana Moringe
Hii ni sehemu tuu ya Wajumbe wa Kikao maalum cha Madiwani na  kutoka manispaa ya Ilala  na Uongozi wa Shirika la Masoko ya Kariakoo wakiwa katika majumuisho mara baada ya kutembelea maeneo ya viwanja vya Shirika.

Tuesday, June 3, 2014

Kariakoo Market Corporation na Habari Mazao Founders

 Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo  Bwana Florens Seiya akisaini Mkataba baina ya Shirika la Masoko ya Kariakoo na Habari Mazao Founders.Mkataba huu wa ushirikano utawezesha sasa KMC kufanya kazi kwa pamoja na Habari Mazao katika kuhakikisha kuwa bei halisi za mazao zinapatikana kwenye Mtandao wa Shirika muda wote na pia Wadau wengine watazipata taarifa hizi kwa njia ya simu zao za mkononi (SMS Solution). Zoezi hili la utiaji saini ulifanyika jana katika Ofisi ya Meneja Mkuu.
 Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo akiupitia Mkataba kwa  mara ya  mwisho  kabla hajausaini jana Ofisini kwake; na aliyeshikilia mikataba ni Mratibu wa Masoko Project kutoka 2SEEDS Network Bi.Monique Galvao ambaye aliiwakilisha Taasisi hiyo.
 Bi.Monique Galvao muwakilishi wa 2SEEDS Network aliyesimama akitoa maelezo ya msingi kuhusiana na Mkataba wa ushirikiano kati ya KMC na Habari Mazao kwa jinsi gani utakavyokuwa na tija kwa Shirika la Masoko ya Kariakoo.Habari Mazao Founders inawaunganisha vijana hawa Christian Mlayi mwenye T-Shirt ya bluu,Kaboda Suguedo mwenye miwani na Bariki mwenye shati nyeusi.
Mjumbe wa Bodi ya Shirika la Masoko ya Kariakoo Bi. Esther Chogero akitia sahihi yake katika Mkataba wa ushirikiano baina Shirika la Masoko ya Kariakoo na Habari Mazao Founders; kwa ajili ya kufanya kazi pamoja katika Mradi wa ukusanyaji na utoaji taarifa za bei  kutoka Soko kuu la Kariakoo kwa njia ya SMS na Website.Hafla hii ya kutiliana saini ilifanyika jana katika Ofisi ya Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko.

Monday, June 2, 2014

Kariakoo Soko Kuu

 Katika picha hapo juu ni Mratibu wa Masoko Project Bi.Monique Galvao na wengine ni Wataalam wa kutengeneza Mifumo ya Kielekroniki kutoka Habari Mazao Team kijana Bariki na mwenzake Kaboda. Hapa walikuwa katika kikao kujadili namna ya kumalizia Project ya Masoko amabapo wao wanahusika katika uundaji wa mfumo saidizi ambao utafanya kazi sambamba na Mfumo mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo(KMC Database System) katika utoaji wa taarifa mbalimbali za bei za mazo yanayouzwa katika Soko Kuu la Kariakoo.Kikao hiki kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Shirika la Masoko mwishoni mwa wiki iliyopita.
Kutoka kushoto ni Bariki na Kaboda kutoka Habari Mazao Team wakiwa na Bwana Anderson Shaka yeye ni Mkuu wa Kitengo wa ICT katika Shirika la Masoko ya Kariakoo.Wote wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa kikao  kilicholenga kujadili na kuona jinsi Project ya Masoko itakavyomalizika na kuanza kuwanufaisha Wakulima,Wafanyabiashara pamoja na Walaji wa bidhaa zinazouzwa katika Soko Kuu la Kariakoo.