Meneja Mkuu akipata maelezo kutoka kwa Muhandisi wa Shirika Bwana Flavian Mlellwa wakati wa ziara ya kuzungukia maeneo ya Soko kuu la Kariakoo mapema leo asubuhi.Meneja Mkuu Bwana Florens Seiya aliambatana na Wakuu wa Idara na Vitengo ambao wote kwa pamoja huunda Menejimenti ya Shirika. Kutoka Kushoto aliyeshika Radio Call ni Mkuu wa Kitengo cha Usalama Bwana Mzava,anayefuata ndiye Meneja Mkuu,anayetoa maelezo ni Mkuu wa Kitengo cha Matunzo(Muhandisi),na wengine ni Meneja wa Fedha Mrs. Marieta Masauwa na Bi.Dainess Sooi anayekaimu nafasi Meneja Mipango na Biashara .
Mfanyabiashara wa Mbogamboga katika eneo la Soko dogo akiongea na Meneja Mkuu wa Shirika kama alivyokutwa na leo asubuhi katika eneo lake la biashara.
Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko Bwana pamoja Menejimenti yake wakiwa wanapokea maelezo kutoka Mfanyabiashara akielezea jinsi ambavyo huwa wanapanga bidhaa zao katika eneo hilo. Hapo katika eneo la Soko dogo.
katika picha hapo juu ni Kisima cha Maji ambacho kinamilikiwa na SMK kipo katika eneo la Soko Dogo. Wiki iliyopita kilikuwa kimeharibiwa kwa kuvunjwa Pampu yake wakati wa bomoabomoa.Ndugu msomaji kama unavyoona katika picha kisima hicho kimefanyiwa ukarabati na Kitengo cha Uhandisi cha Shirika la Masoko na hatimaye kuanza kutoa huduma ya maji tena.
Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko aliyetangulia mbele akiwa anarejea Ofisini kwake leo asubuhi mara baada ya kuzungukia maeneo mbalimbali ya Soko Kuu la huku akiwa ameambatana na Menejimenti yake.
Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo Bwana Florens Seiya akifanya majumuisho ya ziara alioifanya ya kuangalia na kuzungumza na baadhi ya Wafanyabiashara ambao hufanya biashara zao katika maeneo kadhaa ambayo yalikumbwa na bomoabomoa ya Manispaa wiki iliyopita. Majumuisho hayo aliyafanyia Ofisini kwake leo asubuhi baada ya ziara aliyokuwa ameambatana na Wajumbe wa Menejimenti ya Shirika.
No comments:
Post a Comment