Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo Bwana Florens Seiya akipeana mkono na Bwana Beenedict Tesha Mkurugenzi wa Jamaa Technology ambaye ni Service Provider.Hapo walikuwa wakibadilishana mkataba wa utoaji huduma yaani Service Level Agreement (SLA) baada ya kusaini.Hafla hii ilifanyika Jumanne iliyopita katika Ofisi za Shirika la Masoko ya Kariakoo Jijini Dar Es Salaam.Aliyesimama kati yao ni Bi.Anna Rocha Mkurugenzi wa 2SEEDS Network hapa nchini Tanzania.
Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo Bwana Florens Seiya akizungumza na Waandishi wa habari Ofisini kwake mara baada ya uzinduzi wa tovuti ya Shirika la Masoko ya Kariakoo ambayo kwa sasa kwa kupitia tovuti hiyo watu mbalimbali wataweza kuona taarifa mbalimbali za bei za mazao yauzwayo katika Soko Kuu la Kariakoo kila siku na wakati wowote.
Katika picha hapo juu ni Mkuu wa Kitengo cha Tehama(ICT) katika Shirika la Masoko ya Kariakoo Bwana Anderson Shaka akiwa anatoa maelekezo mafupi ya namna gani ya kutumia Simu za mkononi ili kupata bei za mazao mbalimbali yanayouzwa katika Soko Kuu la Kariakoo.lakini pia bei hizo kwa baadhi ya mazao makuu ya chakula bei zake zipo katika Website ya Shirika hili.Waandishi wa habari kutoka katika Vyombo mbalimbali vya habari walihudhuria uzinduzi huo Jumanne wiki iliyopita.
Mkurungenzi wa 2SEEDS Network Tanzania Bi.Anna Rocha akitoa maelezo ya namna gani Mtandao wao unavyofanya kazi hapa nchini tangu mwaka 2011.Pamoja na mambo mengine pia lakini pia 2SEEDS Network ni Washirika wakubwa na Shirika la Masoko ya Kariakoo katika kuwatafutia masoko ya bidhaa/ mazao ya Wakulima kutoka vijijini hasa katika Wilaya ya Korogwe ambako wanawawezesha Wakulima katika kuibua miradi ya uzalishaji mali na kuwaasimamia kwa karibu ili kufikia malengo ya kimaendeleo na maisha bora.
Bwana Christian Mlayi ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Habari Mazao Founders akiwa Ofisini kwa Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo akizungumza na Waandishi wa habari Jumanne iliypita mara baada ya uzinduzi wa Mtandao wa kutoa taarifa za bei za mazao kutoka Soko Kuu la kariakoo. Habari Mazao founders wameshirka wa mradi wa Masoko kwa kutengeneza Mfumo ambata ambao hufanya kazi sambamba na Mfumo mkuu wa bei wa Shirika la Masoko(KMC Database Management System).
No comments:
Post a Comment