Monday, June 15, 2015

Mradi wa Vitunguu saum- Bombo Majimoto Korogwe

Picha ya hapo juu inaonyesha mojawapo ya Nyumba za mazao(Green House) ambazo ndani yake kama unavyoweza kuona mna matuta kadhaa ya vitunguu saum.Mradi huu umeonekana kuwa wenye kuleta mafanikio makubwa kwa wanakikundi cha Bombomajimoto,ambapo mbali ya shamba hili la pamoja tayari kila mwanakikundi ameanzisha shamba lake binafsi ili aweze kustawisha zao hili la vitunguu saum.

 Katika picha hapo juu ni sehemu tuu ya  matuta katika shamba la  vitunguu saum vinavyoendelea kustawishwa na wanakikundi hiki cha Bombomajimoto huko Korogwe Vijijini chini ya uangalizi wa Shirika la 2Seeds Network.

 Katika picha hapo juu ni kabati ambalo linatumiwa na Wanakikundi  cha BomboMajimoto kutunzia vifaa mbalimbali yakiwemo madawa maalum kwa ajili ya kutunza mazao katika mashamba yao.
 Hapo juu ni picha ya pamoja ya Wanakikundi wa Bombo Majimoto na wageni waliowatembelea kuona maendeleo ya mradi wa vitunguu saum unaoendeshwa kwa njia ya kilimo cha kawaida na kwakutumia mfumo wa nyumba za mazao(Green house). Kutoka kushoto ni Bwana Anderson Shaka Mtaalamu wa Mawasiliano kwa njia ya Kompyuta  kutoka Shirika la Masoko Kariakoo, wapili ni Mama Tatu Mwanakikundi, Bwana Vedastus Valentine Afisa Biashara kutoka Shirika la Masoko Kariakoo, Bwana Shebe mwanakikundi  ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kikundi na aliyekaa ni Bwana Hamdani naye ni Mwanakikundi.
Afisa biashara wa Shirika la Masoko Kariakoo aliyesimama katikati Bwana Vedastus Valentine akiwapa ushauri Wanamtandao wa 2Seeds Network wa kikundi cha Bombo Majimoto Korogwe Vijijini wakati alipowatembelea ili kujionea maendeleo ya mradi huo wa vitunguu saum.wengine waliosimama aliyevaa kofia ni Bwana Shebe ambaye ni mwenyekiti wa Kikundi cha mradi huo na mwingine ni Bwana Hamdani.