Sunday, December 14, 2014

Bidhaa za vyakula sokoni Kariakoo

 Karoti nzuri daraja la kwanza kabisa kutoka Mikoa mbalimbali ya Tanzania.Karibu ujipatie bidhaa hii bora kwa matumizi mbalimbali kama vile kutengeneza juice na nakadhalika.
Katika picha hapo juu ni Viazi mviringo vikiwa bado fresh kabisa kutoka mkoani. Mikoa mashuhuri kwa uzalishaji vyazi hapa nchini ni pamoja na Iringa,Njombe na Mbeya

Tuesday, December 9, 2014

Kuelekea Sikukuu za Christmas na Mwaka mpya!

 Njegere ni moja ya bidhaa adimu na yenye kupendwa sana na watu wengi kwa matumizi ya chakula. Njegere huingia katika Soko Kuu la Kariakoo kutoka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania kama vile Morogoro,Iringa,Njombe na kwingineko. Bidhaa hii kuelekea sikukuu za Christmas na Mwaka mpya bado inapatikana kwa wingi hapa Sokoni  hasa eneo la Shimoni.katika picha hapo juu Mfanyabiashara alikutwa na mpiga picha akiwa amekwisha kuzimenya njegere zake tayari kwa kuwauzia wateja mbalimbali.

Sokoni Kariakoo kuna kila aina ya vyakula.Katika picha hapo juu nafaka mbalimbali ambazo huuzwa katika soko Dogo.Mfanya biashara huyu ameweka wazi hata bei za vyakula kwa kuzingatia madaraja au ubora wake.Tunapoelekea katika Sikukuu za mwisho wa mwaka bei za vyakula hazijabadilika sana! Karibuni Sokoni kwa manunuzi ya bidhaa mbalimbali.

Thursday, December 4, 2014

Watumishi KMC

 Katika picha hapo juu ni Meneja Utumishi na Uendeshaji  Bwana Godwin Mrosso akiwa pamoja na  Mkuu  wa Kitengo cha Usalama Bwana Josam Mnzava.  Wote ni Watumishi wa Shirika la Masoko ya Kariakoo.
Katika picha hapo juu ni Mkaguzi Mkuu wa Shirika Bwana Paul Kiwera  akiwa anabadilishana mawazo na Mwanasheria wa Shirika Bibi.Gloria Kalabamu muda mfupi kabla ya kikao cha Bodi.kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa mikutano wa  Shirika la Masoko ya Kariakoo.

Tuesday, October 28, 2014

Mkutano wa Bodi ya Ushauri ya Shirika la Masoko Kariakoo

 Katika picha hapo juu ni Wajumbe wa Mkutano wa Bodi ya Ushauri ya Shirika la Masoko ya Kariakoo wakiwa wanatoka kwenda kupanda basi maalumu lililokuwa  limekodiwa kwa ajili ya kwenda kutembelea na kukagua mali za Shirika. Aliyetangulia mbele ni Meneja Mkuu wa Shirika Bwana Florens Seiya na anayefuata ni Mwenyekiti wa Bodi Bwana Wilson Kabwe.Hii ilikuwa ni mojawapo ya agenda za kikao hicho cha Bodi.
 Miongoni mwa Wajumbe waliohudhuria Mkutano wa  Bodi ya Ushauri wakipanda basi tayari kwa safari kuelekea maeneo ya Mbezi Beach ambako ziko nyumba za Shirika la Masoko ya Kariakoo, mwishoni mwa wiki iliyopita.
 Wajumbe wa Mkutano wa Bodi ya Ushauri wakiwa wamefika mahali zilipo nyumba za Shirika la Masoko ya Kariakoo.Katika picha Mwenyekiti wa Bodi hiyo Bwana Wilson Kabwe akiwasalimia Wajumbe wa Mkutano huo.
 Wajumbe wa mkutano wa Bodi wakitembea kuelekea katika geti la nyumba mojawapo eneo la Mbezi Beach Makonde, huku wakiongozwa mbele na Afisa Usalama Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo Bwana Josam Mnzava ambaye ameshikilia radio Call.
 Wajumbe wa Mkutano wa Bodi ya Ushauri ya Shirika wakiwa nje ya geti la nyumba mojawapo ya Shirika la Masoko Kariakoo,nyumba hizi zipo eneo la Mbezi Beach Mtaa wa Makonde.Anaye toa maelezo hapo ni Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo Bwana Florens Seiya.Hii ilikuwa ni mwishoni mwa wiki liyopita.
 Wajumbe wa Bodi ya ushauri walipata nafasi ya kutembelea na kukagua mali zinazomilikiwa na Shirika la Masoko ya Kariakoo.Hapo juu katika picha ni wajumbe hao walipokuwa eneo la Tabata bima Jijini Dar Es Salaam, ambako walifika kuona nyumba za Shirika hilo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Shirika la Masoko ya Kariakoo Bwana Wilson Kabwe ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Jiji la Dar Es Salaam.Katika picha alikuwa akifungua Mkutano wa Bodi  mwishoni mwa wiki iliyopita.Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Shirika la Masoko ya Kariakoo.

