Picha hiiya pamoja ambayo inaonyesha tukio la kumkaribisha Meneja Mkuu mpya wa Shirika la Masoko Kariakoo siku ya Ijumaa tarehe 30.9.2016 mchana. Hafla hii fupi ilifanyika katika Ofisi za Shirika hili zilizopo katika Jengo Kuu la Soko Kuu la Kariakoo.Aliyeketi katika kiti ni Meneja Mkuu mpya wa Shirika Bwana Hetson Kipsi, na waliosimama kutoka kushoto ni Bwana Mlelo Mgheni Meneja Biashara na Mipango wa Shirika, Bwana Denisi Mfuruki ni Mjumbe wa Bodi ya Shirika,Bwana Cprian Kuyava kutoka Hazina ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi, Bwana Dk. Buhohela Lunogelo ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika, Bwana Florens Seiya aliyekuwa Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko na sasa amemaliza muda wake wa Utumishi katika Shirika hili. Anayefuata ni Meneja Utumishi na Utawala wa Shirika Bwana Godwin Mroso, Bwana Mathias Mbafu Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi katika Shirika,Meneja wa Fedha Bi.Marieta Masaua ambaye ni Meneja wa Fedha katika Shirika,Bwana Donald Sokoni Meneja wa Afya na Usafi,Bwana Josam Mnzava Mkuu wa Kitengo cha Usalama,Bwana Paul Kiwera Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi cha Ndani,na Bwana Flavian Mlelwa Kaim Mkuu wa Kitengo cha Matunzo.
Wakati wa makabidhiano ya Ofisi Dua na Sala fupi zilifanyika ndani ya Ofisi ya Meneja Mkuu kama ishara ya kumuombea mafanikio Meneja Mkuu aliyekuwa akimaliza muda wake na kadhalika kama ishara yakumuombea Meneja Mkuu mpya wa Shirika kupata ufanisi kiutumishi na hekima ya Mungu imuongoze katika utekelezaji wa majukumu yake kama Mtumishi wa Umma mwenye kuwatumikia Watanzania.
Meneja Mkuu mpya Bwana hetson Kipsi akizungumza na Menejimenti ya Shirika pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Shirika la Masoko Kariakoo katika kikao kifupi cha kukabidhiwa Ofisi. Meneja Mkuu huyo mpya alisisitiza ufanisi na uwazi pamoja na kujituma katika Utumishi ndani ya Menejimenti. Mambo hayo ya msingi ndiyo hasa yatakayo lisaidia Shirika hilo kupiga hatua ya kimaendeleo. Lakini alionya tabia ya uzembe kwa Watendaji wa Shirika jambo ambalo alisema hatalivumilia hata kidogo katika uongozi wake katika Shirika hili kongwe lililoanzishwa Mwaka 1974 kwa mujibu wa Sheria ya Bunge Namba36, ya Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Meneja Mkuu Bwana Florens Seiya aliyemaliza muda wakeakitoa hotuba fupi ya kuelezea mwenendo mzima wa Shirika mbele ya Meneja Mkuu mpya Bwana Hetson Kipsi na Mwenyekiti wa Bodi pamoja na Wajumbe wa Menejimenti ya Shirika hilo muda mfupi kabla ya makabidhiano ya ya Ofisi, Ijumaa tarehe 30.9.2016 mchana. Hafla ilyofanyika katika Ofisi za Soko kuu la Kariakoo Jijini Dar Es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika Bwana Dk.Buhohela Lunogelo akipeana na mkono wa na Meneja Mkuu aliyemaliza muda wake wa Utumishi katika Taasisi hii. Anayetazama kwa karibu hapo ni Bwana Hetson Kipsi Meneja Mkuu mpya wa Shirika. Mwenyekiti wa Bodi huyo alimshukuru Meneja Mkuu aliyemaliza muda wake wa Utumishi na kumtakia heri katika muda wake wa utumishi uliobakia katika kuutumikia Umma. Kadhalika alimkaribisha Meneja Mkuu Mpya Ofisini.Bwana Kipsi alikuwa Mtumishi katika Wizara ya TAMISEMI ambayo ipo chini ya Ofisi ya Rais.Meneja huyu mpya ni Mtaalam wa Uchumi kwa taaluma yake.
