Kizazaa cha Mashine za TRA kimepelekea Maduka mengi pamoja na Ofisi kadhaa zinazoendesha shughuli zake za biashara katika mitaa ya hapa Kariakoo kufungwa kabisa na kutofanya shughuli zake za kila siku za uzalishaji mali kwa takribani siku mbili sasa tangu jana!
Kariakoo kama inavyofahamika kuwa ni sehemu yenye pilikapilika nyingi za biashara katika Jiji la Dar Es Salaam; lakini hali haikuwa hivo jana Jumatatu na hata leo hii!
Kama hiyo haitoshi hata msongamano wa magari umepungua sanaaa kwani shughuli nyingi zimesimama!
Baadhi ya Wafanyabiashara walionekana wakiwa wamekaa nje ya maduka yao na wengine kupitapita tuu katika mitaa mbalimbali!
Lakini pia hali hii imeleta usumbufu kwa Wafanyabiashara wa kutoka nchi jirani za Congo DRC,Zambia,Malawi,Uganda,Rwanda,Burundi,Kenya na hata Visiwa vya Commoro ambao wamekuja Jijini DSM kwa ajili ya kununua bidhaa mbalimbali ili kupeleka kwao wamekwama! kwakuwa maduka mengi yamefungwa! Huenda hali hii inaweza kuwaharibia bajeti zao!
No comments:
Post a Comment