Wednesday, April 30, 2014

Sokoni Kariakoo leo!

 Mfanyabiashara Bwana Hussein akiwa ameegemea gari ambalo limebeba  Matikiti yake ambayo aliyafikisha Sokoni Kariakoo . Hapo alikutwa akiwa eneo la Soko la Jumla eneo maarufu kwa jina la Shimoni.
Eneo hilo katika picha hapo ni eneo la wazi lililopo kati ya Jengo la Soko Kuu la Kariakoo na Soko Dogo ambayo yote kwa pamoja yanasimamiwa na Uongozi wa Shirika la Masoko ya Kariakoo. Kwa watu waliozoea siku zilizotangulia eneo hili lilikuwa ni eneo ambalo kila aina ya bidhaa za Matunda,Mbogamboga,Viazi na bidhaa nyinginezo zilikuwa zikiuzwa na Wajasiriamali/ Wafanyabiashara katika eneo hili; Lakini sasa kwa takribani mwezi sasa unakamilika pamekuwa wazi kama panavyoonekana kufuatia bomoa bomoa ya Manispaa ya Ilala kuingia hadi katika eneo hili la Soko.

Monday, April 28, 2014

Sokoni Kariakoo Leo! Karibuniiii!

 Kijana huyu anaeonekana katika picha hapo juu alijitambulisha kwa jina  la Said Eyasi;  alikutwa mapema leo katika eneo la Soko la Jumla eneo la Shimoni. Alipohojiwa kuwa anafanya nini huko? Alijibu kuwa yeye anafanya biashara ya mifuko. Kijana huyu ana umri wa miaka 13 hivi sasa;hata alipoulizwa kuhusu shule, alijibu kuwa yeye alikwisha hitimu elimu ya msingi muda mrefu.

Thursday, April 10, 2014

Matumaini mapya kwa Wafanyabiashara Sokoni Kariakoo!

 Katika picha hapo juu ni jopo la Wakaguzi wa ndani wa Shirika la Masoko ya Kariakoo wakiangalia ubora wa maumbo amabayo yaliletwa katika Ofisi za Shirika  jana.Maumbo hayo yakiisha kuthibitishwa yataanza kutumika katika eneo la Soko la Wazi lililopo kati ya Jengo Kuu la Soko na Soko Dogo ambapo Wafanyabiashara  watayatumia kupanga bidhaa zao mablimbali humo na kuwauzia wateja.Wakaguzi hao wakiongozwa na Mkuu wao Bwana Paul Kiwera aliyevaa kitambulisho kutoka kulia, Bwana Ncheya Kulwa na Bwana Longino .A.k.a Mkulu wa Bangoye!
Katika picha hapo juu ni "Sampo"(sample) ya maumbo ambayo yanatarajiwa kutumiwa na Wafanyabiashara ambao mapema wiki  iliyopita walibomolewa meza zao katika eneo la Soko la  Wazi la Kariakoo.Eneo hilo ni sehemu ya Kiwanja cha Soko Kuu la Kariakoo. Wafanyabiashara hao watakuwa wanatumia maumbo hayo kupanga bidhaa zao mabalimbali wanazoziuza sokoni hapo.

Ziara ya Meneja Mkuu wa Shirika pamoja na Timu yake ya Menejimenti ya Shirika.

