Karoti nzuri daraja la kwanza kabisa kutoka Mikoa mbalimbali ya Tanzania.Karibu ujipatie bidhaa hii bora kwa matumizi mbalimbali kama vile kutengeneza juice na nakadhalika.
Katika picha hapo juu ni Viazi mviringo vikiwa bado fresh kabisa kutoka mkoani. Mikoa mashuhuri kwa uzalishaji vyazi hapa nchini ni pamoja na Iringa,Njombe na Mbeya
Sunday, December 14, 2014
Tuesday, December 9, 2014
Kuelekea Sikukuu za Christmas na Mwaka mpya!
Njegere ni moja ya bidhaa adimu na yenye kupendwa sana na watu wengi kwa matumizi ya chakula. Njegere huingia katika Soko Kuu la Kariakoo kutoka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania kama vile Morogoro,Iringa,Njombe na kwingineko. Bidhaa hii kuelekea sikukuu za Christmas na Mwaka mpya bado inapatikana kwa wingi hapa Sokoni hasa eneo la Shimoni.katika picha hapo juu Mfanyabiashara alikutwa na mpiga picha akiwa amekwisha kuzimenya njegere zake tayari kwa kuwauzia wateja mbalimbali.
Sokoni Kariakoo kuna kila aina ya vyakula.Katika picha hapo juu nafaka mbalimbali ambazo huuzwa katika soko Dogo.Mfanya biashara huyu ameweka wazi hata bei za vyakula kwa kuzingatia madaraja au ubora wake.Tunapoelekea katika Sikukuu za mwisho wa mwaka bei za vyakula hazijabadilika sana! Karibuni Sokoni kwa manunuzi ya bidhaa mbalimbali.
Thursday, December 4, 2014
Watumishi KMC
Katika picha hapo juu ni Meneja Utumishi na Uendeshaji Bwana Godwin Mrosso akiwa pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Usalama Bwana Josam Mnzava. Wote ni Watumishi wa Shirika la Masoko ya Kariakoo.
Katika picha hapo juu ni Mkaguzi Mkuu wa Shirika Bwana Paul Kiwera akiwa anabadilishana mawazo na Mwanasheria wa Shirika Bibi.Gloria Kalabamu muda mfupi kabla ya kikao cha Bodi.kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Shirika la Masoko ya Kariakoo.
Katika picha hapo juu ni Mkaguzi Mkuu wa Shirika Bwana Paul Kiwera akiwa anabadilishana mawazo na Mwanasheria wa Shirika Bibi.Gloria Kalabamu muda mfupi kabla ya kikao cha Bodi.kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Shirika la Masoko ya Kariakoo.
Subscribe to:
Posts (Atom)