Friday, May 8, 2015

SEMINA YA UKIMWI & KIFUA KIKUU Sokoni Karikoo

 Katika picha hapo juu inaonesha muda mfupi kabla ya Semina kuanza ndani ya Ukumbi wa Shirika la Masoko Kariakoo siku ya Jumatano. Kutoka kulia wakwanza ni Dk.Leah Mtui wapili ni Bwana Chiziza Nelson wote wawili ni wafanyakazi kutoka shirika lisiliokuwa la Kiserikali linaloitwa PASADA, na watatu ni Meneja Utumishi na Uendeshaji wa Shirika la Masoko Kariakoo Bwana Godwini Mrosso. Wote wakimsikiliza Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko Kariakoo pichani hayupo.
 Katika picha hapo juu ni Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko Kariakoo Bwana Florens Seiya alipokuwa akitoa maneno ya kuwakaribisha Wawezeshaji wa semina pamoja na Watumishi wa Shirika waliohudhuria semina hiyo maalum. Meneja Mkuu huyo kama Mkuu wa Taasisi aliwaasa wanasemina kufuatilia kwa makini mafunzo hayo yaliyolenga kuwajengea uelewa zaidi kuhusu ugonjwa wa Ukimwi na Kifua Kikuu.Semina hiyo ilifanyika siku mbili Jumanne na Jumatano, siku ya Jumanne semina hiyo iliwahusisha Wafanyabiashara wa Soko la Kariakoo na siku ya Jumatano iliwalenga Watumishi wa Shirika.
 Meneja wa Idara ya Afya na Usafi wa Shirika la Masoko Kariakoo Bwana Donald T.Sokoni akiwa anatoa ukaribisho kwa wanasemina kabla ya kuanza.Hii ilikuwa siku ya Jumatano asubuhi,na semina hiyo ilifanyika ndani ya Ukumbi wa Shirika hilo.
 Bwana Chiziza Nelson ambaye amesimama ni  moja ya Wawezeshaji wa semina hiyo iliyofanyika katika Shirika la Masoko Kariakoo siku ya Jumanne na Jumatano wiki hii. Semina ilikuwa ililenga kuwajengea ufahamu zaidi juu ya magonjwa mawili yakiwa ni Ukimwi na Kifua Kikuu.
 Bwana Nasoro Said mwenye shati la mistari akiwa anamsikiliza kwa utulivu kabisa Muwezeshaji wa Semina Dk.Leah Mtui kutoka shirika la PASADA pichani hayupo wakati anaendelea kutoa mafunzo yahusuyo ugonjwa hatari wa Ukimwi.
 Sehemu ya Wanasemina waliohudhuria wakiwa wameketi na kufuatilia kwa umakini sana mafunzo yaliyokuwa yanaendelea kutolewa na wawezeshaji kutoka shirika lisilokuwa la Kiserikali liitwalo PASADA hii ilikuwa ni siku ya Jumatano wiki hii.
 Katika picha hapo juu aliyesimama ni Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko Kariakoo Bwana Florens Seiya akitoa maneno ya shukrani kwa wawezeshaji wa semina iliyokuwa inahusu Ukimwi na Kifua Kikuu,mara baada ya kufikia mwisho wa mafunzo yaliyotolewa na Wafanyakazi wa Taasisi isiyokuwa ya Kiserikali ijulikanayo kwa jina la PASADA.
Kazi na dawa kwelikweliii! Hapa katika picha ni sehemu ya Watumishi wa Shirika la Masoko ya Kariakoo wakiwa wanapata chakula mara baada ya kuhitimisha Semina maalumu iliyokuwa inahusu kuwajengea uelewa kuhusu magonjwa ya  Ukimwi na Kifua Kikuu.Semina hiyo iliyofanyika katikati ya wiki hii siku ya Jumanne na Jumatano katika ukumbi wa Shirika hilo ilikuwa yenye manufaa zaidi kwa Taasisi hiyo na mtu mmojammoja pia!