Wednesday, October 23, 2013

YALIYOJILI KATIKA HARUSI YA MKUU WA KITENGO CHA ICT -KARIAKOO


Muda mfupi kabla ya kuanza ibada ya ndoa katika Kanisa la KKKT Kijitonyama Jijini Dar Es Salaam;kutoka kushoto ni Bwana harusi Anderson Shaka Mjanga na bestman wake bwana Aron Mjema,wengine ni Frank Mangowi mfanyakazi wa kitengo cha ICT KMC na mwingine ni Kamili Simba pia mfanyakazi wa KMC


Muda mfupi kabla kufunga ndoa Bwana Harusi na Best Man wake wakiwa katika viwanja vya kanisa la KKKT Kijitonyama Jijini Dar Es Salaam. Hii ilikuwa Jumamosi  ya tarehe 19/10/2013

Bwana na Bibi harusi wakiwa wamepozi katika picha ya pamoja mara baada ya kufunga ndoa yao Jumamosi ya tarehe 19/10/2013.
Katika picha hapo juu ni kikundi cha Matarumbeta cha Kanisa la KKKT Kijitonyama jijini DSM kikitumbuiza kanisani hapo mara baada ya Bwana Anderson Shaka Mjana Na Bi Neema Elibariki Mshanga kufunga ndoa yao kanisani hapo Jumamosi ya tarehe 19/10/2013. Bwana harusi ni Mkuu wa Kitengo cha ICT katika Shirika la Masoko ya Kariakoo na Bibi harusi ni Mjasiriamali.

 
Maharusi wakiwa katika picha ya pamoja na ndugu na jamaa  mara baada ya kufunga ndoa katika Kanisa la KKKT Kijitonyama Jijini Dar Es Salaam,Jumamosi ya tarehe 19/10/2013.

Maharusi wakiwa katika picha ya pamoja na Wazazi wa pande zote mbili yaani familia ya Mzee Mjanga na Mzee Mshanga;mara baada ya vijana wao kufunga ndoa jumamosi ya tarehe 19/10/2013, kanisani Kijitonyama KKKT.

Ndugu wa Bwana harusi wakifurahia mara baada ya Ibada ya kufunga ndoa kumalizika kati ya Bwana Anderson Shaka Mjanga na Bi Neema Elibariki Mshanga KKKT pale Kijitonyama.Mwenye suti kushoto ni mdogo wake na Bwana harusi Daktari S.Mjanga toka Hospitali ya Mkoa wa Morogoro;na mwingine ni binamu yake na Bwana harusi.
Muda mfupi baada ya Bwana Anderson Shaka Mjanga  kufunga ndoa  na Bi Neema Elibariki Mshanga.
Katika picha hapo juu ni kikundi cha mameds waliopamba sherehe za harusi ya Bwana Anderson Shaka na Bi Neema Mshanga kwa kucheza Show kali! iliyofanyika Jumamosi ya tarehe 19/10/2013.Ndoa ilifungwa katika kanisa la KKKT Kijitonyama na baadaye tafrija fupi kufanyika katika Ukumbi wa Dolphin 1998 LTD uliopo Sinza karibu na S/Msingi Mugabe.kutoka kushoto ni Everine,Erica,Amina,Munira na Joyce.

  Katika picha hapo juu ni kikundi cha mameds waliopamba sherehe za harusi ya Bwana Anderson Shaka na Bi Neema Mshanga kwa kucheza Show kali! iliyofanyika Jumamosi ya tarehe 19/10/2013.


PATA BIDHAA BORA KUTOKA SOKO LA KARIAKOO

Pichani ni Mhasibu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo (KMC) Bw. Ibrahim Marsha aikwa ofisini kwake hivi karibuni. katika mahojiano yaliyofanywa baina ya mchambuzi wa maswala ya ICT ya Shirika la Masoko ya Kariakoo (Frank Mangowi) hayupo pichani. Marsha alielezea historia fupi ya Shirika la Masoko ya Kariakoo, bofya hapa ili kupata historia ya Shirika la Masoko ya Kariakoo.




Aidha Marsha anachukua nafasi muhimu kuwakaribisha wateja kujipatia bidhaa mbalimbali zinazopatikana sokoni Kariakoo Jijini Dar es Salaam Tanzania.

Hapa ndipo Kariakoo Sokoni, picha ikionesha Soko kubwa(kushoto) na Soko dogo(kulia) la Kariakoo jijini Dar es Salaam.