 Meneja Mkuu akipata maelezo kutoka kwa Muhandisi wa Shirika Bwana Flavian Mlellwa wakati wa ziara ya kuzungukia maeneo ya Soko kuu la Kariakoo mapema leo asubuhi.Meneja Mkuu Bwana Florens Seiya aliambatana na Wakuu wa Idara na Vitengo ambao wote kwa pamoja huunda Menejimenti ya Shirika. Kutoka Kushoto aliyeshika Radio Call ni Mkuu wa Kitengo cha Usalama Bwana Mzava,anayefuata ndiye Meneja Mkuu,anayetoa maelezo ni Mkuu wa Kitengo cha Matunzo(Muhandisi),na wengine ni Meneja wa Fedha Mrs. Marieta Masauwa na Bi.Dainess Sooi anayekaimu nafasi Meneja Mipango na Biashara .
 Mfanyabiashara wa Mbogamboga katika eneo la Soko dogo akiongea na Meneja Mkuu wa Shirika kama alivyokutwa na leo asubuhi katika eneo lake la biashara.
 Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko Bwana pamoja Menejimenti yake wakiwa wanapokea maelezo kutoka Mfanyabiashara akielezea jinsi ambavyo huwa wanapanga bidhaa zao katika eneo hilo. Hapo katika eneo la Soko dogo.
 katika picha hapo juu ni Kisima cha Maji ambacho kinamilikiwa na SMK kipo katika eneo la Soko Dogo. Wiki iliyopita kilikuwa kimeharibiwa kwa kuvunjwa Pampu yake wakati wa bomoabomoa.Ndugu msomaji kama unavyoona katika picha kisima hicho kimefanyiwa ukarabati na Kitengo cha Uhandisi cha Shirika la Masoko na hatimaye kuanza kutoa huduma ya maji tena.

 Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko aliyetangulia mbele akiwa anarejea Ofisini kwake leo asubuhi mara baada ya kuzungukia maeneo mbalimbali ya Soko Kuu la huku akiwa ameambatana na Menejimenti yake.
Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo  Bwana Florens Seiya akifanya majumuisho ya ziara alioifanya ya kuangalia na kuzungumza na baadhi ya Wafanyabiashara ambao hufanya biashara zao katika maeneo kadhaa ambayo yalikumbwa na bomoabomoa ya Manispaa wiki iliyopita. Majumuisho hayo aliyafanyia Ofisini kwake leo asubuhi baada ya ziara aliyokuwa ameambatana na Wajumbe wa Menejimenti ya Shirika.

Habari katika Picha toka Shirika la Masoko ya Kariakoo

Hii ni sehemu ya Wajumbe waliohudhuria Mkutano wa dharula ulioitishwa na Chama cha Wafanyakazi TUICO ili kupeana taarifa za mstakabali wa yaliyotokea na hatua zilizochukuliwa na Uongozi wa Shirika la Masoko ya Kariakoo.Pia katika mkutano huo Uongozi wa TUICO uliwakumbusha Watumishi wa Shirika kuwa na mshikamano wa pamoja ili kuona kuwa Shirika likzidi kupiga hatua kimaendeleo.
 Kutoka kulia ni Katibu wa TUICO katika Shirika la Masoko ya Kariakoo Bibi Ester Chogero,Bwana Joseph Mweyo Mwenyekiti wa TUICO ,na Bwana Ibrahimu Masha amabaye ni Mjumbe wa TUICO Taifa kutoka Shirika la Masoko ya Kariakoo. Wote kwa pamoja wakiendesha Mkutano a Wafanayakazi jana mchana. Mkutano huo ulilenga kujadili Agenda kuu mbili tuu ikiwamo Mwenendo mzima wa Watumishi wa Shirika pamoja na Kuwajulisha Wafanyakazi kuhusu zoezi la bomoabomoa amabalo ililikumba  Shirika wiki iliyopita.
 Aliyesimama ni Katibu Mkuu wa TUICO  Bibi Ester Chogero akisoma waraka maalum sana amabao ulihusishwa na  moja ya agenda muhim zilizojadiliwa katika Mkutano huo wa dharula ulioitishwa na Uongozi huo wa TUICO.
 Viongozi wa TUICO tawi la Masoko ya Kariakoo wakishauriana jambo na Wajumbe wa Menejimenti ya Shirika la Masoko ya Kariakoo. Hii ilikuwa ni jana Jumatano ilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Shirika hilo.
Wafanyakazi wa Shirika la Masoko ya Kariakoo wakitoka nje baada ya mkutano wa Dharula ulioitishwa na Chama cha Wafanyakazi TUICO Tawi la Masoko.Mkutano huu ulifanyika jana Jumatano tarehe 9/4/2014 mchana.

