Katika picha hapo juu ni Wajumbe wa Mkutano wa Bodi ya Ushauri ya Shirika la Masoko ya Kariakoo wakiwa wanatoka kwenda kupanda basi maalumu lililokuwa limekodiwa kwa ajili ya kwenda kutembelea na kukagua mali za Shirika. Aliyetangulia mbele ni Meneja Mkuu wa Shirika Bwana Florens Seiya na anayefuata ni Mwenyekiti wa Bodi Bwana Wilson Kabwe.Hii ilikuwa ni mojawapo ya agenda za kikao hicho cha Bodi.
Miongoni mwa Wajumbe waliohudhuria Mkutano wa Bodi ya Ushauri wakipanda basi tayari kwa safari kuelekea maeneo ya Mbezi Beach ambako ziko nyumba za Shirika la Masoko ya Kariakoo, mwishoni mwa wiki iliyopita.
Wajumbe wa Mkutano wa Bodi ya Ushauri wakiwa wamefika mahali zilipo nyumba za Shirika la Masoko ya Kariakoo.Katika picha Mwenyekiti wa Bodi hiyo Bwana Wilson Kabwe akiwasalimia Wajumbe wa Mkutano huo.
Wajumbe wa mkutano wa Bodi wakitembea kuelekea katika geti la nyumba mojawapo eneo la Mbezi Beach Makonde, huku wakiongozwa mbele na Afisa Usalama Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo Bwana Josam Mnzava ambaye ameshikilia radio Call.
Wajumbe wa Mkutano wa Bodi ya Ushauri ya Shirika wakiwa nje ya geti la nyumba mojawapo ya Shirika la Masoko Kariakoo,nyumba hizi zipo eneo la Mbezi Beach Mtaa wa Makonde.Anaye toa maelezo hapo ni Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo Bwana Florens Seiya.Hii ilikuwa ni mwishoni mwa wiki liyopita.
Wajumbe wa Bodi ya ushauri walipata nafasi ya kutembelea na kukagua mali zinazomilikiwa na Shirika la Masoko ya Kariakoo.Hapo juu katika picha ni wajumbe hao walipokuwa eneo la Tabata bima Jijini Dar Es Salaam, ambako walifika kuona nyumba za Shirika hilo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Shirika la Masoko ya Kariakoo Bwana Wilson Kabwe ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Jiji la Dar Es Salaam.Katika picha alikuwa akifungua Mkutano wa Bodi mwishoni mwa wiki iliyopita.Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Shirika la Masoko ya Kariakoo.
Tuesday, October 28, 2014
Monday, October 20, 2014
Wafanyabiashara wa Soko Kuu la kariakoo
Katika picha hapo juu ni miongoni mwa Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kariakoo wakiwa katika moja ya Masoko ya nje ambayo hufanyika Osterbay na Masaki jijini Dar Es Salaam siku za Jumamosi na Jumapili.Lakini pia katika Masoko haya huwashirikisha wakulima kutoka Wilaya ya Korogwe ambao husimamiwa miradi yao ya uzalishaji mali na matandao wa 2SEEDS Network.
Monday, October 13, 2014
Miongoni mwa Tunu za Hayati Baba wa Taifa Mwl.Julius K.Nyerere ambazo zingali zinaishi hadi leo!
Ni miaka 15 tangu Baba wa Taifa alipotutoka Watanzania na Ulimwengu kwa ujumla,lakini angali anaishi pamoja na Watanzania wa aina zote.Shirika la Masoko Kariakoo ni mojawapo ya Mashirika yaliyoanzishwa wakati wa uongozi wake mnamo mwaka 1974 kwa sheria ya Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.Soko Kuu la Kariakoo lilianzishwa maalum kwa ajili ya Watanzania hasa wakulima na Wafanyabiashara wadogowadogo waendeshe shughuli zao hapa ili kuwakomboa kimaendeleo.Mwalimu alimjali kila mwananchi kwa nafasi yake.
