Friday, March 28, 2014

2SEEDS Network katika Ziara yao Kariakoo

 Katika picha hapo juu ni miongoni mwa Watumishi wa mtandao wa 2SEEDS waliotembelea mapema leo Sokoni Kariakoo.Hapa walikuwa wakipata chakula cha mchana pamoja na mwenyeji wao Bwana Vedastus Valentine ambaye ni Mtumishi wa Shirika la Masoko ya Kariakoo katika Idara ya Biashara.Idadi kubwa ya Watumishi wa 2SEEDS Network huishi Wilayani Korogwe wakifanya shughuli mbalimbali za kiuzalishaji wakishirikiana na Wakulima wadogowadogo kwa lengo la kukuza vipato vya Wakulima hao.
Katika picha  hizo hapo juu ni miongoni mwa Watumishi wa kutoka katika Asasi isiyokuwa ya Kiserikali ijulikanayo kwa jina la 2SEEDS Network yenye Makao Makuu yake nchini Marekani. Leo walikuwa wametembelea Sokoni Kariakoo na kuona maenedeleo ya Mradi ambao wanaufanya kwa ushirikiano na Shirika la Masoko ya Kariakoo.Lakini pia walipata nafasi yakuongea na baadhi ya Wafanya biashara hapo Sokoni.