Soko Kuu la Kariakoo lililopo Jijini Dar Es Salaam ni kubwa siyo tuu Tanzania hapa; bali katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati.Hii hapa katika picha ni sehemu tuu ya Soko hili ambayo imejengwa katika mfumo wa Handaki kuingia kwenda katika sehemu ya Soko la Jumla maarufu kama Shimoni.Magari ya mizigo huingia Shimoni kwa kupitia njia hii kwenda kushusha bidhaa ma mbalimbali kavile Matunda,Viazi,Ndizi na nyinginezo nyingi.
Usalama wako wewe na mali zako Mteja au Mfanyabiashara uwapo Soko kuu la Kariakoo lililopo Jijini Dar Es Salaam siyo wa kutafuta! Ulinzi ulioimara na madhubuti kabisa upo. Kama uonavyo mwenyewe katika picha hapo juu ni moja ya Maafisa waandamizi wa Usalama wa Shirika la Masoko Kariakoo akiwa na Radio Call yake mezani ambayo hutumika katika harakati za kuhakikisha usalama upo sokoni.Bwana Beatus Moringe ni mtu mwenye uzoefu wa muda mrefu katika masuala ya usalama.
No comments:
Post a Comment