Katika picha hapo juu ni moja ya Wajumbe wa Bodi ya Shirika la Masoko Kariakoo Bwana Denis Mfuruki mwenye karatasi mkononi akipeana mkono na Meneja Mkuu mpya wa Shirika hilo Bwana Hetson Kipsi kama ishara ya upendo kumkaribisha Mtendaji Mkuu huyo mpya katika Ofisi ya Meneja Mkuu. Aliyesimama kushoto ni Bwana Florens Seiya ambaye amemaliza muda wake wa kuhudumu katika Shirika hili, baada yakufanya kazi hapa katika kipindi cha miaka saba.Mabadiliko haya ya Uongozi yamekuja baada ya Uteuzi mpya alioufanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dk.John Magufuli mapema mwanzoni mwa mwezi Septemba mwaka huu.
Hapa katika picha ni Meneja Mkuu Bwana Florens Seiya akipeana mkono na Meneja Mkuu mpya wa Shirika la Masoko Kariakoo Bwana Hetson Kipsi. Mameneja hawa walipeana mikono Ofisini katika Ofisi ya Meneja Mkuu wakishuhudiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Masoko, Makamu Mwenyekiti wa Bodi pamoja na Menejimenti ya Shirika hili,siku ya Ijumaa tarehe 30.9.2016 mchana.
Sunday, October 2, 2016
Tuesday, July 12, 2016
Karibuni Wafanyabiashara kwa Matangazo
Shirika la Masoko ya Kariakoo, sasa linakaribisha Wafanyabiashara wa aina zote kwa Matangazo ya Biashara zao. Kwa wale wafanyabiashara wa ndani ya Shirika wanahamasishwa zaidi kutangaza biashara zao!
Lakini pia Makampuni tofauti yanakaribishwa pia kutangaza na sisi katika Blog yetu hii! Kwa mawasiliano zaidi ili kupata nafasi piga namba za simu zilizopo katika Blog.
Ahsanteni sana na Karibuni
Thursday, February 4, 2016
Mazao yanayopatikana Soko Kuu la Kariakoo
Miongoni mwa mazao muhimu ambayo huuzwa katika Soko Kuu la Kariakoo ni pamoja na Nazi.Nazi ambazo huuzwa katika soko hili maarufu zinatoka sehemu mbalimbali hapa nchini.Mikoa ifuatayo Tanga,Morogoro na Pwani ni sehemu ambako nazi huzalishwa kwa wingi.Nazi hizi huuzwa kwa bei ya jumla na rejareja.
Tuesday, November 24, 2015
Mboga aina zote Kariakoo Sokoni
Katika picha hapo juu ni mfanyabiashara wa mazao ya mbogamboga akiwa na mteja katika meza yake.Katika soko hili kila aina ya mbogamboga hupatikana takribani mwaka mzima!
SOKONI KARIAKOO
Eneo la shimoni katika Soko Kuu la Kariakoo ambako bidhaa mbalimbali huuzwa kwa bei ya jumla na rejareja, eneo hili kwa sasa limekuwa bora zaidi kimpangilio kwa wafanyabiashara na kufanyiwa marekebisho ya taa za umeme ambazo zimeongeza mwanga wa kutosha.
Nafaka za aina mbalimbali zinapatikana katika Soko Kuu la Kariakoo,ukifika sokoni utazipata nafaka hizi katika eneo la Soko dogo lililopo pembezoni mwa Jengo la Soko Kuu.Katika picha akina mama hawa wakiwa Sokoni Kariakoo wakiandaa maharage mabichi kwa kuyamenya maganda ili waweze kuwauzia wateja wao. Katika eneo hili kwa sasa limeboreshwa kwani sio tena wanakaa chini badala yake wanatumia meza nzuri na bora kwa kuhifadhia bidhaa zao wakati wa kuuza. Karibu sokoni Kariakoo.
