Tuesday, October 28, 2014

Mkutano wa Bodi ya Ushauri ya Shirika la Masoko Kariakoo

 Katika picha hapo juu ni Wajumbe wa Mkutano wa Bodi ya Ushauri ya Shirika la Masoko ya Kariakoo wakiwa wanatoka kwenda kupanda basi maalumu lililokuwa  limekodiwa kwa ajili ya kwenda kutembelea na kukagua mali za Shirika. Aliyetangulia mbele ni Meneja Mkuu wa Shirika Bwana Florens Seiya na anayefuata ni Mwenyekiti wa Bodi Bwana Wilson Kabwe.Hii ilikuwa ni mojawapo ya agenda za kikao hicho cha Bodi.
 Miongoni mwa Wajumbe waliohudhuria Mkutano wa  Bodi ya Ushauri wakipanda basi tayari kwa safari kuelekea maeneo ya Mbezi Beach ambako ziko nyumba za Shirika la Masoko ya Kariakoo, mwishoni mwa wiki iliyopita.
 Wajumbe wa Mkutano wa Bodi ya Ushauri wakiwa wamefika mahali zilipo nyumba za Shirika la Masoko ya Kariakoo.Katika picha Mwenyekiti wa Bodi hiyo Bwana Wilson Kabwe akiwasalimia Wajumbe wa Mkutano huo.
 Wajumbe wa mkutano wa Bodi wakitembea kuelekea katika geti la nyumba mojawapo eneo la Mbezi Beach Makonde, huku wakiongozwa mbele na Afisa Usalama Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo Bwana Josam Mnzava ambaye ameshikilia radio Call.
 Wajumbe wa Mkutano wa Bodi ya Ushauri ya Shirika wakiwa nje ya geti la nyumba mojawapo ya Shirika la Masoko Kariakoo,nyumba hizi zipo eneo la Mbezi Beach Mtaa wa Makonde.Anaye toa maelezo hapo ni Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo Bwana Florens Seiya.Hii ilikuwa ni mwishoni mwa wiki liyopita.
 Wajumbe wa Bodi ya ushauri walipata nafasi ya kutembelea na kukagua mali zinazomilikiwa na Shirika la Masoko ya Kariakoo.Hapo juu katika picha ni wajumbe hao walipokuwa eneo la Tabata bima Jijini Dar Es Salaam, ambako walifika kuona nyumba za Shirika hilo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Shirika la Masoko ya Kariakoo Bwana Wilson Kabwe ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Jiji la Dar Es Salaam.Katika picha alikuwa akifungua Mkutano wa Bodi  mwishoni mwa wiki iliyopita.Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Shirika la Masoko ya Kariakoo.

Monday, October 20, 2014

Wafanyabiashara wa Soko Kuu la kariakoo

Katika picha hapo juu ni miongoni mwa Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kariakoo wakiwa katika moja ya Masoko ya nje ambayo hufanyika Osterbay na Masaki jijini Dar Es Salaam siku za Jumamosi na Jumapili.Lakini pia katika Masoko haya huwashirikisha wakulima kutoka Wilaya ya Korogwe ambao husimamiwa miradi yao ya uzalishaji mali na matandao wa 2SEEDS Network.

Monday, October 13, 2014

Miongoni mwa Tunu za Hayati Baba wa Taifa Mwl.Julius K.Nyerere ambazo zingali zinaishi hadi leo!

 Ni miaka 15 tangu Baba wa Taifa alipotutoka Watanzania na Ulimwengu kwa ujumla,lakini angali anaishi pamoja na Watanzania wa aina zote.Shirika la Masoko Kariakoo ni mojawapo ya Mashirika yaliyoanzishwa wakati wa uongozi wake mnamo mwaka 1974 kwa sheria ya Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.Soko Kuu la Kariakoo lilianzishwa maalum kwa ajili ya  Watanzania hasa wakulima na Wafanyabiashara wadogowadogo waendeshe shughuli zao hapa ili kuwakomboa kimaendeleo.Mwalimu alimjali kila mwananchi kwa nafasi yake.

 Katika picha hapo juu ni Soko Kuu la Kariakoo katika mwaka wa 1975 mara baada ya kufunguliwa rasmi na Baba wa Taifa Hayati Mwl.Julius K. Nyerere.Wakati huu Soko Kuu la kariakoo lilikuwa na Wafanyabiashara kati ya 200 hadi 300, ambao walikuwa wakifanya biashara zao hapa.

 Hii ilikuwa ni tarehe 8/12/1975 Hayati  Mwalimu Julius K.Nyerere wakati huo akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaonekana akikata utepe kama ishara ya kufungua rasmi Jengo la Soko Kuu la Kariakoo.Ujenzi wake uligharimu kiasi cha Shilingi 22,000,000/=fedha za Kitanzania na pia lilijengwa na Wakandarasi wazawa tangu uchoraji na usanifu wa ramani kazi ambayo ilifanywa na Mhandisi Mzee wetu Beda Amuli nakujengwa na Kampuni ya MECCO kwa wakati. Jengo hili kwa sasa linakadiriwa kuwa na thamani ya Sh.Bilioni 50.

Picha hii hapo juu inaonyesha watumiaji wa Soko Kuu la Kariakoo wakiwa wameongeza sana, hii ni miaka ya hivi karibuni. Wananchi wengi wakiwa wamejaa kupata mahitaji mbalimbali.

Tutakukumbuka daima kwani umetuachia Tunu za kila aina katika Taifa hili.