Thursday, February 26, 2015

Sokoni Kariakoooo leoo!

 Huyu kijana alijitaja jina lake kuwa ni Abdul Abubakari baada yakupata kibano pale alipokamatwa akiwa katika harakati za kuiba vioo vya kwenye magari ambayo yameegeshwa katika eneo la Soko Kuu la Kariakoo.Kijana huyu alinaswa na vijana ambao walikuwa wanaosha magari mapema leo asubuhi
 Katika picha hapo juu ni baadhi ya vifaa vya magari ambavyo kijana huyu alipatikana navyo kijana Abdul Abubakari.
Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi  katika Shirika la Masoko Kariakoo, Bwana Mathias Mbafu akiwa Ofisini kwake akimuelekeza jambo  Msaidizi wake Bi.Henrika Kawili.

Monday, February 23, 2015

Aina mbalimbali za Mazao/Vyakula katika Soko Kuu

 Maboga nayo pia hupatikana hapa katika Soko Kuu la Kariakoo katika bei tofautitofauti,maboga ni miongoni mwa vyakula ambavyo hupendwa na watu wa kada tofauti.

 Viazi mviringo kutoka mikoa ya Nyanda za juu Kusini kama vile Njombe,Mbeya na Iringa, huingia Sokoni Kariakoo kila siku.
Vitunguu safiii kabisa kutoka mikoani Singida,Mbeya,Iringa na kwingineko huingia katika Soko Kuu la Kariakoo.

Thursday, February 19, 2015

Miongoni mwa Watumishi wa Shirika la Masoko

 Kama ilivyo kawaida katika Taasisi mbalimbali za Serikali kuwa na Watumishi wa kada tofautitofauti, katika picha hapo juu ni Bwana Rogers Kuyonga kutoka Kitengo cha Matunzo na Roman Winfred kutoka Kitengo cha Usalama,wote ni waajiriwa katika Shirika la Masoko Kariakoo.
Katika picha hapo juu  kutoka kushoto ni Bwana Charles Sombe mwenye suruali nyeupe kutoka Idara ya Utumishi,Ncheye Kulwa aliyeshika Notebook yeye yuko katika Kitengo cha ndani cha Ukaguzi na Bi.Jackline kutoka katika Idara ya Fedha

Tuesday, February 17, 2015

Bidhaa na Wafanyabiashara Sokoni Kariakoo-Jijini Dar Es Salaam.

 Limau ni moja ya viungo vnavyotumiwa sana na wapishi mbalmbali,Sokoni Kariakoo kuna kila aina ya bidhaa muhim unazozihitaji. Limau hizi huuzwa kwa bei ya rejareja na jumla. Eneo la shimoni ndiko hasa bidhaa hizi zinapatikana kwa wingi sana.

 Ndimu nazo hazijapungua hapa Sokoni Kariakoo,zinapatikana kwa wingi katika bei tofautitofauti kwa jumla na rejareja.Ndimu daraja la kwanza kabisa, fika Sokoni Kariakoo eneo la Shimoni.

 Mfanyabiashara huyu anayejulikana kwa jina la Munguatosha pichani hapo juu, yupo eneo la Shimoni yeye ni maalum tuu kwa uuzaji wa Karoti na pilipili hoho.Pia hupokea mazao kutoka kwa Wakulima mbalimbali kutoka mkoani,kama vile kutoka Wilayani Korogwe na Lushoto mkoani Tanga.
Bwana Dominik Zakayo ni miongoni mwa wafanyabiashara wa vitunguu saum na tangawizi katika Soko Kuu la Kariakoo eneo la Shimoni.Karibu ujipatie bidhaa mbalimbali.

