Tuesday, August 26, 2014
Usafi katika Soko Kuu la Kariakoo-Dar Es Salaam
Katika picha hapo juu ni Mtumishi wa Shirika la Masoko ya Kariakoo Bwana Amiri Magala akiwa anaendelea na shughuli yake ya kusafisha moja ya mifereji ya maji taka iliyopo eneo la Shimoni. Uongozi wa Shirika huzingatia sanaa suala zima la Usafi katika maeneo yote ya Soko Kuu la Kariakoo ambalo ni maarufu sana kwa kupokea bidhaa mbalimbali za mazao kutoka mikoani.Kwa kuzingatia hilo mifereji hii ya maji taka hukaguliwa mara kwa mara kila siku ili kuhakikisha maji taka yanatoka na kuingia katika mfumo mkuu wa Jiji wa maji taka.
LEEKS ni nini?
Kwa wale wataalam wa mapishi na vyakula hawataweza kushangaa sana kuwa majani haya ni ya nini?au majani gani?
Hii ni mojawapo yambogamboga za majani za kisasa zinazoitwa LEEKS hizi hupatikana pia hapa sokoni Kariakoo kwa wingi sanaa! Fika Sokoni Kariakoo eneo la Shimoni katika meza za mbogamboga! zikiwa bado fresh utazipata! Karibu sanaaaa!

ZUKIN na BLUKOLIN
Katika picha hapo juu sio matango; ila ni moja ya mboga aina ya ZUKIN na BLUKOLIN.Aina hzi za mbogamboga huzalishwa kwa wingi katika mikoa ifuatayo; Morogoro,Tanga katika wilaya za Lushoto,Korogwe na kule Arusha.Fika Sokoni Kariakoo eneo la Shimoni utazipata kwa wingi na bei yake ni nzuri. Karibuni sana!
Saturday, August 23, 2014
Shughuli za biashara sokoni Kariakoo
Shughuli za biashara mbalimbali huendelea katika Soko Kuu la Kariakoo kila siku huanza tangu mapema alfajiri.Hapo katika picha wafanyabiashara wa matunda wakiwa katika eneo lao la biashara.Matunda mengi huuzwa eneo la Shimoni kwa bei ya rejareja na jumla pia.
Thursday, August 21, 2014
Usalama katika Soko Kuu la Kariakoo umezidi kuimarishwa
Katika Soko Kuu la Kariakoo lililopo Jijini Dar Es Salaam usalama kwa Wafanyabiashara na Wateja mbalimbali wanaofika kujipatia mahitaji mbalimbali umezidi kuimarishwa kwa kiasi kikubwa sana. Katika picha hapo juu ni Geti lakutokea soko la jumla lililopo sehemu ya Shimoni; askari akiwa getini kabisa hapo akifanya ukaguzi kwa kila anayepita kuingia au kutoka ndani ya soko.
Tunamkukaribisha kila mmoja Sokoni Kariakoo.
Tunamkukaribisha kila mmoja Sokoni Kariakoo.
Thursday, August 14, 2014
Habari toka Soko Kuu la Kariakoo leo!
Mazao ya mbogamboga na Viungo yanapatikana kwa wingi sana katika soko Kuu la Kariakoo.Kama uonavyo katika picha hiyo hapo juu ni baadhi tuu ya mazao ambayo huingia Sokoni kila siku .
Dagaa hawa maalum wanaopatikana katika Ziwa Nyasa lililopo Kusini Magharibi mwa Tanzania;wana ladha ya kipekee sana wanapatikana pia katika Soko hili kubwa la Kariakoo eneo la Shimoni sehemu ya Wafanyabiashara wa dagaa.Karibuni mjipatie bidhaa hii muhim kwa afya ya familia yako.
Shughuli za biashara katika Soko Kuu la Kariakoo hapa Jijini Dar es Salaam huanza mapema sana alfajiri kila siku.Hapa katika picha utaona Wafanyabiashara wa matunda mbalimbali wakiwa eneo la Shimoni wakiendelea na shughuli zao za kibiashara kama walivyokutwa mapema alfajiri majira ya saa 11.30.
Magunia ya vitunguu yakiwa yamepangwa katika eneo la Soko la Jumla Shimoni Kariakoo Jijini Dar Es Salaam.Vitunguu hivi majira haya vinatoka katika mikoa tofautitofauti ikiwamo Morogoro,Mbeya,Iringa na Dodoma pia.

Subscribe to:
Posts (Atom)