Katika picha hapo juu ni Soko Kuu la Kariakoo katika mwaka wa 1975 mara baada ya kufunguliwa rasmi na Baba wa Taifa Hayati Mwl.Julius K. Nyerere.Wakati huu Soko Kuu la kariakoo lilikuwa na Wafanyabiashara kati ya 200 hadi 300, ambao walikuwa wakifanya biashara zao hapa.
Hii ilikuwa ni tarehe 8/12/1975 Hayati Mwalimu Julius K.Nyerere wakati huo akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaonekana akikata utepe kama ishara ya kufungua rasmi Jengo la Soko Kuu la Kariakoo.Ujenzi wake uligharimu kiasi cha Shilingi 22,000,000/=fedha za Kitanzania na pia lilijengwa na Wakandarasi wazawa tangu uchoraji na usanifu wa ramani kazi ambayo ilifanywa na Mhandisi Mzee wetu Beda Amuli nakujengwa na Kampuni ya MECCO kwa wakati. Jengo hili kwa sasa linakadiriwa kuwa na thamani ya Sh.Bilioni 50.
Picha hii hapo juu inaonyesha watumiaji wa Soko Kuu la Kariakoo wakiwa wameongeza sana, hii ni miaka ya hivi karibuni. Wananchi wengi wakiwa wamejaa kupata mahitaji mbalimbali.
Tutakukumbuka daima kwani umetuachia Tunu za kila aina katika Taifa hili.
Friday, September 26, 2014
Mama Majasiriamali
Sokoni Kariakoo leo!
Hawa ni samaki aina ya Sangara kutoka Ziwa Victoria. Samaki hao wameshakaangwa safi tayari kabisa kwa matumizi ya mboga! Ukiwa katika Soko la Kariakoo ingia eneo Shimoni kwenye eneo la biashara ya samaki utawapata.Karibuniii!
Pichani hapo juu ni aina mojawapo ya mboga za majani zinazopatikana katika soko Kuu la Kariakoo; mboga hiyo huuzwa kwa kilo kati ya Sh.1000/= hadi 1500/=. Fika eneo la Shimoni utazipata mboga hizi na nyinginezo pia!

Sunday, September 21, 2014
Ndizi kutoka Morogoro
Tuesday, September 16, 2014
Kariakoo leo
Katika picha hapo juu ni Wajasiriamali ambao hufanya shughuli zao za kutengeneza mifuk/vifungashio vya bidhaa ndogondogo kama vile viungo vya vyakula,karanga, bisi nakadhalika katika ukubwa wa aina tofautitofauti.Wajasiriamali hawa wapo katika moja vyumba vya Soko Dogo la Kariakoo Jijini Dar Es Salaam.Kwa mahitaji yako ya vifungashio hivi Sokoni Kariakoo katika Jengo la Soko Dogo
Katika picha hapo juu ni moja ya Wateja waliofika katika sehemu hii ya Wajasiriamali wanaotengeneza vifungashio vya mifuko ya nailoni ili kununua.Vifungashio hivi hutengenezwa kwa kutmia mashine ndogondogo ambazo huendeshwa kwa mkono na zingine hutumia nishati ndogo ya umeme.
Sokoni Kariakoo kuna mpangilio mzuri wa kila jambo;katika picha hapo juu ni magari ya Wateja mbalimbali ambao wamefika kujipatia mahitaji katika Soko Kuu la Kariakoo.Magari haya yapo katika hali ya usalama bila shaka yoyote! hapo ni Mtaa wa Tandamti.

Monday, September 15, 2014
Kutoka Soko Kuu la Kariakoo - DSM
Kitu gani ambacho ukifika katika Soko Kuu la Kariakoo hutakipataaaa? La hasha kuanzia nafaka,matunda,mboga mboga za majani hadi viungo vya kila aina.Katika picha hapo juu utaona Vitunguu swaum,Tangawizi,Ndimu na vinginevyo vipo kwa wingi mezani vikiwa katika ubora sana.Karibu Soko kuu la Kariakoo ujipatie bidhaa za kila aina. Bei ya vitunguu swaum na tangawizi ni kati ya Sh.4000 hadi 4500 kwa kilo moja.
