Wednesday, October 23, 2013

YALIYOJILI KATIKA HARUSI YA MKUU WA KITENGO CHA ICT -KARIAKOO


Muda mfupi kabla ya kuanza ibada ya ndoa katika Kanisa la KKKT Kijitonyama Jijini Dar Es Salaam;kutoka kushoto ni Bwana harusi Anderson Shaka Mjanga na bestman wake bwana Aron Mjema,wengine ni Frank Mangowi mfanyakazi wa kitengo cha ICT KMC na mwingine ni Kamili Simba pia mfanyakazi wa KMC


Muda mfupi kabla kufunga ndoa Bwana Harusi na Best Man wake wakiwa katika viwanja vya kanisa la KKKT Kijitonyama Jijini Dar Es Salaam. Hii ilikuwa Jumamosi  ya tarehe 19/10/2013

Bwana na Bibi harusi wakiwa wamepozi katika picha ya pamoja mara baada ya kufunga ndoa yao Jumamosi ya tarehe 19/10/2013.
Katika picha hapo juu ni kikundi cha Matarumbeta cha Kanisa la KKKT Kijitonyama jijini DSM kikitumbuiza kanisani hapo mara baada ya Bwana Anderson Shaka Mjana Na Bi Neema Elibariki Mshanga kufunga ndoa yao kanisani hapo Jumamosi ya tarehe 19/10/2013. Bwana harusi ni Mkuu wa Kitengo cha ICT katika Shirika la Masoko ya Kariakoo na Bibi harusi ni Mjasiriamali.

 
Maharusi wakiwa katika picha ya pamoja na ndugu na jamaa  mara baada ya kufunga ndoa katika Kanisa la KKKT Kijitonyama Jijini Dar Es Salaam,Jumamosi ya tarehe 19/10/2013.

Maharusi wakiwa katika picha ya pamoja na Wazazi wa pande zote mbili yaani familia ya Mzee Mjanga na Mzee Mshanga;mara baada ya vijana wao kufunga ndoa jumamosi ya tarehe 19/10/2013, kanisani Kijitonyama KKKT.

Ndugu wa Bwana harusi wakifurahia mara baada ya Ibada ya kufunga ndoa kumalizika kati ya Bwana Anderson Shaka Mjanga na Bi Neema Elibariki Mshanga KKKT pale Kijitonyama.Mwenye suti kushoto ni mdogo wake na Bwana harusi Daktari S.Mjanga toka Hospitali ya Mkoa wa Morogoro;na mwingine ni binamu yake na Bwana harusi.
Muda mfupi baada ya Bwana Anderson Shaka Mjanga  kufunga ndoa  na Bi Neema Elibariki Mshanga.
Katika picha hapo juu ni kikundi cha mameds waliopamba sherehe za harusi ya Bwana Anderson Shaka na Bi Neema Mshanga kwa kucheza Show kali! iliyofanyika Jumamosi ya tarehe 19/10/2013.Ndoa ilifungwa katika kanisa la KKKT Kijitonyama na baadaye tafrija fupi kufanyika katika Ukumbi wa Dolphin 1998 LTD uliopo Sinza karibu na S/Msingi Mugabe.kutoka kushoto ni Everine,Erica,Amina,Munira na Joyce.

  Katika picha hapo juu ni kikundi cha mameds waliopamba sherehe za harusi ya Bwana Anderson Shaka na Bi Neema Mshanga kwa kucheza Show kali! iliyofanyika Jumamosi ya tarehe 19/10/2013.


PATA BIDHAA BORA KUTOKA SOKO LA KARIAKOO

Pichani ni Mhasibu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo (KMC) Bw. Ibrahim Marsha aikwa ofisini kwake hivi karibuni. katika mahojiano yaliyofanywa baina ya mchambuzi wa maswala ya ICT ya Shirika la Masoko ya Kariakoo (Frank Mangowi) hayupo pichani. Marsha alielezea historia fupi ya Shirika la Masoko ya Kariakoo, bofya hapa ili kupata historia ya Shirika la Masoko ya Kariakoo.




Aidha Marsha anachukua nafasi muhimu kuwakaribisha wateja kujipatia bidhaa mbalimbali zinazopatikana sokoni Kariakoo Jijini Dar es Salaam Tanzania.

Hapa ndipo Kariakoo Sokoni, picha ikionesha Soko kubwa(kushoto) na Soko dogo(kulia) la Kariakoo jijini Dar es Salaam.