Thursday, March 19, 2015
Maarifa huongezwa kila siku
Katika picha hapo juu ni Meneja wa fedha Bi.Marieta Massaua na Bwana Peter Mshikilwa ambaye ni Mwanasheria, wote ni watumishi katika Shirika la Masoko Kariakoo. Hapo walikuwa wakihudhuria semina inayohusu Sheria ya manunuzi.Semina hiyo ililenga kuwajengea uwezo watumishi hawa jinsi yakutekeleza sheria hiyo muhim katika shughuli za manunuzi.
Kariakoo
Watumishi wa Kitengo cha Manunuzi Bwana Mathias Mbafu na Henrika Kawili wakijadili jambo kuhusiana na kazi zao za kila siku.Bwana Mathias Mbafu ni Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi.
Ndizi!Ndizi! sokoni Kariakoo
Friday, March 13, 2015
Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko Bwana Florens Seiya akiwa anaongoza Mkutano baina ya Menejimenti ya Shirika na Wajumbe wa kamati kuu ya Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kariakoo, walipokuwa wakijadili kuhusu wazo la kufanya maboresho eneo la maduka ya nyama(mabucha) ndani ya jengo kuu la Soko la Kariakoo Jijini Dar Es Salaam.
Thursday, March 12, 2015
Ushirikishwaji wa Wadau katika maendeleo ni muhimu
Katika picha hizo hapo juu ni Wajumbe wa Kamati Kuu ya Uongozi wa Wafanyabiashara katika Soko Kuu la Kariakoo lililopo Jijini Dar Es Salaam,wakiwa katika Mkutano wa pamoja na Uongozi wa Shirika la Masoko Kariakoo. Mkutano huo ulikuwa na agenda kuu moja tuu ya kuwashirikisha Wafanyabiashara hao katika wazo la kuboresha matumizi ya sehemu ya maduka ya nyama(Mabucha) iliyomo ndani ya jengo la Soko Kuu la Kariakoo, kwa nia ya kuliongezea tija shirika. Kwenye picha ya chini aliyevaa miwani ni Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko Kariakoo Bwana Florens Seiya akifafanua jambo kwa Wajumbe waliohudhuria mkutano huo juzi, mkutano huu ulifanyika ndani Ukumbi wa Mikutano wa Shirika.
Monday, March 9, 2015
Sokoni Kariakoo leo
Thursday, February 26, 2015
Sokoni Kariakoooo leoo!
Huyu kijana alijitaja jina lake kuwa ni Abdul Abubakari baada yakupata kibano pale alipokamatwa akiwa katika harakati za kuiba vioo vya kwenye magari ambayo yameegeshwa katika eneo la Soko Kuu la Kariakoo.Kijana huyu alinaswa na vijana ambao walikuwa wanaosha magari mapema leo asubuhi
Katika picha hapo juu ni baadhi ya vifaa vya magari ambavyo kijana huyu alipatikana navyo kijana Abdul Abubakari.
Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi katika Shirika la Masoko Kariakoo, Bwana Mathias Mbafu akiwa Ofisini kwake akimuelekeza jambo Msaidizi wake Bi.Henrika Kawili.

Monday, February 23, 2015
Aina mbalimbali za Mazao/Vyakula katika Soko Kuu
Maboga nayo pia hupatikana hapa katika Soko Kuu la Kariakoo katika bei tofautitofauti,maboga ni miongoni mwa vyakula ambavyo hupendwa na watu wa kada tofauti.
Viazi mviringo kutoka mikoa ya Nyanda za juu Kusini kama vile Njombe,Mbeya na Iringa, huingia Sokoni Kariakoo kila siku.
Vitunguu safiii kabisa kutoka mikoani Singida,Mbeya,Iringa na kwingineko huingia katika Soko Kuu la Kariakoo.