Monday, February 16, 2015

TUICO-Tawi laShirika la Masoko Kariakoo wapata Uongozi mpya

 Katika picha hapo juu ni Viongozi waliosimamia zoezi la uchaguzi uliowezesha kupata viongozi wapya watakaliongoza Tawi hili katika kipindi cha miaka mitano ijayo kuanzia mwaka huu. Kutoka kushoto ni Bwana Ibrahim Masha ambaye ni Mjumbe wa TUICO Taifa ambaye pia ni mtumishi katika Shirika la Masoko, Bwana Godwin Mrosso amabaye ni Meneja Utumishi na Uendeshaji katika Shirika la Masoko ambaye huyu alimuwakilisha Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo, wengine ni Bwana Willy Kibona ambaye ni Katibu wa TUICO mkoa wa Ilala  na Bi.Maria John Bange yeye ni Mkuu Msaidizi  wa Idara yaWanawake TUICO Mkoa wa Ilala.Hapo walikuwa wakimalizia kujumlisha kura.
 Sehemu ya Wanachama wa TUICO Tawi ,wakiwa katika Ukumbi wa Mikutano wa Shirika la Masoko Kariakoo wakiwa katika hali ya kusubiria matokeo ya uchaguzi yatangazwe na Wasimamizi wa uchaguzi huo.Uchaguzi huo ulifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.
 Baadhi ya Wanachama walioshiriki katika uchaguzi  wakiwa wamesimama nje ya Ukumbi mara baada ya kumaliza kupiga kura za kuwachagua viongozi wa Tawi hilo kuanzia ngazi ya Mwenyekiti,katibu pamoja na Wajumbe wa Halmashauri ya Tawi.
 Katika picha ni Bwana Willy Kibona ateteta jambo na Mjumbe wa TUICO Taifa  Bwana Ibrahim Masha ambaye katika picha hayupo na kulia kwake ni Bi.Maria John Bange wote kwa pamoja walifika kusimamia shughuli nzima ya Uchaguzi huo.
 Katika picha hapo juu ni Bwana Ibrahim Masha Mjumbe wa TUICO Taifa akiwa tayari kabisa kuanza kutangaza matokeo ya uchaguzi mara baada ya zoezi la kuhesabu kura.
 Wanachama wakiwa wametulia kabisa wakisikiliza matokeo ya uchaguzi waliokuwa wameufanya .
 Bwana Ibrahim Masha akitanganza matokeo ya uchaguzi mara baada ya kumalizika kwa zoezi la upigaji kura na kuhesabu.

 Katika picha hapo juu ni dada ambaye alipendekezwa kufanya sala maalum kwa nia ya kumshirikisha  Mungu katika shughuli nzima ya uchaguzi huo.
 Pia katika picha hii hapo juu ni Mzee Idd Mrope nae pia alipendekezwa kufanya Dua maalum kwa ajili uchaguzi huo wakuwapata viongozi bora katika tawi la SMK.
 Wanachama wakiwa wanaimba na kufurahia mara baada ya kumalizika kwa uchagauzi na matokeo kuwa yametangazwa rasmi. Katika uchaguzi huo Bwana Denis Mfuruki alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa TUICO Tawi wakati  katika nafasi ya Katibu Bwana Henry Rweijuna aliibuka mshindi.

Katika picha hapo juu ni sehemu ya wanachama wakitoka ukumbini mara baada ya uchaguzi kumalizika, wakiwa wenye nyuso za furaha kwa kuwapata viongozi wapya watakao waongoza kwa kipindi cha miaka mitano.

Thursday, February 12, 2015

Hawa madogo vipi unawafahamuuuuuuuuuuu?

 Hawa watoto ambao wana rika yakuwa shuleni wanasoma!Lakini huonekana wakizurula ndani ya Soko Kuu la Kariakoo! Jambo ambalo huwapa wakati mgumu hata wateja mbalimbali wanaofika hapa sokoni kujipatia mahitaji mabalimbali!