Thursday, October 22, 2015
Mazao katika Soko Kuu la Kariakoo - Dar Es Salaam
Zabibu ni miongoni mwa bidhaa zinazopatikana hapa Soko Kuu la Kariakoo, Jijini Dar Es Salaam. Bidhaa hii huzalishwa kwa wingi mkoani Dodoma
vitunguu saumu na tangawizi pia huuzwa katika soko kuu la Kariakoo.
Pilipili Hoho hupatikana katika Soko kuu la Kariakoo takribani mwaka mzima. Pilipili hoho huingizwa katika soko hili zikitokea katika mikoa mbalimbali ikiwemo Morogoro,Pwani na Tanga.Kwa bei ya jumla na rejareja huuzwa sokoni hapa kuanzia mapema alfajiri hadi jioni.
Monday, August 24, 2015
Matukio katika Picha
Katika picha hapo juu kutoka kulia ni Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko Kariakoo Bwana Florens Seiya, Mwenyekiti wa TUICO tawi Bwana Dennis Mfuruki aliyesimama na Bwana Henry Rwejuna ambaye ni Katibu wa TUICO tawi, kwa pamoja wakiwa wanaendesha mkutano wa wafanyakazi wa Shirika la Masoko ya Kariakoo mwishoni mwa wiki iliyopita. Ni moja ya mikutano ya kawaida ambayo imekuwa inafanyika kwa nia ya kujenga na kuimarisha mahusiano baina wafanyakazi wa shirika na Mwajiri wao, wakilenga zaidi hali ya mwenendo mzima wa Shirika.
katika picha hapo juu ni vitunguu maji ambavyo ni moja ya bidhaa zinazouzwa hapa katika soko Kuu la Kariakoo jijini Dar Es Salaam.Vitunguu maji hivi hufikishwa sokoni Kariakoo vikiwa vinatoka mikoa mbalimbali ya Tanzania kama vile Mbeya,Arusha,Iringa na Singida.
Picha hiyo hapo juu inaonyesha sehemu tuu ya Watumishi wa Shirika la Masoko ya Kariakoo wakiwa wametulia huku wakifuatilia maelezo ya Meneja Mkuu wa Shirika ,pichani hapo juu hayupo wakati wa mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Shirika mwishoni mwa wiki iliyopita.
Thursday, August 20, 2015
SHIRIKA LA MASOKO YA KARIAKOO
TANGAZO LA KAZI
Shirika
la Masoko ya Karikaoo ni Shirika la Umma lililoanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya
Bunge Na.32 ya mwaka 1974 na kupewa majukumu ya kusimamia na kuendesha Soko Kuu
la Kariakoo pamoja na Masoko mengine yatakayokuwa chini ya usimamizi wa Shirika
pia kujenga Masoko mengine mapya katika Jiji la Dar es Salaam na kusimamia
uendeshaji wake. Shirika linakaribisha maombi ya nafasi mbili za kazi zifuatazo:
- Mwanasheria Daraja la 11
Muombaji
awe na Shahada ya Sheria kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na Serikali. Awe
amepitia Shule ya Sheria na kusajiliwa kama Wakili.
Kazi
na Majukumu.
Kushauri
masuala ya kisheria katika Shirika la Masoko ya Kariakoo.
Kuandaa
nyaraka zote za kisheria kwa ajili ya kusaidia kufikia malengo ya Shirika.
Kufuatilia
na kutunza kumbukumbu muhimu kwa ajili ya kutumika kwenye mashauri Mahakamani.
Kuandaa
mihutasari ya mashauri mbalimbali ya shirika yaliyopo mahakamani.
Kuandaa
na kupeleka notisi za kisheria kwa wadaiwa wa shirika .
Kufanya
shughuli yeyote atakayo pangiwa na Meneja Mkuu au Mkuu wa kitengo.
- Ofisa Ugavi Msaidizi
Muombaji
awe na Stashahada ya katika fani ya ununuzi na ugavi, awe amesajiliwa na PSPTB
Kazi na Majukumu.
Kuhakikisha
kuwa vifaa vinavyonunuliwa vinapokelewa na kuingizwa katika vitabu vya
Shirika..
