Tuesday, January 21, 2014

BCS - WAUZAJI WA MBEGU BORA ZA KILIMO CHA KISASA, WANAPATIKANA SOKONI KARIAKOO

Pichani hapo juu ni mifuko maalum ya kuhifahdia mbegu bora za nyanya, kama inavyoonekana hapo pichani. Mbegu hizi zimehifadhiwa katika mifuko yenye ujazo tofauti tofauti. Ipo ya Gram 10, Gram 25.  Mbegu hizi zinauzwa kwa bei ya Shilingi 5,000/= kwa mfuko.
Pichani hapo juu ni kopo maalum la kuhifadhia mbegu bora za bamia, kama inavyoonekana hapo pichani. Mbegu hizi zimehifadhiwa katika kopo yenye ujazo tofauti tofauti. Ipo ya Gram 10, Gram 25. Mbegu hizi zinauzwa kwa bei ya Shilingi 5,000/= kwa kopo

Huu ni mwonekano wa duka la BCS, Unaweza kuwasiliana nao kwa mawasiliano yafuatayo
+255 (0)754 272853
+255 (0) 787272 853
+255 (0) 715572 853



Monday, January 20, 2014

MATUKIO KATIKA PICHA

Pichani hapo juu ni watumishi wa Shirika la Masoko ya Kariakoo Jijini Dar es Salaam, aliyesimama ni Mkuu wa Idara ya Usafi wa Shirika (Primitiva Kamugisha) na aliyekaa kulia kwake ni Afisa biashara wa Shirika la Masoko Kariakoo (Bi. Soi) wakizungumza na mmoja wa wafanyabiashara wa sokoni Kariakoo (haonekani pichani) hivi karibuni katika ofisi ya Afisa biashara wa Shirika.

PATA BAMIA, NYANYA CHUNGU NA HOHO HAPA KARIAKOO SOKONI.

Friday, January 10, 2014

I.S & M (METALS) LIMITED

BUGGATI SPRAYER ZINAUZWA SHILINGI 25,000/=
 I.S & M Metals Limited ni wauzaji wa pembejeo za kilimo sokoni Kariakoo Jijini Dar es Salaam-Tanzania.
Pichani hapo juu ni kifaa kinachotumika kunyunyizia dawa katika bustani na maeneo mengine.


 I.S & M Metals Limited ni wauzaji wa pembejeo za kilimo sokoni Kariakoo Jijini Dar es Salaam-Tanzania.
Pichani hapo juu ni kifaa kinachotumika kunyunyizia dawa katika bustani na maeneo mengine.

Unaweza kuwapata I.S & M Metals Limited, Sokoni Kariakoo
Mawasilano yao ni: 0767 277473
                              0715 484444
                  Email: baly@intafrica.com




Wednesday, January 8, 2014

NAFAKA, MATUNDA NA MBOGA MBOGA ZINAZOPATIKANA SOKONI KARIAKOO



MAHARAGE-SOKONI KARIAKOO


HOHO
Hoho zinazopatikana sokoni Kariakoo eneo maarufu kama Shimoni katika meza ya mfanyabiashara ya Munguatosha.

KUNDE
 Karibuni sokoni Kariakoo mjipatie bidhaa mbalimbali zikiwemo kunde na bidhaa nyinginezo nyingi.

Tuesday, January 7, 2014

KMC STAFF


Pichani ni baadhi ya watumishi wa Shirika la Masoko ya Kariakoo Jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye ofisi ya Afisa biashara mapema leo asubuhi.

SOKO LA WAZI KARIAKOO


Pichani hapo juu ni eneo la wazi la soko Kuu la Kariakoo ambalo ni maarufu kama soko la wazi, eneo hili unaweza kupata matunda na mboga mbalimbali kama vile nyanya, maembe, karoti, hoho, pilipili na mengine mengi.

Thursday, January 2, 2014

BEI YA SAMAKI YA PANDA KUTOKA SH.15,000/= HADI 16,000/= KWA KILO

Pichani hapo juu ni mteja wa samaki aliyefika katika maduka ya samaki wabichi ndani ya Soko Kuu la Kariakoo Jijini Dar es Salaam.
Samaki wanaoonekana pichani hapo juu wanauzwa Shilingi 16,000/= kwa kilo moja na shilingi 4,000/= kwa kipande.

Monday, December 30, 2013

MAANDALIZI YA SIKU KUU YA MWAKA MPYA 2014


Pichani hapo juu ni baadhi ya wafanyabiashara wa soko la wazi la Kariakoo, wakiwa na wateja wao mapema leo asubuhi. Soko la wazi Kariakoo unaweza kupata mahitaji yako mbalimbali kama inavyoonekana pichani hapo juu.


Jipatie nyanya kwa Shilingi 5,000=/ tu sokoni Kariakoo Jijini Dar es salaam Tanzania, bidhaa hizi zinatoka sehemu mbalimbali nchini Tanzania kama vile Morogoro, Mwanza, Iringa, Tanga na maeneo mengine nchini.

Nyanya zikiwa kwenye sado ya lita4 zikiuzwa kwa shilingi 5,000
Viazi vinauzwa kwa shilingi 7,000=/ tu!



Thursday, December 26, 2013

WATU WAFURIKA SOKONI KARIAKOO KUFUATA BIDHAA

Magari yakiwa yameegeshwa katika eneo la soko Kuu la Kariakoo Jijini Dar es Salaam. 


 Pichani hapo juu ni baadhi ya wateja waliofika sokoni Kariakoo Jijini Dar es Salaam wakipata huduma kutoka kwa wafanyabiashara wa sokoni hapa, mahala hapa palikuwa panauzwa nguo kwa bei ya chini sana.

Maegesho ya magari katika eneo la soko Kuu la Kariakoo likiwa limefurika magari ya watu mbalimbali waliokuja Kariakoo kujipatia huduma kama inavyoonekana pichani hapo juu.

Sunday, December 22, 2013

BIDHAA SAFI NA BORA ZINAPATIKANA SOKONI KARIAKOO JIJINI DAR ES SALAAM

Wafanyabiashara wa Soko la Wazi Sokoni Kariakoo, wakiwa na wateja wao mapema leo asubuhi katka soko Kuu la Kariakoo Jijini Dar es Salaam.

Katika msimu huu wa siku kuu karibuni sokoni Kariakoo wateja wetu wote ili muweze kujipatia bidhaa bora sokoni Kariakoo Jijini Dar es Salaam.