Thursday, February 19, 2015
Miongoni mwa Watumishi wa Shirika la Masoko
Kama ilivyo kawaida katika Taasisi mbalimbali za Serikali kuwa na Watumishi wa kada tofautitofauti, katika picha hapo juu ni Bwana Rogers Kuyonga kutoka Kitengo cha Matunzo na Roman Winfred kutoka Kitengo cha Usalama,wote ni waajiriwa katika Shirika la Masoko Kariakoo.
Katika picha hapo juu kutoka kushoto ni Bwana Charles Sombe mwenye suruali nyeupe kutoka Idara ya Utumishi,Ncheye Kulwa aliyeshika Notebook yeye yuko katika Kitengo cha ndani cha Ukaguzi na Bi.Jackline kutoka katika Idara ya Fedha
Tuesday, February 17, 2015
Bidhaa na Wafanyabiashara Sokoni Kariakoo-Jijini Dar Es Salaam.
Limau ni moja ya viungo vnavyotumiwa sana na wapishi mbalmbali,Sokoni Kariakoo kuna kila aina ya bidhaa muhim unazozihitaji. Limau hizi huuzwa kwa bei ya rejareja na jumla. Eneo la shimoni ndiko hasa bidhaa hizi zinapatikana kwa wingi sana.
Ndimu nazo hazijapungua hapa Sokoni Kariakoo,zinapatikana kwa wingi katika bei tofautitofauti kwa jumla na rejareja.Ndimu daraja la kwanza kabisa, fika Sokoni Kariakoo eneo la Shimoni.
Mfanyabiashara huyu anayejulikana kwa jina la Munguatosha pichani hapo juu, yupo eneo la Shimoni yeye ni maalum tuu kwa uuzaji wa Karoti na pilipili hoho.Pia hupokea mazao kutoka kwa Wakulima mbalimbali kutoka mkoani,kama vile kutoka Wilayani Korogwe na Lushoto mkoani Tanga.
Bwana Dominik Zakayo ni miongoni mwa wafanyabiashara wa vitunguu saum na tangawizi katika Soko Kuu la Kariakoo eneo la Shimoni.Karibu ujipatie bidhaa mbalimbali.
Monday, February 16, 2015
TUICO-Tawi laShirika la Masoko Kariakoo wapata Uongozi mpya
Katika picha hapo juu ni Viongozi waliosimamia zoezi la uchaguzi uliowezesha kupata viongozi wapya watakaliongoza Tawi hili katika kipindi cha miaka mitano ijayo kuanzia mwaka huu. Kutoka kushoto ni Bwana Ibrahim Masha ambaye ni Mjumbe wa TUICO Taifa ambaye pia ni mtumishi katika Shirika la Masoko, Bwana Godwin Mrosso amabaye ni Meneja Utumishi na Uendeshaji katika Shirika la Masoko ambaye huyu alimuwakilisha Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo, wengine ni Bwana Willy Kibona ambaye ni Katibu wa TUICO mkoa wa Ilala na Bi.Maria John Bange yeye ni Mkuu Msaidizi wa Idara yaWanawake TUICO Mkoa wa Ilala.Hapo walikuwa wakimalizia kujumlisha kura.
Sehemu ya Wanachama wa TUICO Tawi ,wakiwa katika Ukumbi wa Mikutano wa Shirika la Masoko Kariakoo wakiwa katika hali ya kusubiria matokeo ya uchaguzi yatangazwe na Wasimamizi wa uchaguzi huo.Uchaguzi huo ulifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.
Baadhi ya Wanachama walioshiriki katika uchaguzi wakiwa wamesimama nje ya Ukumbi mara baada ya kumaliza kupiga kura za kuwachagua viongozi wa Tawi hilo kuanzia ngazi ya Mwenyekiti,katibu pamoja na Wajumbe wa Halmashauri ya Tawi.
