Monday, October 7, 2013

TAA MPYA ZAFUNGWA SOKONI KARIAKOO

Fundi umeme wa Shirika la Masoko ya Kariakoo akifunga taa mpya katika Soko la Kariakoo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kufanya shughuli za biashara kuendeshwa nyakati za usiku hapa sokoni.






Mafundi umeme wa Shirika la masoko ya Kariakoo bwana Rogers Kuyonga na Mdami wakiwa katika kazi ya kufunga taa kubwa ambazo zitatumika kutoa mwanga wa kutosha nyakati za usiku kwa ajili ya shughuli za biashara; hii itawawezesha hata wateja wale ambao wamekuwa wakikosa kupata huduma wakati wa mchana kuweza kufika hapa sokoni majira ya usiku na kununua bidhaa wanazozihitaji.



Pichani mafundi wa Shirika la Masoko wakishirikiana katika kazi ya kufunga taa mojawapo mwishoni mwa wiki iliyopita! Hii ni sehemu ya maandalizi ya kuliwezesha Soko la Kariakoo kutoa huduma zake hata nyakati za usiku kwa wateja wake!





Mafundi wapo kaziniiii! kuhakikisha mikakati ya Shirika ya kuweza kuwahudumia wananchi wa Jiji la Dar Es Salaam na vitongoji vyake hata nyakati za usiku inafanikiwa,hivi karibuni!