Miongoni mwa Watumishi wa Shirika la masoko ya Kariakoo ni Bwana Idd Mrope ambaye anaonekana katika picha hapo juu.Hapa yupo katika maeneo ya Ofisi za Shirika zilizopo katika ghorofa ya kwanza katika jengo la Soko Kuu.
Soko Kuu la Kariakoo ni Soko kubwa kuliko hapa nchini Tanzani,hii picha inaonesha sehemu mojawapo ya soko hili ambapo hapa barabara inayoingia katika eneo la soko la Jumla maarufu kama Shimoni.Eneo hili linaloonekana katika picha ni Geti Namba. 5 ambapo bidhaa karibu zote ambazo huingia hapa Sokoni hupitia hapa.

Friday, September 12, 2014
Matunda soko kuu kariakoo
Picha ya zabibu kama inavyoonekana hapo juu katika Soko la Kariakoo leo ilikuwa ikiuza kwa bei ya shillingi elfu mbili mia tano kwa kilogram na shillingi elfu thelathini kwa jumla
Katika picha hapo juu ni matunda aina ya ambazo kwa kiasi kikubwa huingizwa katika soko kuu la Kariakoo kila siku kutoka mikoani na hususani katika mkoa Morogoro zinauzwa kwa bei ya rejareja na jumla
Katika picha hapo juu ni matunda aina ya ambazo kwa kiasi kikubwa huingizwa katika soko kuu la Kariakoo kila siku kutoka mikoani na hususani katika mkoa Morogoro zinauzwa kwa bei ya rejareja na jumla
Saturday, September 6, 2014
Hafla ya kukabidhi vyeti kwa Wafanyakazi bora
Katika picha hapo juu ni Meneja Utumishi na Uendeshaji katika Shirika la Masoko ya Kariakoo Bwana Godwin Mrosso anayepiga makofi mara baada ya kumkabidhi cheti maalum cha ufanyakazi bora Bibi Romana Lukanga aliyeshika cheti,na aliyesimama katikati ni Bwana Joseph Mweyo ambaye ni Mwenyekiti wa TUICO katika Shirika la Masoko; na ambaye ameshika bahasha kulia kabisa ni Bibi Ester Chogero yeye ni Katibu wa TUICO hapa katika Shirika la Masoko.Meneja Utumishi alimuwakilisha Meneja Mkuu wa Shirika Bwana Florens Seiya ambaye alikuwa na shughuli zingine za kiofisi.Hafla hiyo ilifanyika jana mchana katika Ukumbi wa mikutano wa Shirika.
Katika picha hapo juu ni Bibi Primitiva Kamugisha Kaimu Meneja wa Idara ya Usafi akipokea cheti cha Ufanyakazi bora kwa niaba ya Mtumishi wa Idara yake ambaye hakuwepo katika hafla hiyo hapo jana.
Aliyesimama ni Bibi Romana Lukanga akitoa shukrani kwa Uongozi wa Shirika kwa niaba ya Wafanayakazi bora waliotunukiwa vyeti,pamoja na shukrani lakini pia aliwasisitiza wafanyakazi wenzake waliopata vyeti hivyo kuwa wasibweteke nakuona kuwa wameshashinda bali inawapasa kuongeza bidii katika utendaji wao wa kazi ili wazidi kuwa mfano mara kwa mara katika Shirika.
Katika picha hapo juu aliyesimama ni Meneja wa fedha katika Shirika la Masoko Mrs.Marieta Massaua akitoa pongezi kwa Watumishi wa Shirika walioshinda na kuwa Wafanyakazi bora katika Shirika.Hafla hiyo iliyofanyika jana mchana katika Ukumbi wa Mikutano wa Shirika.
Bwana Ibrahim Masha akiwa amesimama kutoa nasaha kwa Watumishi wa Shirika waliohudhuria hafla ya kukabidhi vyeti kwa Wafanyakazi bora wa Shirika kwa mwaka 2012/2013.Hafla hiyo ilifanyika jana mchana katika Ukumbi wa Mikutano wa Shirika. Bwana Ibrahim Masha yeye ni Mjumbe wa halmashauri ya TUICO ngazi ya Taifa.

Subscribe to:
Posts (Atom)