Kuhakikisha
kuwa nyaraka zote za stoo zinajazwa kwa ufasaha na kwa wakati.
Kuhakikisha
kuwa mali zote zilizoifadhiwa stoo zinatuzwa
bila upotevu wowote.
Kuhakikisha
kuwa uingizaji na utoaji wa bidhaa unafuata sheria na kanuni za manunuzi ya
umma.
Kuhakikisha
kuwa vifaa na mali zinazohifadhiwa stoo zinatunzwa katika mpangilio mzuri
Kufanya kazi zozote
atakazopangiwa na Mkuu wa Kitengo.
MASHARTI
YA JUMLA
Waombaji
wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
Waombaji wote waambatishe nakala ya cheti cha
kuzaliwa. Na picha (passport size) moja ya rangi
Waombaji
waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye
anwani na namba za simu pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu
wa kuaminika.
Maombi yote yaambatane na nakala za
vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho
na nakala ya vyeti vya kuhitimu mafunzo
mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
Mwisho wa Kupokea maombi ni 29/08/2015.
Maombi hayo yatumwe kwa :
Meneja Mkuu,
Shirika la Masoko ya Kariakoo,
P.O.BOX 15789,
Dar es Salaam.
Na kwa Email: info@kariaakoo.or.tz.
Thursday, August 13, 2015
TANGAZO MAALUM
SHIRIKA LA
MASOKO KARIAKOO
(KARIAKOO MARKETS CORPORATION)
AP/109/KMC/2015/2016/C
Expression of Interest
For
PROVISION
OF CONSULTANCY SERVICES
Date: 10th
August 2015
1. The Kariakoo
Markets Corporation has set aside funds towards the cost of providing
consultancy services as described below and
it intends to apply part of the proceeds of this fund to cover eligible
payments under the contract.
|
S/N
|
TENDER DESCRIPTION
|
LOT/TENDER NUMBER
|
|
01
|
Preparation of Strategic plan (2015 – 2018)
|
PA/109/2015/2016/STP/C/01
|
|
02
|
Valuation of Assets
|
PA/109/2015/2016/VA/C/01
|
2. The Kariakoo
Markets Corporation
now invites eligible registered Local
Consultancy firms to indicate their interests in providing the services
mentioned above.
3. Interested individual consultants must provide information
indicating that they are qualified to perform the services by submitting
consultant’s profile, description of similar assignments, experience in similar
conditions, availability of appropriate skills among staff, etc.
4. A consultant will be selected in accordance with the procedures
set out in the Public
Procurement Act 2011 and the Public Procurement Regulations – Government Notice
No. 466 of 2013.
5. Interested
eligible consultants may obtain further information
from the office of the Tender Board
Secretary, Kariakoo Markets Corporation,
P.o.Box 15789, Dar es Salaam from
08:30am to 03:30 pm on Monday to Friday inclusive except on public
holidays.
6. Expressions of Interest (EoI) must be delivered to the
address below not more than 25thAugust
2015 at or before 10:00hrs.
The Secretary,
Kariakoo
Markets Corporation Tender Board,
P.o.Box 15789,
Dar es Salaam.
7. Closing date
for receiving the expression of interest is 25thAugust 2015 at
10:00. Late Expressions of Interest shall not be
accepted for evaluation irrespective of the circumstances.
General
Manager
Kariakoo
Market Corporation
WANAMTANDAO WA LUTINDI-KOROGWE
Miongoni mwa miradi ambayo imepata mafanikio makubwa inayosimamiwa na 2SEEDS Network wilayani Korogwe Vijijini ni ule uliopo katika kijiji cha Lutindi. Mradi huu unastawisha mazao ya mbogamboga kama vile inavyoonekana katika picha hapo juu shamba la moga aina ya kabichi linavyoendelea kutunzwa na wanakikundi.Mbali na mboga aina ya kabichi pia wanazalisha pilipili hoho,bitroots,bilinganya na nyanya chungu.
Subscribe to:
Posts (Atom)











