Thursday, August 20, 2015

SHIRIKA LA MASOKO YA KARIAKOO



TANGAZO LA KAZI

Shirika la Masoko ya Karikaoo ni Shirika la Umma lililoanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Bunge Na.32 ya mwaka 1974 na kupewa majukumu ya kusimamia na kuendesha Soko Kuu la Kariakoo pamoja na Masoko mengine yatakayokuwa chini ya usimamizi wa Shirika pia kujenga Masoko mengine mapya katika Jiji la Dar es Salaam na kusimamia uendeshaji wake. Shirika linakaribisha maombi ya nafasi  mbili za kazi zifuatazo:
  1. Mwanasheria  Daraja la 11
Muombaji awe na Shahada ya Sheria kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na Serikali. Awe amepitia Shule ya Sheria na kusajiliwa kama Wakili.
Kazi na Majukumu.
Kushauri masuala ya kisheria katika Shirika la Masoko ya Kariakoo.
Kuandaa nyaraka zote za kisheria kwa ajili ya kusaidia kufikia malengo ya Shirika.
Kufuatilia na kutunza kumbukumbu muhimu kwa ajili ya kutumika kwenye mashauri Mahakamani.
Kuandaa mihutasari ya mashauri mbalimbali ya shirika yaliyopo mahakamani.
Kuandaa na kupeleka notisi za kisheria kwa wadaiwa wa shirika  .
Kufanya shughuli yeyote atakayo pangiwa na Meneja Mkuu au Mkuu wa kitengo.
  1. Ofisa Ugavi Msaidizi
Muombaji awe na Stashahada ya katika fani ya ununuzi na ugavi, awe amesajiliwa na PSPTB
Kazi na Majukumu.
Kuhakikisha kuwa vifaa vinavyonunuliwa vinapokelewa na kuingizwa katika vitabu vya Shirika..
Kuhakikisha kuwa nyaraka zote za stoo zinajazwa kwa ufasaha na kwa wakati.
Kuhakikisha kuwa mali zote zilizoifadhiwa stoo zinatuzwa  bila upotevu wowote.
Kuhakikisha kuwa uingizaji na utoaji wa bidhaa unafuata sheria na kanuni za manunuzi ya umma.
Kuhakikisha kuwa vifaa na mali zinazohifadhiwa stoo zinatunzwa katika mpangilio mzuri
Kufanya kazi zozote atakazopangiwa na Mkuu wa Kitengo.
MASHARTI YA JUMLA
Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
 Waombaji wote waambatishe nakala ya cheti cha kuzaliwa. Na picha (passport size) moja ya rangi
Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
Maombi yote yaambatane na nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na nakala ya  vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.

Mwisho wa Kupokea maombi ni 29/08/2015.

Maombi hayo yatumwe kwa :

Meneja Mkuu,
Shirika la Masoko ya Kariakoo,
P.O.BOX 15789,
Dar es Salaam.
Na kwa Email: info@kariaakoo.or.tz.