Katika picha hapo juu aliyesimama ni Bwana Paul Nsimbila Mtaalam wa Manunuzi kutoka PPRA akiwa amemaliza kugawa karatasi za maswali kwa Watumishi wa Shirika la Masoko ya Kariakoo ambao wanahudhuria Semina kuhusu manunuzi ya Umma.Mkufunzi Bwana Nsimbila alianza kutoa mafunzo hayo jana Jumatatu asubuhi katika Ukumbi wa mikutano wa Shirika hili, pamoja na mambo mengine Bwana Nsimbila anatoa mafunzo kuhusu Sheria mpya ya manunuzi pamoja kanuni zake ili kuwajengea uwezo watumishi wa shirika hili katika kutekeleza shughuli za manunuzi kwa weredi na kuleta tija kwa Shirika.
Katika picha hapo juu ni Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko la Kariakoo Bwana Florens Seiya na Meneja wa Fedha Bi.Marieta Massaua wakiwa wanajadiliana swali ambalo Mkufunzi Muwezeshaji kutoka PPRA Bwana Paul Nsimbila alikuwa ametoa kwa kila watu wawiliwawili ili kupima uelewa kuhusu namana ya kupangilia mpango mzima wa manunuzi wa mwaka ndani ya taasisi. (Annua Procurement Plan)
Watumishi hawa katika picha kutoka kutoka Vitengo vya Manunuzi na Ukaguzi wakiwa wanaendelea na kufanya swali linalohusu (APP) yaani Annual Procurement Plan, kutoka kulia ni Bwana Mathias Mbafu (Mkuu wa kitengo cha Manunuzi), Bi.Henrika Kawili (Afisa Manunuzi na Ugavi), Bwana Longino Rugaikamu na Yustino Man wote kutoka Kitengo cha Ukaguzi.
Hapo juu pichani ni Bwana Flavian Mlelwa ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Matunzo akiwa na Bi.Dayness Sooyi wakiendelea kufanya swali lililotolewa na Mkufunzi Muwezeshaji kutoka PPRA Bwana Paul Nsimbila, hii ni mapema leo asubuhi kabla ya somo jipya kuhusu sheria mpya ya manunuzi ya Umma na kanuni zake.
Katika picha hapo juu ni Mkuu wa Kitengo cha Tehama Bwana Anderson Shaka Mjanga kushoto akiwa na Bwana Marco Mganga, Afisa Manunuzi kutoka Kitengo cha Manunuzi, kwa pamoja wakijadiliana swali linalohusu mpango wa manunuzi wa mwaka.
Mkaguzi Mkuu wa ndani Bwana Paul Kiwera akiwa na Muhasibu Bi.Semeni Yamawe kwa pamoja wakiendelea kulichambua swali linalohusu Mpango wa manunuzi wa mwaka au Annual Procurement Plan kwa lugha ya kiutalaam. Bwana Paul Nsimbila Muwezeshaji katika mafunzo haya alitoa kuwapa watu walifanye ili ajiridhishe kuona kile anachowafundisha Watumishi hawa wanaelewa hasa na kwamba wataweza kufanya kwa vitendo mara baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo?
Watumishi wawili wa mwanzo ni Bwana Ncheye Kulwa na Luchemo Chiimba wote kutoka katika Kitengo cha Ukaguzi wakiwa makini kufuatilia jambo wakati mafunzo yakiendelea Ukumbini.Mafunzo hayo yakuwajengea uwezo Watumishi hawa wa Shirika yamekusudiwa kuwa ni siku tatu (3) yalianza jana Jumatatu 9/02/2015 na yatamalizika Jumatano ya wiki hii tarehe 11/02/2015
No comments:
Post a Comment