Monday, October 21, 2013

PEMBEJEO ZA KILIMO ZINAPATIKANA SOKONI KARIAKOO




Wakati serikali ikiweka jitihada nyingi katika kuinua uchumi nchini (KILIMO KWANZA), kuwa na uhakika wa chakula cha kutosha, wafanya biashara pia hawako nyuma, wengi wao hapa nchini wamekuwa wakiuza pembejeo za kilimo cha kisasa kama inavyoonekana katika picha. Mfanya biashara () aliyepo ndani ya soko Kuu la Kariakoo (KMC) akionesha mfuko wa dawa “Ivory M 72 wp” inayosaidia kuondoa ukungu,fangasi  katika mimea mbalimbali kama mua, mboga za majani nk.
Miongoni mwa bidhaa zinazopatika ni pamoja na mbegu za Arizeti, mbegu za maboga, mahindi, figiri mchina na nyinginezo nyingi.
Pichani ni miongoni mwa mbegu za kisasa za mazao mbalimbali zinazopatikana dukani  “ZAWADI AGROVET” lilopo ndani ya soko kuu la Kariakoo-Dar es salaam.
Simu :0764 534005 au 0716 931940.



Friday, October 18, 2013

JIPATIE PILIPILI, VIAZI, VITUNGUU KWA BEI NAFUU SOKONI KARIAKOO


Jipatie pilipili

Wafanya biashara wakiwa kwenye harakati za kuandaa bidhaa zao kwa ajili ya biashara mapema leo asubuhi.


Wafanya biashara wakiwa kwenye harakati za kuandaa bidhaa zao kwa ajili ya biashara mapema leo asubuhi Sokoni Kariakoo Jijini Dar es Salaam.

Thursday, October 17, 2013

Maonesho

Afisa Biashara Muandamizi wa Shirika la Masoko ya Kariakoo Bi.Daynes Sooi (katikati) akizungumza na wawakilishi wa Kikundi cha MUDA Afrika sambamba na wawakilishi wa UN hivi karibuni. MUDA Afrika walihitaji kupewa nafasi watakayo fanyia shughuli zao za maonesho kwa muda wa siku mbili katika eneo la Soko Kuu la Kariakoo.
_______________________________________________________________________

Pichani Afisa Biashara Muandamizi wa Shirika la Masoko ya Kariakoo Bi.Daynes Sooi akiendelea na mazunguzo na wawakilishi wa MUDA Afrika.
_____________________________________________________________________

Tuesday, October 15, 2013

KIBA INVESTMENT: WAUZAJI WA VIUNGO VYA PILAU SOKONI KARIAKOO




Pichani ni baadhi ya viungo vya pilau vinavyo patikana katika duka la KIBA INVESTIMENT, duka lililopo Sokoni Kariakoo.
Vitunguu maji

vitunguu swaumu

Mr. Kiba,  mmoja ya wafanya biashara maarufu sokoni kariakoo akiwa dukani kwake mapema leo asubuhi.

HEKA HEKA ZA SIKU KUU YA IDD EL HAJJ

Wateja wakijipatia mahitaji yao sokoni Kariakoo kama inavyoonekana hapo juu pichani, hili ni eneo la wazi la Soko Kuu la Kariakoo Jijini Dar es Salaam.

Nyanya, vitunguu, hoho karoti zapatikana kwa wingi Sokoni Kariakoo.
Njegere
Katika harakati za siku kuu ya Id-Elhaj baadhi ya bidhaa zapanda bei, baadhi ya bidhaa hizo ni kama vile njegere.

Baadhi ya bidhaa ambazo zimeonekana kupatikana kwa wingi sokoni Kariakoo ni pamoja na nyanya, vitunguu maji & swaumu.



Pichani ni mfanya biashara wa Soko Kuu la Kariakoo eneo la Soko la wazi Merck Wandao Twanga  ambae pia ni Mwenyekiti wa wafanya biashara wa eneo la wazi sokoni Kariakoo.




Jipatie karoti, hoho, tango







Thursday, October 10, 2013

YALIYOJILI LEO SOKONI KARIAKOO!!

Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo, Ndugu Florens M. Seiya, akiongoza mkutano wa  Menejiment ya Shirika la Masoko ya Kariakoo leo,ikiwa ni moja ya  mikutano ya asubuhi ya kawaida ambayo hufanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Shirika. Mikutano ya namna hii hufanyika mara mbili katika wiki  ikiwa na lengo la kujadili na kutathimini utendaji kazi.


katika picha hapo juu ni Meneja wa fedha Mrs.Marieta Masaua akiwasilisha taarifa ya mapato ya Shirika,kushoto kwake ni Afisa Biashara Muandamizi wa Shirika la Masoko ya Kariakoo Bi.Daynes Sooi


Bwana Marco Mganga , Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi akifuatilia kwa makini maelezo ya Meneja wa fedha mapema leo asubuhi katika mkutano ambao ulifanyika katika ukumbi wa mikutano.

Menejimenti ya Shirika la Masoko ya Kariakoo ikiwa katika mkutano wake wa kawaida leo asubuhi! Mkutano ulifanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Shirika la Masoko.



Bi.Kamugisha  Mkuu wa kitengo cha Usafi katika Shirika la Masoko ya Kariakoo akifuatilia jambo katika  mkutano wa asubuhi mapema leo asubuhi.

Bi.Primitiva Kamugisha Mkuu wa Kitengo cha Usafi katika Shirika la Masoko ya Kariakoo akiwa katika mkutano wa kawaida wa Menenjimenti wa asubuhi , kulia kwake  ni Bi. Gloria Kalabamu  Mkuu wa Kitengo cha sheria Shirika la Masoko.

NJOO KARIAKOO UJIPATIE SAMAKI WABICHI.


 Pichani ni mfanya biashara maarufu wa samaki anayejulikana kwa jina la Bw Ramadhani Mlekwa anayefanya shughuli zake katika Soko kuu la Kariaoo. samaki wanaoonekana pichani ni aina ya "King fish"


 Mteja akihakiki uzito wa samaki aliyemnunua  kwa kupima katika mizani.Samaki hawa wanapatikana Sokoni kariakoo.


Baadhi ya wateja waliofika leo  kununua samaki ndani ya Soko Kuu la Kariakoo kama inavyoonekana
pichani.Sokoni Kariakoo kila bidhaa hupatikana  kuanzia  Nafaka,Matunda,Viungo,Mbogamboga,Samaki na nyama


 Wafanya biashara wa Shirika la Masoko ya Kariakoo wakiuza bidhaa zao kama inavyoonekana pichani, katika soko la wazi. katika vipimo vya lita nne maarufu kama sado.Nyanya zinauzwa kati ya Sh.2000/= hadi Shilingi 3000/=kwa bei ya leo kwa sado



Biashara ya nyanya, karoti,hoho na nyinginezo mbalimbali hufanyika katika  Soko kuu la  Kariakoo kwa bei za rejareja na jumla. Katika hapo juu ni moja ya wafanya biashara mashuhuri sana hapa Sokoni akiwa katika meza yake! Karibuni wote mjipatie bidhaa safi na bora!!









Mawasiliano katika biashara ni mhimu! mama ambaye jina lake halikupatikana mapema akipanga bidhaa zake katika meza ya biashara huku akiwasiliana  na wateja wake kama anavyooneakana katika picha.


Kitengo cha Usalama katika Shirika la Masoko ya Kariakoo



Katika picha hapo juu ni  mtuhumiwa wa wizi wa simu akiwaamekula pingu baada kutiwa mbaroni kwa tuhuma ya kuhusika katika wizi wa simu.Hapo anasubiri kuhojiwa na Afisa muandamizi wa Usalama
.

Katika picha hapo juu ni  mtuhumiwa wa wizi wa simu akiwa chini ya ulinzi mkali wa askari wa usalama wa Shirika la Masoko ya Kariakoo. (Jina lake limehifadhiwa)








Tuesday, October 8, 2013

Staff

Bwana Paul Kiwera Mkaguzi Mkuu wa ndani wa Shirika la Masoko ya Kariakoo akiwa Ofisini kwake.
Katika picha hapo juu ni Bwana Flavian Mlellwa Mkuu wa kitengo cha Uhandisi  katika  Shirika la Masoko ya Kariakoo akiwa Ofisini kwake.
Bwana Rogers Kuyonga akiwa Ofisini kwa Muhandisi wa Shirika akipewa maelekezo ya namna ya kuwatangazia matangazo mbalimbali wafanyabiashara wa sokoni hapo, mkononi mwake akiwa ameshika kipaza sauti.


Baadhi ya Mitambo inayo tumika kwa ajili ya kutangaza matangazo mbalimbali katika Shirika la Masoko ya Kariakoo; Soko kuu la Kariakoo lipo Jijini DSM.