Tuesday, April 8, 2014

Kutoka Kariakoo leo Jioni

 Katika picha hizi utaona ni Timu ya Menejimenti pamoja na Wafanyabiashara wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa Shirika la Masoko ya Kariakoo,hapa walikuwa wakipewa mrejesho wa kikao ambacho kilikuwa kimefanyika Kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ofisini kwake na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala. Hii imekuja baada ya uharibifu ulifanyika katika Soko la Kariakoo mwishoni mwa wiki iliyopita.
 Wajumbe wa Menejimenti ya Shirika la Masoko ya Kariakoo pamoja na Ujumbe wa Wafanayabiashara kwa pamoja wakiwa wanasikiliza mrejesho wa Kikao baina ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala,Mkuu wa Wilaya ya Ilala na Ujumbe wa Shirika la Masoko ya Kariakoo ulioongozwa na Meneja Mkuu wa   Shirika la Masoko ya Kariakoo. Katika kikao hiki Meneja Mkuu hakuwepo badala yake aliwakilishwa na Meneja wa Fedha ambaye aliambatana naye.
Mfanyabiashara Mzee Mwinyishehe mwenye kofia akiwa anamsikiliza mjumbe mmojawapo alipokuwa anachangia mawazo na kuishukuru timu nzima iliyokuwa imeambatana na Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo. Mrejesho wa kikao hicho uliwasilishwa na Mrs.Marieta Masaua Meneja wa Fedha kwa niaba ya Meneja Mkuu wakisaidiana na Mzee Mwinyishehe kama Muwakilishi wa Wafanayabiashara na  Kaimu Mhandisi wa Shirika Bwana Flavian Mlelwa

Friday, April 4, 2014

Uharibifu umeendelea tena usiku wa kuamkia leo katika Shirika la Masoko ya Kariakoo

 Katika picha hapo juu ni sehemu ya Pampu ya maji ambayo ilikuwa inatumika kusukuma maji katika kisima ambacho kipo eneo la Soko dogo la Kariakoo.Pampu hii imevunjwa usiku wa kuamkia leo na Burudoza la Manispaa ya Ilala katika zoezi lao.Ndugu Msomaji Pampu hii ilikuwa ndani ya kiwanja cha Shirika la Masoko ya Kariakoo;lakini ndiyo hivyo imevunjwa.
 Katika picha hapo juu ni Watumishi wa Shirika la Masoko ya Kariakoo Bwana Flavian Mlelwa na Denis Mfuruki kutoka Kitengo cha Uhandisi wakifungua mabomba ya maji yaliyokuwa yameunganishwa na Pampu amabayo imevunjwa .Kuvunjwa kwa Pampu hii kumelitia hasara kubwa  Shirika  la Masoko.
Hapa katika picha Wahandisi wa Shirika wakimalizia kufungua nyaya za umeme ambazo zilikuwa zinatumika kupeleka  nishati ya umeme kwenye Pampu ya maji ambayo imevunjwa.

Thursday, April 3, 2014

Shirika la Masoko ya Kariakoo lavamiwa Mapema leo alfajiri!

