Sunday, March 30, 2014
Friday, March 28, 2014
2SEEDS Network katika Ziara yao Kariakoo
Katika picha hapo juu ni miongoni mwa Watumishi wa mtandao wa 2SEEDS waliotembelea mapema leo Sokoni Kariakoo.Hapa walikuwa wakipata chakula cha mchana pamoja na mwenyeji wao Bwana Vedastus Valentine ambaye ni Mtumishi wa Shirika la Masoko ya Kariakoo katika Idara ya Biashara.Idadi kubwa ya Watumishi wa 2SEEDS Network huishi Wilayani Korogwe wakifanya shughuli mbalimbali za kiuzalishaji wakishirikiana na Wakulima wadogowadogo kwa lengo la kukuza vipato vya Wakulima hao.
Katika picha hizo hapo juu ni miongoni mwa Watumishi wa kutoka katika Asasi isiyokuwa ya Kiserikali ijulikanayo kwa jina la 2SEEDS Network yenye Makao Makuu yake nchini Marekani. Leo walikuwa wametembelea Sokoni Kariakoo na kuona maenedeleo ya Mradi ambao wanaufanya kwa ushirikiano na Shirika la Masoko ya Kariakoo.Lakini pia walipata nafasi yakuongea na baadhi ya Wafanya biashara hapo Sokoni.

Thursday, March 27, 2014
Matunda ya kila aina yanapatikana Kariakoo Sokoni.
Maembe hayo katika picha hapo juu yapo tayari kwa kuuzwa kwa wateja wa jumla na rejareja pia!
Bei yake ni kati ya TSh.500 hadi 700
Katika picha hapo juu ni mifuko ambayo ina matunda aina ya Apples yakiwa yameshushwa toka katika gari mojawapo leo mapema alfajiri. Matunda haya kwa sasa yanatoka katika Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga. Asilimia kubwa ya matunda yanayotoka Lushoto huuzwa katika Soko Kuu la Kariakoo lililopo Jijini Dar Es Salaam.

Wednesday, March 26, 2014
Kariakoo Leo!
Katika picha hapo juu ni moja ya Magari ya mizigo ambayo huleta mazao mabalimbali katika Soko la Kariakoo. Hapo lipo ndani katika Soko la Jumla Shimoni, lilikutwa leo alfajiri likishusha Matunda aina ya Apples toka Lushoto Tanga.
Matikiti haya yanauzwa kwa bei ya Jumula na rejareja Soko kuu la Kariakoo Jijini Dar Es Salaam.Kwa mahitaji ya matunda kila aina fika Kariakoo Shimoni
Matikiti haya yanauzwa kwa bei ya Jumula na rejareja Soko kuu la Kariakoo Jijini Dar Es Salaam.Kwa mahitaji ya matunda kila aina fika Kariakoo Shimoni
Tuesday, March 25, 2014
Mboga za Majani zinapatikana Sokoni Kariakoo pia!
Leo ni mbogamboga tuu! ndugu Mteja mboga hizi zinatokea katika mikoa ya Tanga sehemu za Lushoto,Korogwe na kule mkoani Arusha.
Hapo juu katika picha ni mchanganyiko wa mbogamboga kama vile Zukin hizo zenye muonekano kama matango,Cotmill,Retus na nyinginezo.Hizi zinapatikana Kariakoo sokoni katika eneo la soko wazi.
Thursday, March 20, 2014
Habari toka ndani ya Kariakoo Market Corporation leo
Katika picha hapo juu ni Wanafunzi wanaosoma kozi ya Uhasibu katika chuo cha
The Kilimanjaro Institute of Business & Technology kilichopo Jijini DSM. Wanafunzi hawa wapo katika mafunzo kwa vitendo (PT) katika Shirika la Masoko ya Kariakoo.Hapa wanaelekezwa jambo na Mtumishi mmojawapo wa Shirika mwenye Tsheti nyeupe MrsMwinga. Wanafunzi kutoka kulia ni Pendo Francis,Libelius Vedastus,Elisamehe Temu na Lipina David.
Mwanafunzi huyu Elisamehe Temu akiwa anaendelea na shughuli zake mapema leo asubuhi katika Ofisi za Shirika la Masoko ya Kariakoo;hapa alikutwa akifanya moja ya kazi ambayo alipangiwa na msimamizi wake.

Tuesday, March 18, 2014
TANGAZA BIASHARA YAKO KWA BEI NAFUU
Sasa unaweza kutangaza biashara yako katika mtandao wa Shirika la Masoko Kariakoo (www.kariakooblog.blogspot.com) kwa bei nafuu sanaaa kama inavyoonekana pichani hapo juu. Sehemu zote zinazowakilishwa na herufi zinauzwa. Tangazo lako litalipiwa kwa mwezi. Biashara yako itaonekana Dunia nzima!
NB: bei ya matangazo inaweza kubadilika.
NB: bei ya matangazo inaweza kubadilika.
Thursday, March 6, 2014
SASD TRADING COMPANY: WAUZAJI WA BIDHAA ZA PLASTIC SOKO KUU KARIAKOO
Suleiman Ahmed Dudu akiwa kazini kwake |
Managing Director Suleiman Ahmed Dudu unaweza kumpata kwa mawasiliano yafuatayo |
MATUNDA
Pichani hapo juu ni matunda aina ya maembe yakiwa mezani katika sokoni Kariakoo eneo maarufu kama soko la wazi. Pata maembe safi kutoka kariakoo.
Subscribe to:
Posts (Atom)