 Asilimia kubwa ya watoto hawa wakihojiwa wanakotoka hutoa majibu kuwa wanatokea mkoa wa Tanga, na jambo la kusikitisha utafiti mdogo uliofanyika watoto hawa hufika hapa Sokoni kwa usafiri wa malori na tena wakiwa na umri dogo kati ya miaka 11 hadi 13, hivyo basi hukulia katika mazingira haya ya hapa Sokoni wakijishughulisha na kazi za hapa na palee!kujikimu kimaisha!
Katika picha hizo zote hapo juu ni watoto kadhaa waliokamatwa na Maafisa Usalama wa Shirika la Masoko Kariakoo mapema leo asubuhi! Basi ndugu Watanzania anayehusika na mtoto mmojawapo kati ya hao waliopo katika picha hizo, karibu ufike sokoni hapa Kariakoo ili uweze kumpata!

Kinachoendelea -Kariakoo Market Corporation

 Bwana Paul Nsimbila Mkufunzi mwenye laptop akiwa katika Ukumbi wa Shirika la Masoko wakati akiendesha semina kwa watumishi wa Shirika kuhusu Sheria mpya ya manunuzi na kanuni zake.
 Watumishi wa Shirika la Masoko ya Kariakoowaliohudhuria mafunzo ya kuhusu Sheria mpya ya manunuzi wakiwa wanafanya swali mojawapo alilowapa Mkufunzi Bwana Paul Nsimbila jana asubuhi, kama sehemu ya mazoezi
Watumishi katika makundi ya watu wawiliwawili wakiendelea na zoezi la kujibu swali mojawapo alilolitoa kama sehemu ya mazoezi katika mafunzo.

Tuesday, February 10, 2015

Semina Maalum kuhusu Sheria ya manunuzi ya Umma

 Katika picha hapo juu aliyesimama ni Bwana Paul Nsimbila Mtaalam wa Manunuzi kutoka PPRA akiwa amemaliza kugawa karatasi za maswali kwa Watumishi wa Shirika la Masoko ya Kariakoo ambao wanahudhuria Semina kuhusu manunuzi ya Umma.Mkufunzi Bwana Nsimbila alianza kutoa mafunzo hayo jana Jumatatu asubuhi katika Ukumbi wa mikutano wa Shirika hili, pamoja na mambo mengine Bwana Nsimbila anatoa mafunzo   kuhusu Sheria mpya ya manunuzi pamoja kanuni zake ili kuwajengea uwezo watumishi wa shirika hili katika kutekeleza shughuli za manunuzi kwa weredi na kuleta tija kwa Shirika.

 Katika picha hapo juu ni Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko la Kariakoo Bwana Florens Seiya na Meneja wa Fedha Bi.Marieta Massaua wakiwa wanajadiliana swali ambalo Mkufunzi Muwezeshaji kutoka PPRA Bwana Paul Nsimbila alikuwa ametoa kwa kila watu wawiliwawili ili kupima uelewa kuhusu namana ya kupangilia mpango mzima wa manunuzi wa mwaka ndani ya taasisi. (Annua Procurement Plan)

 Watumishi hawa katika picha kutoka kutoka Vitengo vya Manunuzi na Ukaguzi wakiwa wanaendelea na kufanya swali linalohusu (APP) yaani Annual Procurement Plan, kutoka kulia ni Bwana Mathias Mbafu (Mkuu wa kitengo cha Manunuzi), Bi.Henrika Kawili (Afisa Manunuzi na Ugavi), Bwana Longino Rugaikamu na Yustino Man wote kutoka Kitengo cha Ukaguzi.

 Hapo juu pichani ni Bwana Flavian Mlelwa ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Matunzo akiwa na Bi.Dayness Sooyi wakiendelea kufanya swali lililotolewa na Mkufunzi Muwezeshaji kutoka PPRA Bwana Paul Nsimbila, hii ni mapema leo asubuhi kabla ya somo jipya kuhusu sheria mpya ya manunuzi ya Umma na kanuni zake.

Katika picha hapo juu ni  Mkuu wa Kitengo cha Tehama Bwana Anderson Shaka Mjanga kushoto akiwa na Bwana Marco Mganga, Afisa Manunuzi  kutoka Kitengo cha Manunuzi, kwa pamoja wakijadiliana swali linalohusu mpango wa manunuzi wa mwaka.

