Monday, September 30, 2013

KARIAKOO SOKONI LEO


 Jipatie karoti zinazopatikana sokoni Kariakoo katika meza ya biashara ya Mr. Mtui, kama zinavyoonekana hapo pichani. Karoti zinazopatikana kwa Mr. Mtui zinatoka Lushoto Mkoani Tanga. Karoti hizi zinauzwa kwa kilo kati ya shiling 1500/=  na 2000/= unaweza kupata bidhaa hizi mara ufikapo sokoni kariakoo kwa mawasiliano yafuatayo. 0713 767038 au mtuimunguatosha@gmail.com

 Pichani ni Karoti, Tangawizi na Vitunguu swaumu vinavyopatikana katika meza ya biashara ya Nasoro Atanasi iliyopo  Kariakoo  sehemu ya chini maarufu kama "Shimoni" anapatikana kwa mawasiliano yafuatayo 0716 272720

 Njegele safi zinapatika kwa Mr. Sultan Ahamed Kindwanga kwa bei nafu sana. 
1kg Shilingi 1500/= bei hii ni kwa njegele ambazo hazijamenywa.
1kg Shilingi 3000/= bei hii ni kwa njegele zilizo menywa.
kama zinavyooneka katika picjha hapo chini.

Njegele zilizomenywa tayari kwa kupikwa, Shilingi 3000/= kwa kilo.
Simu 0713 506445 au 0782 506545

SAMAKI (Kingfish)

Mfanyabiahara wa Soko kuu la kariakoo (Ramadhani Mlekwa ) akiwa katika sehemu yake ya biashara, akiuza samaki wabichi kama wanavyoonekana hapo katika picha. Samaki hawa wanauzwa Shilingi 15000 kwa kilo moja.


Samaki (Kingfish)

Friday, September 27, 2013

MTAKWIMU WA SHIRIKA LA MASOKO YA KARIAKOO AKIWA NA MRATIBU WA MRADI WA MASOKO WAKITEMBELEA MAENEO MBALIMBALI YA SOKO !


 Monique Galvao akipokea zawaidi ya muwa kutoka kwa mfanyabiashara(wa kwanza kulia)  wakati Monique alipotembelea sehemu ya chini ya Soko la Kariakoo maarufu kama Shimoni mapema leo asubuhi. 

 Mtakwimu wa Shirika la Masoko la Kariakoo Bw. Henry Rwejuna akimuonesha ramani ya Soko la Kariakoo sehemu ya chini(Shimoni) Monique ambaye ni Mratibu wa Mradi wa Masoko (Masoko Project) kutoka Shirika la  2Seeds Network.

Henry Rwejuna akitoa maelekezo  ya namna anavyo fanya shughuli zake sokoni hapo.



Sophie Hollingsworth Mratibu wa Mradi wa Masoko akiwa ofisini kwake Sokoni Kariakoo.

 Sophie Hollingsworth (kushoto) akiwa na Monique Galvao wakiwa wamefurahi wakati wa mapumziko.

Watumishi wa Shirika la Masoko ya Kariakoo.




Wafanyakazi wa Shirika la Masoko ya Kariakoo (KMC) wakifurahia jambo kama wanavyoonekana pichani.Charles Simba (kushoto) na  Saumu Kiula


Pichani ni watumishi wa Shirika la Masoko ya Kariakoo Enock Ndumule (kushoto) na Ester Chogero wakibadilishana mawazo.

Thursday, September 26, 2013

JIPATIE VYOMBO VYA NYUMBANI

Chaguo ni lako, Je unataka kipi? Swali hili halimhusu tuu  mama au dada pekee yake! bali hata wewe baba au kaka unaweza kutembelea hapa sokoni na kununua vyombo kwa ajili ya matumizi ya familia yako! Fika ndani ya Soko kuu Kariakoo vyombo kibaoooo!!

SAMAKI: NGURU, SANGARA, TAA WANAPATIKANA SOKONI KARIAKOO, NJOO UNUNUE KWA BEI NAFUU





Pichani ni samaki aina ya Nguru wanaopatikana katika meza ya biashara ya Jamary Bakari Sokoni Kariakoo jijini Dar es Salaam, Nguru wanaoonekana pichani wamevuliwa katika bahari ya Hindi.Samaki hawa wanauzwa kwa Shilingi 25000 kwa kila mmoja kwa bei ya leo.

Hawa ni Sangara ambao wanavuliwa ziwani Victoria (Mwanza) pia wanauzwa Sokoni Kariakoo

Hawa ni Samaki aina ya taa ambao wanavuliwa katika bahari ya Hindi,pia wanapatikana hapa sokoni Kariakoo kwa wingi.


Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wauza Dagaa na Samaki Wakavu (UWADASA) Bw. Mahafudh Magoma akiwa katika biashara yake ya kuuza samaki katika Soko la Kariakoo (Shimoni)

Tuesday, September 24, 2013

Katibu Muhtasi


Katika picha hapo juu anayeonekana  ni Dada Lilian Orongai ambaye ni katibu Muhtasi wa Shirika la Masoko ya Kariakoo.(KMC)  katika Idara ya Fedha na Biashara.


Monday, September 23, 2013

Mchambuzi TEHAMA (ICT Analyst)


Katika picha ni Frank Mangowi  huyu ni  Mfanyakazi wa  Shirika la Masoko ya Kariakoo (KMC); kutoka katika Kitengo cha ICT akiwa ofisini kwake akiendelea na shughuli zake za kila siku.
Anayo furaha kukukaribisha kutembelea Blog ya kariakoo ili uweze kujipatia habari mbalimbali kuhusu bidhaa kadhaa wa kadhaa

Saturday, September 21, 2013

KARIBUNI KARIAKOO SOKONI UJIPATIE BIDHAA BORA.

Picha ikionesha bidhaa mbalimbali kutoka pande mbalimbali za Tanzania

Friday, September 20, 2013

AFISA MTUNZA KUMBUKUMBU WA SHIRIKA LA MASOKO YA KARIAKOO (KMC) Charles Anthony Simba

Mr. Charles Simba akiwa ofisini kwake hivi karibuni, akiendelea na shughuli za kuhifadhi kumbukumbu za Shirika la Masoko ya Kariakoo (Kariakoo Market Corporation )
CHARLES ANTHONY SIMBA

Thursday, September 19, 2013

URASA & KIBA INVESTIMENT Wauzaji wa Viungo vya Pilau nk.

URASA & KIBA INVESTIMENT Wauzaji wa viungo vya chakula,
Karibu dukani kwa Mr. Urasa ujipatie bidhaa mbalimbali kama vile tea masala, viungo vya pilau, mdalasini wa unga, tangawizi na kadharika


URASA & KIBA INVESTIMENT 
Duka linalouza viungo vya chakula Kariakoo Sokoni

Karibu dukani



                                           Muuzaji akionesha baadhi ya bidhaa zinazopatika na ndani ya URASA & KIBA INVESTIMENT

Muuzaji akionesha baadhi ya bidhaa zinazopatika na ndani ya URASA & KIBA INVESTIMENT
tunapatikana kwa namba 0785 804202

BORESHA AFYA YAKO KWA MATUNDA SAFI TOKA KARIAKOO

Watu wengi hawapendi kula matunda kwa hiari, baadala yake mpaka asukumwe ama aaigizwe kufanya hivyo na Dakitari, ndugu msomaji jali afya yako kwa kula tikiti maji zinazopatikana Sokoni Kariakoo kwa bei nafuu, usingoje uumwe ndipo ule!
Tikiti maji

SAUMU KIULA:

Pichani ni Saumu Kiula ni miongoni mwa wafanyakazi wa Shirika la Masoko ya Kariakoo.


                                                                     Saumu Kiula

Afisa Utuzaji Kumbukumbu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo  Charles Anthony Simba akiwa ofisini kwake hivi karibuni akitekeleza wajibu wake.

Utambulisho.

Mwakilishi wa Shirika la 2Seeds Monique Galvao (kushoto) ambae pia ni Coordinator wa Masoko Project   kwa Shirika la Masoko ya Kariakoo akizungumza na mmoja wa washindi wa shindano lliloandaliwa na Shirika hilo la 2Seeds. Galvao pamoja na Sophie Hollingsworth (huyupo pichani) ambao ni wakilishi wapya katika Shirika la Masoko la Kariakoo jijini Dar es salaamu.
Monique Galvao (kushoto) akiwa na Ekyarisinna Carolyue miongoni mwa washindi wa Masoko Challange.

Tuesday, September 10, 2013

NGUVU YAKO NI MTAJI!

Jamaa mmoja ambaye jina lake halikufahamika mapema, akiwa amebeba gunia la vitungu lenye uzito zaidi ya 100Kg za vitunguu linalouzwa kwa Sh. 90,000/= akitoka nje ya lango kuu la kutokea sokoni maarufa kama "Shimoni". ndani ya soko kuu la Kariakoo jijini Dar es salaam