Friday, September 26, 2014

Mama Majasiriamali


Mama huyu katika picha hufanya biashara ya dagaa katika Soko Kuu la Kariakoo. Mezani kwake kuna kila aina ya dagaa ambao huwauza.Mama huyu yupo eneo la Wauza dagaa na samaki katika eneo la Shimoni.Katika alikutwa akiwapimia wateja wake dagaa!

Sokoni Kariakoo leo!

 Hawa ni samaki aina ya Sangara kutoka Ziwa Victoria. Samaki hao wameshakaangwa safi tayari kabisa kwa matumizi ya mboga! Ukiwa katika Soko la Kariakoo ingia eneo Shimoni kwenye eneo la biashara ya samaki utawapata.Karibuniii!
Pichani hapo juu ni aina mojawapo ya mboga za majani zinazopatikana katika soko Kuu la Kariakoo; mboga hiyo huuzwa kwa kilo kati ya Sh.1000/= hadi 1500/=. Fika eneo la Shimoni utazipata mboga hizi na nyinginezo pia!

Sunday, September 21, 2014

Ndizi kutoka Morogoro

Ndizi aina hii kwa wakati huu zinatoka Mkoani Morogoro hasa katika wilaya ya Kilombero katika kijiji maarufu kiitwacho Mbingu. Kijiji hiki kinapitiwa na barabara inayounganisha mji wa Ifakara na Mlimba.Ndizi Mzuzu huzalishwa kwa wingi sana katika kijiji hiki.

Tuesday, September 16, 2014

Kariakoo leo

 Katika picha hapo juu ni Wajasiriamali ambao hufanya shughuli zao za kutengeneza mifuk/vifungashio vya bidhaa ndogondogo kama vile viungo vya vyakula,karanga, bisi nakadhalika katika ukubwa wa aina tofautitofauti.Wajasiriamali hawa wapo katika moja vyumba vya Soko Dogo la Kariakoo Jijini Dar Es Salaam.Kwa mahitaji yako ya vifungashio hivi Sokoni Kariakoo katika Jengo la Soko Dogo
 Katika picha hapo juu ni moja ya Wateja waliofika katika sehemu hii ya Wajasiriamali wanaotengeneza vifungashio vya mifuko ya nailoni ili kununua.Vifungashio hivi hutengenezwa kwa kutmia mashine ndogondogo ambazo huendeshwa kwa mkono na zingine hutumia nishati ndogo ya umeme.
Sokoni Kariakoo kuna mpangilio mzuri wa kila jambo;katika picha hapo juu ni magari ya Wateja mbalimbali ambao wamefika kujipatia mahitaji katika Soko Kuu la Kariakoo.Magari haya yapo katika hali ya usalama bila shaka yoyote! hapo ni Mtaa wa Tandamti.

Monday, September 15, 2014

Kutoka Soko Kuu la Kariakoo - DSM

 Kitu gani ambacho ukifika katika Soko Kuu la Kariakoo hutakipataaaa? La hasha kuanzia nafaka,matunda,mboga mboga za majani hadi viungo vya kila aina.Katika picha hapo juu utaona Vitunguu swaum,Tangawizi,Ndimu na vinginevyo vipo kwa wingi mezani vikiwa katika ubora sana.Karibu Soko kuu la Kariakoo ujipatie bidhaa za kila aina. Bei ya vitunguu swaum na tangawizi ni kati ya Sh.4000 hadi 4500 kwa kilo moja.

 Miongoni mwa Watumishi wa Shirika la masoko ya Kariakoo ni Bwana Idd Mrope ambaye anaonekana katika picha hapo juu.Hapa yupo katika maeneo ya Ofisi za Shirika zilizopo katika ghorofa ya kwanza katika jengo la Soko Kuu.
Soko Kuu la Kariakoo ni Soko kubwa kuliko hapa nchini Tanzani,hii picha inaonesha sehemu mojawapo ya soko hili ambapo hapa barabara inayoingia katika eneo la soko la Jumla maarufu kama Shimoni.Eneo hili linaloonekana katika picha ni Geti Namba. 5 ambapo bidhaa karibu zote ambazo huingia hapa Sokoni hupitia hapa.

