Hii ni sehemu ya Wajumbe waliohudhuria Mkutano wa dharula ulioitishwa na Chama cha Wafanyakazi TUICO ili kupeana taarifa za mstakabali wa yaliyotokea na hatua zilizochukuliwa na Uongozi wa Shirika la Masoko ya Kariakoo.Pia katika mkutano huo Uongozi wa TUICO uliwakumbusha Watumishi wa Shirika kuwa na mshikamano wa pamoja ili kuona kuwa Shirika likzidi kupiga hatua kimaendeleo.
Kutoka kulia ni Katibu wa TUICO katika Shirika la Masoko ya Kariakoo Bibi Ester Chogero,Bwana Joseph Mweyo Mwenyekiti wa TUICO ,na Bwana Ibrahimu Masha amabaye ni Mjumbe wa TUICO Taifa kutoka Shirika la Masoko ya Kariakoo. Wote kwa pamoja wakiendesha Mkutano a Wafanayakazi jana mchana. Mkutano huo ulilenga kujadili Agenda kuu mbili tuu ikiwamo Mwenendo mzima wa Watumishi wa Shirika pamoja na Kuwajulisha Wafanyakazi kuhusu zoezi la bomoabomoa amabalo ililikumba Shirika wiki iliyopita.
Aliyesimama ni Katibu Mkuu wa TUICO Bibi Ester Chogero akisoma waraka maalum sana amabao ulihusishwa na moja ya agenda muhim zilizojadiliwa katika Mkutano huo wa dharula ulioitishwa na Uongozi huo wa TUICO.
Viongozi wa TUICO tawi la Masoko ya Kariakoo wakishauriana jambo na Wajumbe wa Menejimenti ya Shirika la Masoko ya Kariakoo. Hii ilikuwa ni jana Jumatano ilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Shirika hilo.
Wafanyakazi wa Shirika la Masoko ya Kariakoo wakitoka nje baada ya mkutano wa Dharula ulioitishwa na Chama cha Wafanyakazi TUICO Tawi la Masoko.Mkutano huu ulifanyika jana Jumatano tarehe 9/4/2014 mchana.
No comments:
Post a Comment