Monday, October 20, 2014

Wafanyabiashara wa Soko Kuu la kariakoo

Katika picha hapo juu ni miongoni mwa Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kariakoo wakiwa katika moja ya Masoko ya nje ambayo hufanyika Osterbay na Masaki jijini Dar Es Salaam siku za Jumamosi na Jumapili.Lakini pia katika Masoko haya huwashirikisha wakulima kutoka Wilaya ya Korogwe ambao husimamiwa miradi yao ya uzalishaji mali na matandao wa 2SEEDS Network.

Monday, October 13, 2014

Miongoni mwa Tunu za Hayati Baba wa Taifa Mwl.Julius K.Nyerere ambazo zingali zinaishi hadi leo!

 Ni miaka 15 tangu Baba wa Taifa alipotutoka Watanzania na Ulimwengu kwa ujumla,lakini angali anaishi pamoja na Watanzania wa aina zote.Shirika la Masoko Kariakoo ni mojawapo ya Mashirika yaliyoanzishwa wakati wa uongozi wake mnamo mwaka 1974 kwa sheria ya Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.Soko Kuu la Kariakoo lilianzishwa maalum kwa ajili ya  Watanzania hasa wakulima na Wafanyabiashara wadogowadogo waendeshe shughuli zao hapa ili kuwakomboa kimaendeleo.Mwalimu alimjali kila mwananchi kwa nafasi yake.

 Katika picha hapo juu ni Soko Kuu la Kariakoo katika mwaka wa 1975 mara baada ya kufunguliwa rasmi na Baba wa Taifa Hayati Mwl.Julius K. Nyerere.Wakati huu Soko Kuu la kariakoo lilikuwa na Wafanyabiashara kati ya 200 hadi 300, ambao walikuwa wakifanya biashara zao hapa.

 Hii ilikuwa ni tarehe 8/12/1975 Hayati  Mwalimu Julius K.Nyerere wakati huo akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaonekana akikata utepe kama ishara ya kufungua rasmi Jengo la Soko Kuu la Kariakoo.Ujenzi wake uligharimu kiasi cha Shilingi 22,000,000/=fedha za Kitanzania na pia lilijengwa na Wakandarasi wazawa tangu uchoraji na usanifu wa ramani kazi ambayo ilifanywa na Mhandisi Mzee wetu Beda Amuli nakujengwa na Kampuni ya MECCO kwa wakati. Jengo hili kwa sasa linakadiriwa kuwa na thamani ya Sh.Bilioni 50.

Picha hii hapo juu inaonyesha watumiaji wa Soko Kuu la Kariakoo wakiwa wameongeza sana, hii ni miaka ya hivi karibuni. Wananchi wengi wakiwa wamejaa kupata mahitaji mbalimbali.

Tutakukumbuka daima kwani umetuachia Tunu za kila aina katika Taifa hili.

Friday, September 26, 2014

Mama Majasiriamali


Mama huyu katika picha hufanya biashara ya dagaa katika Soko Kuu la Kariakoo. Mezani kwake kuna kila aina ya dagaa ambao huwauza.Mama huyu yupo eneo la Wauza dagaa na samaki katika eneo la Shimoni.Katika alikutwa akiwapimia wateja wake dagaa!

Sokoni Kariakoo leo!

 Hawa ni samaki aina ya Sangara kutoka Ziwa Victoria. Samaki hao wameshakaangwa safi tayari kabisa kwa matumizi ya mboga! Ukiwa katika Soko la Kariakoo ingia eneo Shimoni kwenye eneo la biashara ya samaki utawapata.Karibuniii!
Pichani hapo juu ni aina mojawapo ya mboga za majani zinazopatikana katika soko Kuu la Kariakoo; mboga hiyo huuzwa kwa kilo kati ya Sh.1000/= hadi 1500/=. Fika eneo la Shimoni utazipata mboga hizi na nyinginezo pia!

Sunday, September 21, 2014

Ndizi kutoka Morogoro

Ndizi aina hii kwa wakati huu zinatoka Mkoani Morogoro hasa katika wilaya ya Kilombero katika kijiji maarufu kiitwacho Mbingu. Kijiji hiki kinapitiwa na barabara inayounganisha mji wa Ifakara na Mlimba.Ndizi Mzuzu huzalishwa kwa wingi sana katika kijiji hiki.

Tuesday, September 16, 2014

Kariakoo leo

 Katika picha hapo juu ni Wajasiriamali ambao hufanya shughuli zao za kutengeneza mifuk/vifungashio vya bidhaa ndogondogo kama vile viungo vya vyakula,karanga, bisi nakadhalika katika ukubwa wa aina tofautitofauti.Wajasiriamali hawa wapo katika moja vyumba vya Soko Dogo la Kariakoo Jijini Dar Es Salaam.Kwa mahitaji yako ya vifungashio hivi Sokoni Kariakoo katika Jengo la Soko Dogo
 Katika picha hapo juu ni moja ya Wateja waliofika katika sehemu hii ya Wajasiriamali wanaotengeneza vifungashio vya mifuko ya nailoni ili kununua.Vifungashio hivi hutengenezwa kwa kutmia mashine ndogondogo ambazo huendeshwa kwa mkono na zingine hutumia nishati ndogo ya umeme.
Sokoni Kariakoo kuna mpangilio mzuri wa kila jambo;katika picha hapo juu ni magari ya Wateja mbalimbali ambao wamefika kujipatia mahitaji katika Soko Kuu la Kariakoo.Magari haya yapo katika hali ya usalama bila shaka yoyote! hapo ni Mtaa wa Tandamti.