Friday, September 12, 2014

Matunda soko kuu kariakoo

 Picha ya zabibu kama inavyoonekana hapo juu katika Soko la Kariakoo leo ilikuwa ikiuza kwa bei ya shillingi elfu mbili mia tano kwa kilogram  na shillingi elfu thelathini kwa jumla


Katika picha hapo juu ni matunda aina ya ambazo kwa kiasi kikubwa huingizwa katika soko kuu la Kariakoo kila siku kutoka  mikoani na hususani katika mkoa Morogoro zinauzwa kwa bei  ya rejareja na jumla




Saturday, September 6, 2014

Hafla ya kukabidhi vyeti kwa Wafanyakazi bora

 Katika picha hapo juu ni Meneja Utumishi na Uendeshaji katika Shirika la Masoko ya Kariakoo Bwana Godwin Mrosso anayepiga makofi mara baada ya kumkabidhi cheti maalum cha ufanyakazi bora Bibi Romana Lukanga  aliyeshika cheti,na aliyesimama katikati ni Bwana Joseph Mweyo ambaye ni Mwenyekiti wa TUICO katika Shirika la Masoko; na ambaye ameshika bahasha kulia kabisa ni Bibi Ester Chogero yeye ni Katibu wa TUICO hapa katika Shirika la Masoko.Meneja Utumishi alimuwakilisha Meneja Mkuu wa Shirika Bwana Florens Seiya ambaye alikuwa na shughuli zingine za kiofisi.Hafla hiyo ilifanyika jana mchana katika Ukumbi wa mikutano wa Shirika.
 Katika picha hapo juu ni Bibi Primitiva  Kamugisha  Kaimu Meneja wa Idara ya Usafi akipokea cheti cha Ufanyakazi bora kwa niaba ya Mtumishi wa Idara yake ambaye hakuwepo katika hafla hiyo hapo jana.
 Aliyesimama ni Bibi Romana Lukanga akitoa shukrani kwa Uongozi wa Shirika  kwa niaba ya Wafanayakazi bora waliotunukiwa vyeti,pamoja na shukrani lakini pia aliwasisitiza wafanyakazi wenzake waliopata vyeti hivyo kuwa wasibweteke nakuona kuwa wameshashinda bali inawapasa kuongeza bidii katika utendaji wao wa kazi ili wazidi kuwa mfano mara kwa mara katika Shirika.
 Katika picha hapo juu aliyesimama ni Meneja wa fedha katika Shirika la Masoko Mrs.Marieta Massaua akitoa  pongezi kwa Watumishi wa Shirika walioshinda na kuwa Wafanyakazi bora katika Shirika.Hafla hiyo iliyofanyika jana mchana katika Ukumbi wa Mikutano wa Shirika.
Bwana Ibrahim Masha akiwa amesimama kutoa nasaha kwa Watumishi wa Shirika waliohudhuria hafla ya kukabidhi vyeti kwa Wafanyakazi bora wa Shirika kwa mwaka 2012/2013.Hafla hiyo ilifanyika jana mchana katika Ukumbi wa Mikutano wa Shirika. Bwana Ibrahim Masha yeye ni Mjumbe wa halmashauri ya TUICO ngazi ya Taifa.

Thursday, September 4, 2014

Coneflowers & Salad

Coneflowers na Salad ni miongoni mwa mbogamboga ambazo hufikishwa sokoni Kariakoo kila siku.
Mboga hizi zinazalishwa mikoa ya Morogoro,Tanga na Arusha kwa  hapa Tanzania.
Karibu upate mbogamboga zilizo "fresh"

Wednesday, September 3, 2014

Matunda katika Soko Kuu la Kariakoo


 Aina hii ya maembe ni nzuri sana kwa kuandaa juisi na matumizi mengineyo! mahali pazuri yanapopatikana kwa bei nzuri ni katika Soko kuu la Kariakoo. Kwa bei ya jumla na rejareja utapata bila taabu! Katika soko hili maarufu kila aina ya matunda hupatikana muda wote katika mwaka!Fika eneo la Shimoni katika eneo la matunda.Karibu sanaa!


Tuesday, September 2, 2014

Nyanya Bora zinapatikana Soko Kuu la Kariakoo

 Katika picha hapo juu ni Mama Mjasiriamali ambaye alijitambulisha kwa jina la Mama Shakila; Mama huyu hufanya biashara ya nyanya katika Soko Kuu la Kariakoo eneo la Shimoni kuanzia mapema asubuhi hadi jioni.Katika mahojiano aliniambia nyanya hizi kwa majira haya zinatoka mkoani Morogoro.
Sokoni Kariakoo ni mahali pekee amabapo unaweza kupata bidhaa bora na ambazo zinaweza kukidhi mahitaji yako ya kila siku kwa bei ya wastani.Kama katika picha hapo juu nyanya nzuri amabazo zipo katika kiwango safi cha ubora zinapatikana hapa sokoni. Ukifika Kariakoo tunakukaribisha katika eneo la Soko la jumula na rejareja eneo la Shimoni. Nyanya ni moja bidhaa kadhaa ambazo husafirishwa kwenda katika visiwa vya Commoro. Karibuni mjipatie bidhaa hizi bora!