Wednesday, May 7, 2014

Kutoka Soko Kuu la Kariakoo leo!! Shirika la Masoko ya Kariakoo limesaini makubaliano na SIBESONK.

 Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo akisaini Waraka wa makubaliano (MoU) ambao utaiwezesha Kampuni ya SIBESONKE ya nchini Finland kutumia Mfumo wa Taarifa wa Kielektroniki unaomilikiwa na Shirika la Masoko ya Kariakoo katika kuwatumia taarifa za bei za mazao mbalimbali yanayouzwa  katika Soko Kuu la Kariakoo. Kampuni hiyo iliwakilshwa na Mkurugenzi wake Mkuu (CEO) Bwana Uwe Schwarz.
 Bwana Uwe Schwarz akisaini waraka wa makubaliano (MoU) ili Kampuni yake SIBESONKE yenye makao Makuu nchini Finland iweze kutumia Taarifa zinazokusanywa katika Database ya Shirika la Masoko  ili kuwatumia Wakulima,Wafanyabiashara pamoja na Wadau wengine wa bidhaa mbalimbali ambazo huuzwa katika Soko Kuu la Kariakoo lililopo Jijini Dar Es Salaam.
 CEO wa SIBESONKE akisaini MoU katika Ofisi za Shirika la Masoko anaemuelekeza ni Mwanasheria wa Shirika Mrs.Glory Kalabamu na anaeshuhudia ni Bwana Anderson Shaka yeye ni Mkuu wa Kitengo cha ICT katika Shirika la Masoko ya Kariakoo.Utiaji saini huo umefanyika leo mchana katika Ofisi za Shirika.
 Bwana Uwe Schwarz Mkurugenzi Mkuu wa SIBESONKE akiwa Ofisini kwa Meneja Mkuu pichani hayupo mara baada ya kuwasili ili kusaini Makubaliano (MoU);wa kulia kwake ni Mkuu wa Kitengo cha ICT wa Shirika la Masoko Bwana Anderson Shaka.
 Katika picha hapo juu kutoka kulia ni Mkurugenzi Mkuu (CEO)wa kampuni SIBESONKE Bwana Uwe Schwarz kutoka Finland,Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo,Bwana Florens Seiya,Mkuu wa Kitengo cha ICT wa Shirika la Masoko ya Kariakoo Bwana Anderson Shaka na Mrs. Glory Kalabamu Mwanasheria wa Shirika la Masoko;mara baada ya kusaini (MoU) ya kutumia KMC DBS ili kupata taarifa na kuzirusha kwa Wakulima na Wafanyabiashara.Zoezi la utiaji saini lilifanyika leo mchana katika Ofisi za Shirika Jijini DSM.
Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo akipeana mikono na Bwana Uwe  Schwarz (CEO) wa Kampuni ya SIBESONKE mara baada ya kusaini makubaliano ya kupata idhini ya kutumia Mfumo wa taarifa wa Shirika kurusha taarifa za bei za mazao yanayouzwa katika Soko Kuu la Kariakoo.