TANGAZO LA KAZI
Shirika
la Masoko ya Karikaoo ni Shirika la Umma lililoanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya
Bunge Na.32 ya mwaka 1974 na kupewa majukumu ya kusimamia na kuendesha Soko Kuu
la Kariakoo pamoja na Masoko mengine yatakayokuwa chini ya usimamizi wa Shirika
pia kujenga Masoko mengine mapya katika Jiji la Dar es Salaam na kusimamia
uendeshaji wake. Shirika linakaribisha maombi ya nafasi mbili za kazi zifuatazo:
- Mwanasheria Daraja la 11
Muombaji
awe na Shahada ya Sheria kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na Serikali. Awe
amepitia Shule ya Sheria na kusajiliwa kama Wakili.
Kazi
na Majukumu.
Kushauri
masuala ya kisheria katika Shirika la Masoko ya Kariakoo.
Kuandaa
nyaraka zote za kisheria kwa ajili ya kusaidia kufikia malengo ya Shirika.
Kufuatilia
na kutunza kumbukumbu muhimu kwa ajili ya kutumika kwenye mashauri Mahakamani.
Kuandaa
mihutasari ya mashauri mbalimbali ya shirika yaliyopo mahakamani.
Kuandaa
na kupeleka notisi za kisheria kwa wadaiwa wa shirika .
Kufanya
shughuli yeyote atakayo pangiwa na Meneja Mkuu au Mkuu wa kitengo.
- Ofisa Ugavi Msaidizi
Muombaji
awe na Stashahada ya katika fani ya ununuzi na ugavi, awe amesajiliwa na PSPTB
Kazi na Majukumu.
Kuhakikisha
kuwa vifaa vinavyonunuliwa vinapokelewa na kuingizwa katika vitabu vya
Shirika..
Kuhakikisha
kuwa nyaraka zote za stoo zinajazwa kwa ufasaha na kwa wakati.
Kuhakikisha
kuwa mali zote zilizoifadhiwa stoo zinatuzwa
bila upotevu wowote.
Kuhakikisha
kuwa uingizaji na utoaji wa bidhaa unafuata sheria na kanuni za manunuzi ya
umma.
Kuhakikisha
kuwa vifaa na mali zinazohifadhiwa stoo zinatunzwa katika mpangilio mzuri
Kufanya kazi zozote
atakazopangiwa na Mkuu wa Kitengo.
MASHARTI
YA JUMLA
Waombaji
wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
Waombaji wote waambatishe nakala ya cheti cha
kuzaliwa. Na picha (passport size) moja ya rangi
Waombaji
waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye
anwani na namba za simu pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu
wa kuaminika.
Maombi yote yaambatane na nakala za
vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho
na nakala ya vyeti vya kuhitimu mafunzo
mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
Mwisho wa Kupokea maombi ni 29/08/2015.
Maombi hayo yatumwe kwa :
Meneja Mkuu,
Shirika la Masoko ya Kariakoo,
P.O.BOX 15789,
Dar es Salaam.
Na kwa Email: info@kariaakoo.or.tz.
No comments:
Post a Comment