Friday, February 28, 2014

Watumishi wa Shirika la Masoko ya Kariakoo.


Pichani hapo juu ni Bwana Ncheye Kulwa akiwa ofisini kwake ,yeye ni Mkaguzi wa ndani.
Bwana Luchemo Chiimba kutoka katika Kitengo cha Ukaguzi wa ndani akiendelea na shughuli zake za kila siku.


Bwana Yustino Man kutoka katika Kitengo cha Ukaguzi wa ndani katika Shirika la Masoko akifanya kazi zake kama alivyokutwa mapema leo ofisini kwake.

Katika picha hapo juu ni bwana Charles Sombe akiwa ofisini kwake yeye ni Afisa Utumishi msaidizi.

Bwana Charles Simba akiwa makini kuziangalia nyaraka zilizomfika ofisini kwake leo asubuhi ili aweze kuzihifadhi yeye ni Record Management Officer (RMO) wa Shirika la Masoko

Monday, February 24, 2014

WAFANYA BIASHARA WAKIENDELEA NA SHUGHULI ZAO ZA KILA SIKU SHIMONI KARIAKOO

Pichani ni baadhi ya bidhaa zinazopatikana Shimoni Kariakoo. Ikionesha unaweza kupata viazi, vitunguu na bidhaa nyingine nyingi. Viazi vinavyoonekana pichani hapo juu vinauzwa shilingi 800 kwa kilo moja.
Mfanyabiashara maarufu wa Viazi akifurahuia namna Shirika la Masoko la Kariakoo linavyootumia Teknologia  katika kupanua wigo wa biashara ndani na nje ya Tanzania. Unaweza kumpata :Bwana Shomari Mkang'a mfanya biashara huyu kwa mawasiliano yafuatayo  Simu :0716 231524
 

Friday, February 21, 2014

Habari za leo kutoka Shirika la Masoko ya Kariakoo Jijini Dar Es Salaam-Tanzania


 Katika picha hapo juu ni Wajumbe wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Shirika la Masoko Kariakoo ambacho kimefanyika leo Ijumaa tarehe 21/2/2014 katika ukumbi wa mikutano wa shirika hilo.
 Wajumbe wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi  wakimsikiliza Meneja Mkuu wa shirika la Masoko ya Kariakoo yeye kama Mwenyekiti wa kikao hicho alipokuwa akiongoza leo Ijumaa tarehe 21/2/2014.
 Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya kariakoo Bwana Florence  Seiya akifafanua jambo wakati wa kikao cha baraza la Wafanyakazi katika shirika la Masoko Kariakoo-(SMK); kwa kawaida kikao hiki huhudhuriwa pia na Mjumbe mmoja wa TUICO kutoka  Ofisi kuu ya TUICO mkoa.
 Katika picha hapo juu  ambaye amesimama na kunyosha mkono ni Katibu Mkuu wa TUICO kutoka mkoa wa Ilala DSM akiwaaga wajumbe wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi; mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho.
Katika hapo juu ni Katibu wa TUICO toka mkoani Ndugu Willy Kibona  katikati;akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa TUICO katika Shirika la Masoko ya Kariakoo, Bibi Ester Chogero Katibu na Bwana Ncheye Kulwa ambaye ni Mjumbe wa TUICO katika Shirika
Mzee Rashid Nguyu (Mfanyakazi wa Shirika)akiwa katika kikao cha baraza la wafanyakazi  akiwa amepozii akifuatilia  maelezo ya Meneja Mkuu  pichani hayupo, pembeni yake katika kiti ni kabrasha lake alilokuwa amepewa siku (3) kabla ya kikao hicho.

Tuesday, February 18, 2014

JIPATIE BAISKELI ZA WATOTO KWA BEI YA 80,000/= TU

Nunua baiskeli kwa ajiri ya mtoto wako kwa shilingi 80,000/= tu hapa sokoni Kariakoo.
Piga simu  kwa Emma Macherehani

0755 363157
0717 830813





Thursday, February 13, 2014

MAZUNGUMZO; MATUKIO KATIKA PICHA



Meneja Mkuu Ndugu Frolens M. Seiya akiwa ofisini kwake na wageni kutoka Asasi ya 2Seeds Network kutoka Marekani hawapo pichani. 

Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo (kulia) na James Meeks Mkuu wa asasi ya 2Seeds Network nchini Marekani (wa pili)

Wageni wakipata matunda huku mazungumzo yakiendelea ofisini kwa Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo Jijini Dar es Salaam

Wageni na wenyeji wakimsilikiliza kwa Makini Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo Ofisini kwake 

 James Meeks pamoja na Meneja Mkuu  la Masoko ya Kariakoo (walio simama katikati) wakiwa nje ya ofisi 

James Meeks Mwenyekiti wa 2Seeds Network toka nchini Marekani  akiagana na Meneja Mkuu  wa shirika  Frolens M. Seiya  baada ya Mkutano  uliokuwa unahusu taarifa ya maendeleo ya mradi wa Masoko(Masoko Project) unaohusu Mfumo wa ukusanyaji na utoaji taarifa za mazao yanayoingia katika soko kuu la Kariakoo la Jijini  DSM-Tanzania

James Meeks akiagana na Meneja Mkuu  wa Shirika  Ndugu Frolens M. Seiya

Mtakwimu mkuu wa Shirika la Masoko Henry Rwejuna Mutungi akimwonesha James Meeks mfumo mpya wa ukusanyaji bei za mazao kwa kutumia simu ya kiganjani. Huku taarifa hizo zikirushwa moja kwa moja kwenda kwenye
 tovuti ya Shirika la Masoko.

Sunday, February 9, 2014

PATA SAMAKI WABICHI KATIKA MADUKA YA SAMAKI NDANI YA SOKO KUU LA KARIAKOO

Wateja wakinunua samaki wabichi katika duka mojawapo la samaki lililopo ndani ya soko Kuu la Kariakoo Jijini Dar es Salaam, Tanzania. Samaki wanaouzwa hapa ni kingfish kutoka katika Bahari ya Hindi. Hapa unaweza kununua samaki hawa kwa vipande ama  kwa kilo. Kipande kimoja cha samaki kinauzwa shilingi 1,000/= tu! Karibuni wateja wetu wote mjipatie samaki bora kutoka soko Kuu la Kariakoo Jijini Dar es Salaam.

Mteja akinunua samaki mapema leo asubuhi

Thursday, February 6, 2014

ROMANA R. LUKANGA, MTUMISHI MPYA WA IDARA YA BIASHARA KATIKA SOKO KUU LA KARIAKOO

Pichani hapo juu ni watumishi wakiendelea na kazi katika ofisi za Shirika la masoko Kariakoo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Romana R. Lukanga ambae ni Mtumishi mpya katika idara ya biashara ndani ya Shirika la Masoko Kariakoo, kulia ni Henry R. Mutungi ambae mtakwimu wa Shirika la Masoko Kariakoo.

Tuesday, February 4, 2014

MATUKIO KATIKA PICHA LEO ASUBUHI SOKONI KARIAKOO


Wateja wakiwa sokoni Kariakoo Jijini Dar es Salaam wakijipatia baadhi ya bidhaa bora kama inavyoonekana katika picha hapo juu. Hapa unaweza kupata karoti, hoho, bamia na bidhaa nyinginezo nyingi kama inavyoonekana pichani.


Hili ni eneo la soko la Kariakoo, kwa jina maarufu kama soko la wazi ambalo unaweza kupata mbogomboga, viazi , matunda na bidhaa nyinginezo kama invyoonekana.