 Mapema leo alfajiri Soko Kuu la Kariakoo lilivamiwa na Kundi la Mgambo wa  kutoka Manispaa ya Ilala linaloendesha zoezi la kusafisha Jiji la Dar Es Salaam na kufanya uharibifu mkubwa kama unavyoonekana katika picha hapo juu. Kitendo hiki kimeushitua Uongozi wa Shirika la Masoko pamoja na Wafanyabiashara ambao huendesha shughuli zao katika Soko hili.
 Eneo lililovamiwa na kuharibiwa kabisa ni hilo linaloonekana katika picha hapo juu;lipo katikati ya Jengo Kuu lenye paa la miavuli  kushoto na Soko Dogo kulia ambalo katika picha hapo lina rangi ya kijani eneo hilo ni maarufu kama Soko la Wazi.Uharibifu huu ambao umefanyika mapema leo alfajiri umewaacha Wajasiriamali wengi katika hali ya sitofahamu hatma yao; lakini zaidi umeliingiza Shirika la Masoko katika hasara ambayo ni kubwa kimapato.
 Kwa mujibu wa ramani hiyo hapo juu Kiwanja ambapo Soko Kuu la Kariakoo lilipo ni Eneo hilo katika mgawanyo wa viwanja linaonekana lenye umbo la herufi L (Block 40) na kwa mujibu wa ramani hiyo ambayo imesainiwa na Wizara yenye dhamana na ardhi inaonyesha eneo hilo lililovamiwa na kuharibiwa linamilikiwa na Shirika la Masoko ya Kariakoo.
Eneo hili kwa wale watu wenye  mazoea ya  kufika katika Soko Kuu la Kariakoo kujipatia mahitaji bila shaka watakuwa wanalijua , huwapo Wafanyabiashara wengi wakiwemo akina Mama Wajasiriamali na Vijana ambao hudamka mapema kila siku na kufanya biashara zao! lakini ilikuwa ni tofauti kabisaa  leo pale walipofika na kuona eneo hilo limeharibiwa na Wanamgambo hao wa Manispaa ya Ilala.

Tuesday, April 1, 2014

Kutoka Kariakoo Soko Kuu leo

 Soko Kuu la Kariakoo lililopo Jijini Dar Es Salaam ni kubwa siyo  tuu Tanzania hapa; bali katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati.Hii hapa katika picha ni sehemu tuu ya Soko hili ambayo imejengwa katika mfumo wa Handaki  kuingia kwenda katika sehemu ya Soko la Jumla maarufu kama Shimoni.Magari ya mizigo huingia Shimoni kwa kupitia njia hii kwenda kushusha bidhaa ma mbalimbali kavile Matunda,Viazi,Ndizi na nyinginezo nyingi.
Usalama wako wewe na mali zako Mteja au Mfanyabiashara uwapo  Soko kuu la Kariakoo lililopo Jijini Dar Es Salaam siyo wa kutafuta! Ulinzi ulioimara na madhubuti kabisa upo. Kama uonavyo mwenyewe katika picha hapo juu ni moja ya Maafisa waandamizi wa Usalama wa Shirika la Masoko Kariakoo akiwa na Radio Call yake mezani ambayo hutumika katika harakati za kuhakikisha usalama upo sokoni.Bwana Beatus Moringe ni mtu mwenye uzoefu wa muda mrefu katika masuala ya usalama.

USAFI NI SEHEMU YA MAISHA YETU SOKO KUU LA KARIAKOO

Shirika la Masoko ya Kariakoo (SMK), huzingatia sana suala zima la Usafi katika maeneo yake kila siku. Katika picha hapo juu ni Gari mojawapo kati ya mengi likiwa eneo la Shimoni likiwa linapakia takataka; hufanya kazi ya kuondoa takataka zinazozalishwa Katika Soko Kuu la Kariakoo kutokana na uingizwaji wa bidhaa mbalimbali toka mikoani.Magari haya hufanya kazi Usiku na Mchana ili kuhakikisha eneo la Soko  Kuu la Kariakoo linakuwa safi muda wote.
Katika picha hapo juu ni Bwana Seifu Abdalah ambaye  ni Mtumishi wa Shirika la Masoko kutoka katika Idara ya Usafi,alikutwa eneo la Shimoni akikagua mifereji ya Majitaka inayopita eneo hilo ili kuhakikisha Mfumo mzima wa maji taka upo sawa sawa.Kutokana na umuhimu wa Mfumo huu wa majitaka katika miundombinu ya Soko hili ukaguzi kama  huu hufanyika kila siku na mara kwa mara.