Katika picha ni Bwana Willy Kibona ateteta jambo na Mjumbe wa TUICO Taifa Bwana Ibrahim Masha ambaye katika picha hayupo na kulia kwake ni Bi.Maria John Bange wote kwa pamoja walifika kusimamia shughuli nzima ya Uchaguzi huo.
Katika picha hapo juu ni Bwana Ibrahim Masha Mjumbe wa TUICO Taifa akiwa tayari kabisa kuanza kutangaza matokeo ya uchaguzi mara baada ya zoezi la kuhesabu kura.
Wanachama wakiwa wametulia kabisa wakisikiliza matokeo ya uchaguzi waliokuwa wameufanya .
Bwana Ibrahim Masha akitanganza matokeo ya uchaguzi mara baada ya kumalizika kwa zoezi la upigaji kura na kuhesabu.
Wanachama wakiwa wanaimba na kufurahia mara baada ya kumalizika kwa uchagauzi na matokeo kuwa yametangazwa rasmi. Katika uchaguzi huo Bwana Denis Mfuruki alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa TUICO Tawi wakati katika nafasi ya Katibu Bwana Henry Rweijuna aliibuka mshindi.
Katika picha hapo juu ni sehemu ya wanachama wakitoka ukumbini mara baada ya uchaguzi kumalizika, wakiwa wenye nyuso za furaha kwa kuwapata viongozi wapya watakao waongoza kwa kipindi cha miaka mitano.
Sehemu ya Wanachama wa TUICO Tawi ,wakiwa katika Ukumbi wa Mikutano wa Shirika la Masoko Kariakoo wakiwa katika hali ya kusubiria matokeo ya uchaguzi yatangazwe na Wasimamizi wa uchaguzi huo.Uchaguzi huo ulifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.
Baadhi ya Wanachama walioshiriki katika uchaguzi wakiwa wamesimama nje ya Ukumbi mara baada ya kumaliza kupiga kura za kuwachagua viongozi wa Tawi hilo kuanzia ngazi ya Mwenyekiti,katibu pamoja na Wajumbe wa Halmashauri ya Tawi.
Katika picha ni Bwana Willy Kibona ateteta jambo na Mjumbe wa TUICO Taifa Bwana Ibrahim Masha ambaye katika picha hayupo na kulia kwake ni Bi.Maria John Bange wote kwa pamoja walifika kusimamia shughuli nzima ya Uchaguzi huo.
Katika picha hapo juu ni Bwana Ibrahim Masha Mjumbe wa TUICO Taifa akiwa tayari kabisa kuanza kutangaza matokeo ya uchaguzi mara baada ya zoezi la kuhesabu kura.
Wanachama wakiwa wametulia kabisa wakisikiliza matokeo ya uchaguzi waliokuwa wameufanya .
Bwana Ibrahim Masha akitanganza matokeo ya uchaguzi mara baada ya kumalizika kwa zoezi la upigaji kura na kuhesabu.
Katika picha hapo juu ni dada ambaye alipendekezwa kufanya sala maalum kwa nia ya kumshirikisha Mungu katika shughuli nzima ya uchaguzi huo.
Pia katika picha hii hapo juu ni Mzee Idd Mrope nae pia alipendekezwa kufanya Dua maalum kwa ajili uchaguzi huo wakuwapata viongozi bora katika tawi la SMK.Wanachama wakiwa wanaimba na kufurahia mara baada ya kumalizika kwa uchagauzi na matokeo kuwa yametangazwa rasmi. Katika uchaguzi huo Bwana Denis Mfuruki alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa TUICO Tawi wakati katika nafasi ya Katibu Bwana Henry Rweijuna aliibuka mshindi.
Katika picha hapo juu ni sehemu ya wanachama wakitoka ukumbini mara baada ya uchaguzi kumalizika, wakiwa wenye nyuso za furaha kwa kuwapata viongozi wapya watakao waongoza kwa kipindi cha miaka mitano.
Subscribe to:
Posts (Atom)