Mkaguzi Mkuu wa ndani Bwana Paul Kiwera akiwa na Muhasibu Bi.Semeni Yamawe kwa pamoja wakiendelea kulichambua swali linalohusu Mpango wa manunuzi wa mwaka au Annual Procurement Plan kwa lugha ya kiutalaam. Bwana Paul Nsimbila Muwezeshaji katika mafunzo haya alitoa kuwapa watu walifanye ili ajiridhishe kuona kile anachowafundisha Watumishi hawa wanaelewa hasa na kwamba wataweza kufanya kwa vitendo mara baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo?

Watumishi wawili wa mwanzo ni Bwana Ncheye Kulwa na Luchemo Chiimba wote kutoka katika Kitengo cha Ukaguzi wakiwa makini kufuatilia jambo wakati mafunzo yakiendelea Ukumbini.Mafunzo hayo yakuwajengea uwezo Watumishi hawa wa Shirika yamekusudiwa kuwa ni siku tatu (3) yalianza jana Jumatatu 9/02/2015  na yatamalizika Jumatano ya wiki hii tarehe 11/02/2015

Thursday, February 5, 2015

Biashara ya vitunguu Sokoni

 Pichani hapo juu ni miongoni mwa Wafanyabiashara wa biashara ya vitunguu katika Soko Kuu la Kariakoo Bwana Abdul.Mfanyabiashara huyu yeye huuza vitunguu saum na tangawizi, pia na viungo vya pilau kama anaonekana katika  meza yake.Bei ya tangawizi iliuzwa kwa Sh.6000/- kwa kilo na Vitunguu saum ilikuwa Sh.8000/-
Vitunguu maji ni miongoni mwa bidhaa ambazo hupatikana katika katika Soko la Kariakoo. Bei ya vitunguu kwa jumla ni Sh.130,000/- kwa gunia.wakati kwa bei ya rejareja ni kati ya Sh.1000 na 1500.

Wednesday, February 4, 2015

Zabibu Sokoni Kariakoo


Katika picha hapo juu ni matunda aina ya zabibu ambazo huingizwa katika Soko Kuu la Kariakoo zikitokea mkoani Dodoma.Leo zilikuwa zikiuzwa kwa bei ya Sh.2500/- kwa kilo na kwa bei ya jumla ilikuwa ni Sh.30,000/-kwa  katoni au Box

Tuesday, February 3, 2015

Kutoka Soko Kuu la Kariakoo

 Muhandisi wa Shirika la Masoko ya Kariakoo Bwana Flavian Mlelwa akiwa katika hali ya kutafakari jambo wakati Mtumishi mwenzake Bwana Denis Mfuruki pichani hayupo alipomtembelea Ofisini kwake.
Bwana Flavian Mlellwa ambaye ni Muhandisi wa Shirika la Masoko ya Kariakoo akiwa Ofisini kwake mapema leo asubuhi. Mtumishi huyu ni nadra sana kuonekana ofisini akiwa amekaa ametulia hivi kwani muda mwingi huwepo katika maeneo mbalimbali jengo la Soko kukagua miundombinu na kusimamia shughuli mbalmbali za kiufundi hasa masuala yote yahusuyo umeme,maji na ukarabati wa sehemu mbalimbali za Jengo la soko.

Monday, February 2, 2015

Mazao Sokoni Kariakoo

 Coneflower ni mojawapo ya mazao ya mbogamboga yanayopatikana katika Soko Kuu la Kariakoo. Kwa bei za kawaida kabisa, unakaribishwa kujipatia mahitaji mabalimbali ya kila siku katika Soko hili Kongwe katika Jiji la Dar es Salamu. Aina hii ya mbogamboga zinazalishwa katika mikoa ya Tanga, Arusha na Morogoro.
Magimbi ni chakula kinachopendwa na watu wengi. Katika picha hapo juu ni magimbi fresh kabisa kutoka shambani. Bei ya magimbi huanzia kati ya shililngi 500 hadi 2000 kulingana na ukubwa wake.
Karibu sana Sokoni.