Sunday, January 11, 2015

Kutoka Soko Kuu la Kariakoo

 Katika picha hapo juu ni mjumbe akiwa anasaini daftari la mahudhurio katika Ukumbi wa Mikutano wa Shirika la Masoko ya Kariakoo.Mwishoni mwa wiki iliyopita siku ya Jumamosi Chama Kikuu cha Ushirika cha  Akiba na Kukopa SACCOS ambacho kinawashirikisha  Wafanyakazi wa Shirika, kilifanya Mkutano muhimu wa kuwapata Viongozi wapya wa kukiongoza Chama hicho kwa muda wa miaka mingine mitatu.
 Katika picha hapo juu ni baadhi tuu ya Wajumbe wapya wa Bodi ya SACCOS kutoka  kushoto ni Bwana Yustino Man mwenye shati nyeusi,wapili ni Bwana Dennis Mfuruki na wa mwisho ni Bwana James Kanyiriri wakiwa katika ukumbi wa mikutano katika Soko kuu la Kariakoo.
 Miongoni mwa Wajumbe (Wanachama) wa Chama cha Ushirika cha Akiba na Kukopa Soko Kuu Savings LTD waliohudhuria mkutano maalum huo uliofanyika Jumamosi iliyopita katika Ukumbi wa Mikutano. Mkutano huo ulikuwa na Agenda moja tuu ya kuwachagaua viongozi wapya wa Ushirika huo.
Wajumbe wa Kamati ya Usimamizi waliochaguliwa ni Bwana Bolingo Malya,Ncheye Kulwa Ncheye na Onesmo Sinziga
Bwana Godwin Mbuya akisaini akisaini karatasi maalumu ya mahudhurio aliyeshika karatasi kuhakiki jina la mwanachama huyo ni Makamu Mwenyekiti Bwana Mohamed Chikwama.
Mkutano huo uliwachagua Bwana Dennis Mfuruki,James Kanyiriri,Mohamed Chikwama,Yustino Man,Alphonce Mweri na Anderson Shaka Mjanga kuwa Wajumbe wa Bodi wa Saccos hiyo.